Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

Hon. Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

MHE. GRACE V. TENDEGA – MWENYEKITI WA KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, nakushukuru sana wewe na wote waliochangia hoja hii na Mawaziri wote ambao wamechangia kwa namna moja au nyingine katika kujibu hoja hizi. Nawashukuru sana kwa sababu wameunga mkono hoja zote za Kamati ambazo tumezitoa na ndiyo maana tulizitoa katika maoni yetu na pia nimepokea pongezi zenu zote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wengi wamejikita kujengea tu hoja zile namna ya kutoa maelekezo, basi nitambue michango ya waliochangia katika Kamati yetu ya LAAC. Kwanza Mheshimiwa Selemani Zedi, Mheshimiwa Twaha Mpembenwe, Mheshimiwa Ali Kasinge, Mheshimiwa Conchesta Rwamlaza, Mheshimiwa Tauhida Gallos Nyimbo, Mheshimiwa Abubakari Asenga, Mheshimiwa Francis Mtinga,

Mheshimiwa Japhet Hasunga, Mheshimiwa Anastazia Wambura; na Mawaziri, Mheshimiwa Dkt. Festo Dugange na Mheshimiwa George Simbachawene, tunawashukuru kwa michango yenu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, yale yote ambayo wameyasema, basi tunaomba yakawe katika utekelezaji kwa sababu tunafanya kazi kwa mujibu wa taarifa ya CAG. Kwa hiyo, tunashukuru sana kwa yale ambayo wameji-commit lakini katika mifumo, lakini kama alivyoeleza Mheshimiwa Naibu Waziri Dkt. Festo Dungage tuwaombe basi Ofisi ya Rais, TAMISEMI mharakishe kuleta mifumo kama huo mfumo wa tausi ili kuweza kudhibiti hizo fedha ambazo zinatumika fedha mbichi. Hii itasaidia Serikali iweze kupata mapato ya kasaidia wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia hii ya kufuata miamala, mmesema mtaangalia ile bureaucracy the way ilivyo kuhakikisha Maafisa Masuhuli wanakuwa responsible, itasaidia sana kwa sababu yeye ndio accounting officer atatusaidia kuweza kuona kwamba fedha zile zinakuwa katika mikono salama.

Mheshimiwa Spika, upungufu wa watumishi na watu wengine kama walivyosema Waheshimiwa wa Bunge katika kuchangia kwao, Serikali iweze kutoa mafunzo kama tulivyosema katika taarifa yetu, itasaidia sana watendaji kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kuongeza mapato.

Mheshimiwa Spika, kuhusu 10%, hilo tunaomba Serikali iweze kufanyia kazi kwa umadhubuti kabisa kwa sababu fedha zile zikirudi kuna baadhi ya Halmashauri zitakuwa zimefikia ukomo wa kutenga tena; na zile fedha zitatosha kuwakopesha wananchi wetu wengi zaidi wakaweza kunufaika.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba kukushukuru na nishukuru watendaji wote wa meza yako.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Spika, naafiki.