Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuanzia Januari, 2021 hadi Februari, 2022 pamoja na Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kwa Kipindi cha Januari 2021 hadi Januari 2022

Hon. David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuanzia Januari, 2021 hadi Februari, 2022 pamoja na Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kwa Kipindi cha Januari 2021 hadi Januari 2022

MHE. DAVID M. KIHENZILE – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa nafasi hii ili niweze kuhitimisha hoja ya Kamati yangu, lakini na mimi niungane na Wabunge wenzangu kukupongeza kwa ushindi mkubwa ulioupata kwa nafasi ya Naibu Spika wetu. (Makofi)

Niwapongeze na kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge waliopata nafasi ya kuchangia kwenye hoja yangu, kwa uchache Mheshimiwa Cecil Mwambe, Engineer Ezra Chewelesa, Mheshimiwa Maryam Omar Said, Mheshimiwa Deo Mwanyika, Mheshimiwa Juma Usonge, Mheshimiwa Humphrey Polepole, Mheshimiwa Neema Lugangira, Mheshimiwa Nusrat Hanje, Mheshimiwa Exaud Kigahe, Mbunge na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara na Mheshimiwa Dkt. Suleiman Jafo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja mbalimbali zimezungumzwa katika kuchangia kwenye hoja zetu, lakini pamoja mambo mengine kwa kirefu sana imezungumziwa hoja ya Liganga na Mchuchuma.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hoja zingine tunaamini Serikali imechukua na kwa uzito mkubwa itakwenda kufanyia kazi hoja hizo kwa maslahi makubwa ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba Bunge lako Tukufu sasa lipokee na kukubali maoni ya Kamati yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.