Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023

Hon. Juma Hamad Omar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ole

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023

MHE. JUMA HAMAD OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunipa fursa hii adhimu kuwa ni mmoja wa wachangiaji wa jioni ya leo. Mheshimiwa Naibu Spika na Mheshimiwa Spika nyote mmekuwa mkitulea vizuri sana katika Bunge hili mpaka kufikia kiasi cha kusema Mheshimiwa Spika anataka Bunge hili lifanye mageuzi katika kilimo. Nasema hilo ni jambo zuri kwa sababu kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini wewe umekuwa mlezi wetu mkubwa sana kwa maana ya kujadili kwa mujibu wa kanuni na sheria tulizojiwekea. Siku zote huwa ninakuita dictionary wa kanuni kwa hiyo, nakupongezeni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Rais wetu, Mheshimiwa Suluhu Hassan. Kwa kweli, kama kuna Rais ambaye ametu- encourage, ametunyanyua nchi hii, yeye ni mmojawapo. Na ninasema hivi kwa sababu, bado amebaki na adhma au na dhima ya kujenga uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya watu. Na hivi karibuni ameonesha kwamba, kweli anajali, amefanya mambo mengi ambayo nitayataja as I go through my speech, kwa hiyo, kwa kweli, tunampongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Mchemba mmoja katika Waziri ambao kwa kweli, nimebahatika kufanya kazi na Mawaziri wa Fedha muda mwingi sana nikiwa kama Naibu wao, lakini kama kuna Waziri wa Fedha aliyekuwa msikivu, hayuko adamant, yuko dactyl naweza ukampa mawazo na akayakubali, sisemi atakubali yote asilimia 100, lakini ni mwepesi wa kukubali yuko dactyl nakupongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nataka nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Mwenyekiti wetu wa Kamati, Daniel Sillo, kwa kweli, ni Mwenyekiti mzuri sana. Kamati hii imeuchambua mwongozo huu wa mpango na imekuja na mapendekezo mazuri. Kwa hiyo, ni matumaini yangu kwamba, Mheshimiwa Waziri wa Fedha utayachukua mapendekezo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hivyo nataka niseme hivi, Kamati yetu ya Bajeti, nikiwa ni mmoja katika Wajumbe, imechunguza hali ya uchumi katika kipindi pre-covid na katika kipindi post-covid na tumeona mengi sana na tumependekeza mengi. Mmoja katika wachangiaji hapa, Dkt. Kimei amesema kwamba, Sera ya Riba ambayo inakuwa determined na Bank of Tanzania ni moja katika kigezo kikubwa cha kukuza uchumi au cha kufufua uchumi, nasema ni sawa kabisa ametueleza vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nijikite katika suala la ujazi wa fedha, money in circulation ambayo inakwenda sambamba na hii sera ya, au hii tune dhana ya kuchochea uchumi kwa maana ya riba aliyoitaja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, over some time now ujazi wa fedha umekuwa ukipungua, money in circulationa. Na kwa tafsiri pana wale wataalam wanasema M3 na ni kweli, ukienda mwaka 2019/2020 ujazi wa fedha ulikuwa kwa asilimia 10, lakini unakwenda mwaka 2020/2021 lengo lilikuwa asilimia 10, lakini ujazi wa fedha umekuwa kwa 7.6. Hii ni dhahiri kwamba, money in circulation, pesa ile inayozunguka imepungua, lakini unajiuliza kwa nini? Nadhani hilo ndio la msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazungumza kwamba, private sector ni engine ya uchumi, engine ya kuchochea uchumi. Private sector hawana fedha za kuzungusha na kwa nini hawana fedha, nitakuja. Lakini sababu kubwa zilizotolewa ni tatu kwa nini money in circulation inapungua; moja ni shughuli za uchumi hasa katika sekta ya biashara, katika sekta ya utalii na katika uwekezaji katika private sector zimepungua. Na kwa nini zimepungua? Nadhani nakuja hapo, kuna hizo sababu tatu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kimsingi ni kwamba, private sector ambayo ndio engine ya kufufua uchumi haina access kubwa na na mikopo. Wengi hawa wanashindwa kwenda