Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, natoa shukurani zangu za dhati kwako kwa kinipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba hii ya Wizara ya Kilimo. Wizara hii ni miongoni mwa Wizara muhimu sana katika nchi yetu.

Pili nampongeza Mheshimiwa Waziri wa Wizara hii pamoja na watendaji wake wote kwa kutayarisha na hatimaye kuiwakilisha katika Bunge lako Tukufu kwa ufasaha na umakini mkubwa. Hotuba hii ni imesheheni mambo ambayo kwa sasa yanahitajika katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia maeneo yafuatayo, nikianza na umwagiliaji na ushirika.

Mheshimiwa Spika, napenda kuipongeza kwa dhati Serikali yetu kwa namna inavyochukua jitihada kubwa katika kuboresha kilimo katika nchi yetu. Kama inavyojulikana kuwa kilimo ni uti wa mgongo katika nchi.

Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri imetaja namna inavyoendelea kuchukua juhudi za kutengeneza maeneo ya unwagiliaji katika nchi yetu. Hivyo imeonesha kuwa kuna engezeko la hekta 330 kutoka mwaka 2020 mpaka 2021.

Mheshimiwa Spika, hotuba imeonesha kuwa mwaka 2020 ilikuwa na hekta 694,715 na mwaka 2021 ni hekta 695,045 za umwagiliaji; sawa na ongezekko la hekta 330.

Mheshimiwa Spika, hili ni ongezeko dogo sana ukilinganisha na umuhimu wa kilimo katika nchi yetu. Aidha, ni ongezeko dogo sana ukilinganisha na ukubwa wa eneo la ukubwa wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu kwa Serikali ni kuongeza juhudi kwa kasi ya zaida kuongeza maeneo ya umwagiliaji.

Pili ni upatikanaji wa pembejeo; wananchi wa Tanzania wanajitahidi sana pamoja na watendaji wa Wizara hii ya Kilimo kutaka kufikia malengo yao ya kimaisha kupitia kilimo. Lakini juhudi hizi zinakwama kutokana na matatizo makubwa ya pembejeo na zana za kilimo. Bado kuna ukakasi mkubwa wa upaikanaji wa pembejeo. Wakulima wanapata shida kupata pembejeo katika maeneo yao.

Aidha, wakulima wetu wanapata shida na wanashindwa kumudu kununua zana za kisasa za kilimo. Bado upatikanaji wa zana hizo ni jambo ambalo ni gumu kwa wakulima wa kawaida. Mfano Serikali ina lengo la kuwatoa wakulima kutumia jembe la mkono, lakini mpaka leo bei ya trekta moja ni kubwa sana kiasi ambacho sio rahisi kwa wakulima wa hali ya chini ambao ni kundi kubwa katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu kwa Serikali kuhusu jambo hili ni kuangalia namna ya kuboresha upatikanaji wa pembejeo na urahisi wa bei za zana za kilimo.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.