Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Naibu Spika, natoa shukurani zangu za dhati kwako kwa kinipatia fursa hii ya kuchangia katika hotuba hii ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Pili, napenda kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kutayarisha na hatimaye kuiwalisha katika Bunge lako tukufu kwa umakini mkubwa na kwa ufasaha wa hali ya juu kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi katika kutoa mchango wangu kwa Wizara hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo; kwanza ni kuhusu Jeshi la Kujenga Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jeshi la Kujenga Taifa ni kitengo muhimu sana katka nchi yetu, ni kitengo kinacholea vijana na kuwaelekeza namna bora ya kuishi katika nchi yetu na katika jamii kwa jumla. Jeshi hili ni lina vitengo muhimu sana katika maisha ya kiuchumi na kuwawezesha wananchi kiuchumi, kwa mfano uvuvi, mifugo na kilimo. Jeshi hili lina wataalam wa kutosha katika maeneo hayo. Aidha, maeneo hayo yanahitajika sana na wananchi wa maeneo hayo huku uraiani ili kuweza kujikwamua kiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu kwa Wizara na Serikali kwa jumla ni kuushusha utaalam huu kwa raia kwa kuwaelimisha namna ya kuendeleza miradi hii.

Kuhusu makazi ya wanajeshi, napenda kuipongeza Serikali yetu kwa namna inavyochukua juhudi kubwa ya kuwawezesha wanajeshi wetu katika maeneo kadhaa ili kuwafanya wanajeshi wetu kuweza kufanya majukumu yao ya kila siku. Lakini wanajeshi wetu bado wanakabiliwa na tatizo dogo la makazi. Wanajeshi wetu kama binadamu wengine wanahitaji mambo yote ya kimsingi (chakula na makazi). Serikali inachukua jitihada kubwa kwa kuwapatia chakula cha kutosha na bora. Lakini bado wanajeshi wetu makazi yao hayaridhishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, bado katika maeneo kadhaa wanajeshi wetu wanafanyakazi makambini lakini wanalala uraiani. Hii ni hatari kwa usalama wa wanajeshi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu kwa Serikali kuendelea kuchukua juhudi za makusudi ili kutatua tatizo hili la makazi kwa wanajeshi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.