kwenye commercial banks wakakopa, wanashindwa kwa sababu interest ambazo zilikuwa zinatolewa na commercial banks despite the fact kwamba, BOT na Mama Samia hapa amefanya mambo mengi. Hawa commercial banks wengi hawafikiki katika kutoa. Sisi Wabunge ni mashahidi, sisi Wabunge tunajulikana address zetu zinajulikana, lakini tunachukua mikopo yetu at an interest rate of 15%, 16%. Hawa private sector wanapewa zaidi ya hapo, nasema hilo ni tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiwa ujazi wa fedha unapungua hilo ni tatizo maana ili fedha izunguke yule tajiri anataka awe na fedha nyingi na masikini basi humohumo anauza mazao yake naye atapata fedha, lakini kama haizunguki, kama fedha haizunguki tutauwa na matatizo tu. Kwa hivyo, nasema pamoja na kwamba, Mama yetu Rais ametusaidia sana, kwa mfano hivi karibuni katoa 1.1 billion kawapa Benki Kuu ya Tanzania. Kama hiyo haitoshi, juzi katusaidia amepata 1.3 trillion zote hizo zitatiwa ziende zikapunguze suala la ujazi wa fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo nasema pamoja na mambo mazuri anayotufanyia Mheshimiwa Rais wetu, lakini bado money in circulation ujazi wa fedha umekuwa ni tatizo. Kwa hiyo, ninapendekeza yafuatayo, ili kukabiliana na suala hili la ujazi wa fedha:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tu-encourage PPP (Public Private Partnership). Hivi tujiulize tokea sheria hii ipite ya PPP ni miradi mingapi ambayo imefanywa kwa njia ya ubia? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani kama sikosei ni Daraja la Kigamboni basi, Daraja la Kigamboni. Na Kigamboni pale ni private, lakini kwa maana ya shirika letu la hifadhi NSSF, lakini hakuna jitihada ambazo zimeelekezwa ku-encode PPP. Sasa hilo ni tatizo na ninadhani PPP katika ulimwengu huu ina play part kubwa, hasa katika miradi ambayo ni capital intensive; mradi kama wa SGR, mradi kama wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, mradi kama wa njia nne kutoka Kibaha mpaka Chalinze. Mradi kama ule wangepata private sector tukafanya partnership nao nadhani kwa kiasi kikubwa Serikali isingekuwa na haja ya kuwekeza fedha kama hizo kwa hiyo, nadhani hiyo ni njia moja tu-encourage PPP.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, BoT, Benki Kuu ya Tanzania, lazima pamoja na kwamba, kuna kitu Dkt. Kimei amekitaja kinaitwa Statutory Minimum Reserve Requirement, pamoja na kwamba, Benki Kuu ya Tanzania imepunguza hii Statutory Minimum Reserve Requirement, lakini hii haisaidii. Inasaidia kuhakikisha benki zetu endapo zitapata matatizo zinaweza kurejesha fedha za watu kwa sababu benki haina fedha zake, benki inakusanya amana na kuna benki nyingi kwa mfano Greenland Bank kuna wakati ilifilisika kwa hivyo, Benki Kuu ikatakiwa irejeshe amana pale ikarejesha. Kwa hivyo, hii haimsaidii mtu binafsi wala haiwasaidii watu wa private sector, zaidi inasaidia kuhakikisha kwamba, benki zetu ziko liquid at a given time.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la tatu ninalopendekeza ni kwamba, lazima tukataka tusitake, private sector iende ikafanye kazi hasa katika miradi ile kwa PPP kama tulivyosema, lakini kuna kuna miradi kwa mfano, nitawapa mfano; mradi wa Mchuchuma na Liganga, mradi wa Liganga, chuma cha Liganga na makaa ya Mchuchuma. Hii miradi kama sisahau mradi wa Liganga umekuweko tokea miaka ya 1990s, mimi niko Bungeni wakati huo, Mheshimiwa Kihaule, if I can remember very well alikuwa anauzungumzia mradi huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini so far mradi huu huwezi kuamini, so far mradi huu nafikiri umetumia only shilingi 5.7 billion huu ni LNG, Mchuchuma nafikiri umetumia kidogo zaidiā€¦

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Juma. Mda wako umekwisha.

MHE. JUMA HAMAD OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, haya. Kwa sababu muda hauniruhusu naomba kuunga mkono hoja zote hizi. (Makofi)