Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuanzia Januari, 2021 hadi Februari, 2022 pamoja na Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kwa Kipindi cha Januari 2021 hadi Januari 2022

Hon. Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuanzia Januari, 2021 hadi Februari, 2022 pamoja na Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kwa Kipindi cha Januari 2021 hadi Januari 2022

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na mimi nichukue nafasi hii kukupongeza sawa na watangulizi waliopita kwa nafasi hii muhimu na nyeti katika Bunge letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa nijikite kwenye suala la Liganga na Mchuchuma maana ni jambo ambalo limekuwa kizunguzungu kwenye Kamati yetu, tunaona tangu tumeingia ni hadithi zimekuwa nyingi, sasa nikasema nijaribu kufanya utafiti wangu kidogo ili nijue ni nini kinakwamisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika miradi ya kimkakati ambayo imetajwa katika mpango wetu wa mwaka huu 2021/ 2022 ambao uliwasilishwa mwezi Machi, 2021 miongoni mwa miradi muhimu ambayo ilitajwa ilikuwa ni mradi wa Liganga na Mchuchuma, lakini mpaka leo ni miezi sita imepita, tunategemea kupokea mpango mwingine mwezi wa Machi mwaka huu lakini ninachosema ni kwamba hatuna kilichofanyika mpaka sasa, siyo pesa ni hadithi tu vitu vyote vimebaki kama vilivyokuwa vimewasilishwa pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lazima tujaribu kujikita kuona tatizo ni nini, maana huu mgodi umeongelewa kwa muda mrefu na ni mgodi wenye manufaa sana katika nchi hii lakini hakuna ambacho kinafanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuangalia hii kampuni ya Sichuan Hongda ambayo ndiyo mkandarasi, nimejaribu kufuatilia nikajua hawa watu wanachokwama ni nini. Katika ripoti ambayo tumepewa na NDC inaonekana hata teknolojia yenyewe ya kuchenjua madini haya kwa sababu madini ya chuma yapo na vanadium, yapo na titanium, teknolojia yenyewe kaja nayo huyu Mkandarasi ambaye tumepewa. Kwa hiyo kwa upande mkubwa hata Taifa hatukuwa tumejiandaa kwa sababu hatukujua hata uchenjuaji hata hiyo process itafanyika vipi.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuangalia zaidi, huyu Sichuan Hongda anachokifanya ana-deal na Zinc, Zinc Oxide products ana-deal na mbolea na vitu vingine, he has never done any product on ferrous metal kabisa! Anavyo- deal navyo ni non-ferrous metal, ambapo tutakuta titanium, tutakuta na vanadium lakini chuma ambayo ndiyo product hakuna profile inayoonesha kwamba huyu mtu amefanya. Sasa huenda anashindwa kuendelea na huu mradi kwa sababu uwezo hana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu ambao ninataka tuende nao, process hii as a chemistry process ambayo ni ya kawaida kabisa maana kuna study zimefanyika, wenzetu South Africa wanachimba chuma, Egypt wanachimba chuma, Libya wanachimba chuma, hizi ni nchi ambazo tumekuwa na ushirikiano nazo mkubwa, tungeweza hata kwenda kujifunza tukajua mtu huyu tunayemkabidhi mradi ana uwezo au hana uwezo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukijaribu kuangalia, mradi wa bilioni tatu investment kwa mwaka mmoja tunategemea tupate bilioni 1.736; kwa hiyo mwaka wa pili ile investment yote ya bilioni 3 itakuwa imerudi kwa sababu tutakuwa na 3.4 bilion, lakini mradi huu umekwama. Ungekuwa ni mradi mtu anauweza huyu mtu angeshakuja kuufanya, jambo ambalo inabidi tujiulize ni nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, China ndiyo nchi inayoongoza kwa production ya steel hapa duniani, mtu huyu anatoka China, je, kama kuna ucheleweshaji kama sehemu ya hujuma ili huu mradi usiendelee wao waendelee kufanya biashara hii? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuishauri Serikali, kwanza kwa sababu ya muda inabidi niende haraka haraka, huu mradi contract yake kwanza iwe terminated, huyu mtu hawezi na ameshindwa kufanya hii, kwa sababu hata uwezo wa vitu anavyovifanya hauendani na chuma ambayo tumeitafuta wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine tumeona upande wa TPDC, tumeona na sehemu nyingine wanapeleka vijana wao kusoma, leo tuna watalaam wa gesi hapa, tuna watalaam wa petroli hapa, lakini tunapokuja kwenye chuma hata tukiwauliza watu ile content yenyewe ya hii chuma ya Liganga na Mchuchuma kuna nini? Chuma ni asilimia ngapi, hiki ni asilimia ngapi, mtachenjua vipi? Wanakuambia yule mwekezaji ndiye anayekuja kuangalia njia ya kuchenjua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama inawezekana Serikali ijikite kuwezesha vijana wa Kitanzania sawa na tulivyowekeza kwenye petroli, sawa na tulivyowekeza kwenye gesi, tuwekeza kwa vijana wa Kitanzania wakasome material specifically kwa ajili ya material, wakirudi hapa watakuwa wanajua hata hizo process za uchenjuaji ni chemistry ya form two, lakini watu wetu hawajawezeshwa! Kama hawajawezeshwa huyu mtu anatupiga chenga kila siku, kwa hiyo kwa sababu ya muda ninapenda niishie hapo na ninaunga mkono hoja kwamba huyu mtu aondolewe tutafute mwekezaji mwingine ambaye atalisaidia Taifa. Ahsante sana. (Makofi)