Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia hoja ya Kamati yetu ya LAAC, mimi ni Mjumbe wa LAAC ya taarifa yetu ya mwaka ya ukaguzi wa fedha.
Mheshimiwa Spika, kwanza napenda nichukue fursa hii kukupongeza mimi nimeulizwa maswali mengi kwamba, kura nilimpigia nani nikasema mimi nampigia mwanamke lakini mwanamke mwenye uwezo. Kwa hiyo, kura yangu haipigwi holela, kwa hiyo nakupongeza sana Mungu akubariki, ubarikiwe sana. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Spika, halmashauri hizi zina kazi kubwa. Kazi yake kwanza ni kutoa huduma kwa wananchi, lakini pia, halmashauri hizi zinatekeleza maagizo, sera, maelekezo ya Serikali Kuu. Ukiyatazama majukumu hayo ni majukumu makubwa ambayo yanataka udhibiti na usimamizi mkubwa na udhibiti huu unapaswa ufanywe ndani ya halmashauri zenyewe, lakini pia kupitia Serikali Kuu, Wizara ya TAMISEMI lakini pia na hata Sekretarieti za Mikoa chini ya RAS na Mkuu wa Mkoa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Kamati yetu ya LAAC tunafanya kazi ya uchambuzi wa taarifa za CAG lakini mengi tumeyaandika katika taarifa yetu, lakini hatuwezi kuandika maneno yote, kuna mengine ambayo tutachangia kidogo kulingana na muda.
Mheshimiwa Spika, nitaongea kuhusu miradi inayotekelezwa kwa mfumo wa force account. Force account ni kitu kizuri sana, Serikali inatekeleza miradi yake kwa bei nafuu na tunapata miradi mingi ambayo inatekelezeka. Ipo miradi ambayo inatekelezwa na force account ambayo sio mizuri na sio imara ambayo inaleta hofu kwamba, inawezekana huko mbele baada ya miaka fulani tunaweza kuleta crisis za majengo haya kutoendelea kutumika vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali kwamba ifikirie sasa kuwa na ukomo wa kiwango cha fedha zitakazotumika katika force account. Kwa mfano, tulikwenda kutembelea Mradi wa Machinjio kule Vingunguti katika Wilaya ya Ilala Dar es Salaam; wanao mradi mzuri sana ambao umetekelezwa kwa zaidi ya Shilingi bilioni 12, lakini wameweka mkandarasi ambaye ni National Housing Corporation. Kwa hiyo, unaweza kuona ule mradi ulitekelezwa kwa sababu una fedha nyingi na waliweka mkandarasi ndio aliweza kutekeleza. Kwa hiyo, miradi kama hii haiwezi kutekelezwa kwa force account. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ni vyema Serikali iweze kutenga kwamba fedha hizi kama mwisho ni Shilingi bilioni tano iende kwa force account; na kama ni zaidi ya hapo basi wasiogope kuweka wakandarasi ili kuwe na ufanisi wa miradi. Nayasema hayo kwa sababu gani? Ukienda katika miradi hii ambayo inatekelezwa kwa force account, zipo Kamati za Ujenzi, Kamati hizi zina watu ambao sio wataalam hata kidogo ni wachache. Hakuna ma-engineer katika halmashauri, kwa hiyo, unakuta hizi kazi zinafanywa bila kuwa na usimamizi ambao unaleta ufanisi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, napenda niishauri Serikali kwamba sasa umefika wakati kwa vile hatuna ma-engineer, basi kuwepo na Mpango, wa kufundisha watoto wetu kupitia VETA tupate technicians ambao wanaweza kwenda kufanya kazi hizi katika ngazi za chini. Kwa sababu, kule tumegundua kwamba wakati mwingine wana-pick Walimu tu, mtu yeyote ambaye anajua kuweka tofali tu, wala hajawahi kujenga chochote katika maisha yake ambacho ni mradi wa kudumu.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunashauri Serikali itazame ni namna gani ya kuweza ku-train technicians, wapo vijana ambao wamemaliza form six wamechukua masomo ya kisayansi. Wanaweza kupelekwa wakafundishwa, yaani huo ni mpango mkakati halafu tukawaajiri vijijini kule, wakaenda kusaidia katika kusimamia majengo hayo. Pia waajiri ma-engineer, halmashauri haina ma-engineer, ma- engineer wote walihamia TARURA, kutoka halmashauri kwa sababu TARURA wana package nzuri za mishahara. Kwa hiyo, ni vyema tukahakikisha kwamba ma-engineer wanaajiriwa sambamba na ma-technicians, ambao wanaweza kusaidia kazi hizi zikaendelea kule vijijini na sehemu nyingine. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nikimaliza hiyo nije kwenye Mfuko wa Wanawake pamoja na kwamba muda ni mfupi. Mfuko wa Wanawake ni Mfuko mzuri sana na nimekuwa nikiusema kwamba una malengo mazuri sana ya kusaidia vijana wetu kusaidia wanawake na watu wenye ulemavu. Hata hivyo, ukiangalia katika ripoti ya CAG ya mwaka, 2019/2020 amesema, fedha ambazo zimekopeshwa ni zaidi ya Shilingi bilioni 27, hazijarejeshwa. Jana Mheshimiwa Kimei aliuliza swali Na. 136 ambalo alitaka kuona ufafanuzi wa fedha hizi, katika miaka mitatu mfululizo na nashukuru kwamba TAMISEMI walitoa taarifa na nafikiri ni latest. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwamba mwaka, 2018/2019 halmashauri zote Tanzania nzima zilikopesha Shilingi bilioni 42.06; mwaka, 2019/2020 Shilingi bilioni 40.73; mwaka, 2020/ 2021 Shilingi bilioni 51.81. Fedha zilizorudishwa katika fedha hizo ambazo ni Shilingi bilioni 135 ni Shilingi bilioni 48 tu. Kwa hiyo, unaweza kuona taswira ikoje ya fedha hizi kama tunaweza kuwa na zaidi ya Shilingi bilioni 50 kwa miaka mitatu mfululizo, ziko hazijarudishwa, ina maana hizi fedha ambazo ni fedha za walipakodi, ambazo ni fedha za watu wanaochanga ndani ya halmashauri hazirejeshwi, taswira ya Mfuko huu ni nini hasa inacholenga. (Makofi)
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
SPIKA: Ahsante.
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Spika, naona dakika tano ni kidogo naomba kuunga hoja Kamati hii. (Makofi)