Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Hesabu za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021

Hon. Geoffrey Idelphonce Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Masasi Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Hesabu za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021

MHE. GEOFFREY I. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, napenda kushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia na mimi hoja tatu ambazo zimewekwa mbele yetu lakini kipekee nitajikita kwenye hoja zilizoletwa na Kamati ya PAC.

Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi kubwa anazozifanya za kuhakikisha kwamba tunatoa huduma bora kwa wananchi wetu na kuzingatia value for money kwenye miradi yetu, lakini tunaongeza makusanyo na kuboresha hali ya wananchi.

Mheshimiwa Spika, naichukulia hali ya ukaguzi uliofanywa kwenye taasisi lakini pia na Wizara kama huduma ambayo CAG anaitoa kwa Bunge. Na ninachukulia kwamba sisi Wabunge ni Madaktari na tumemuomba CAG atuangalizie mgonwa ambae ni Serikali na CAG yeye ni mtaalam wa Maabra. Baada ya ukaguzi wa damu, CT scan mRI akatuletea matokeo na matokeo ambayo ametuletea Kamati inawasilisha kwenye Bunge kama jopo la Madaktari ili tuweze kujadili na kutoka na maazimio ya ni namna gani mgonjwa wetu atatibiwa.

Mheshimiwa Spika, tumesikia hoja za wajumbe mbalimbali lakini pia za Mwenyekiti wetu wa PAC kuhusiana na yale tuliyoyabaini kwenye majadiliano yetu na CAG pia na taasisi husika. Kuna changamoto nyingi tumeziona lakini ninaweza kuzipanga katika maeneo matatu au manne.

Mheshimiwa Spika, eneo la kwanza ni mikataba. mikataba mingi ambayo inaonekana imesainiwa inatugharimu mabilioni ya pesa kama Taifa. Ukiangalia kwa mfano bilioni 355 ambazo tunaenda kuzilipa kwa Symbion, ukigawa milioni tano tano kwa wanafunzi wetu wa vyuo vikuu, tungeweza kuwahudumia wanafunzi 71,715 kwa kuwapa mikopo; lakini hiyo tunakwenda kuwalipa Symbion tu kwa mkataba wa awali ambao kimsingi ulisainiwa under emengency power plan, mwaka 2006/2007. Vile vile bado ukaongezwa mwaka 2008 ukasogwezwa ukatuletea matatizo.

Mheshimiwa Spika, tumeona kuna vihenge. Kuna mkataba wa ujenzi wa vihenge, kuna Mkataba wa Aurial ambayo ni kampuni ya Philips ambayo iko kule Uholanzi ya ku-supply vifaa vya tiba. Kuna mikataba mingi ambayo imetusababishia hasara ya fedha nyingi. Pia kuna mikataba mingine mingi ambayo hatujaiona, na labda baadhi ya wabunge hawajaiona.

Mheshimiwa Spika, tunayo pia mikataba ambayo tunatakiwa tulipe kama current liabilities, kama madai sasa ni trilioni 1.7 kwa TANESCO kutokana na kesi mbalimbali zinazotokana na uzalishaji wa umeme, usamabazaji na matumizi yake, ambako kuna kampuni tatu zinatutadai ikiwemo kampuni maarufu IPTL kupitia Standard Chartered Bank Hong kong.

Mheshimiwa Spika, Kwa hiyo ukingalia mikataba mingi ambayo tu nayo inatunyonya sana kuliko kutusaidia kama nchi, na inatumika kama conduit, ni kama vile tumechukua tenga tunaenda kubeba maji; ambazo ni fedha, halafu yanadondoka nje kwa sababu tu hatujaweza kuziba mianya kupitia mikataba.

Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria na unafahamu uandaaji wa mikataba. Ni kesi chache sana ambazo Serikali imewahi kushinda kwenye mabaraza ya usuluhishi au Mahakama, kesi chache sana. Nafikiri wengi watakumbuka City Water ndiyo ambayo tumewahi kushinda, lakini kesi zingine zote tunashindwa, hata pale ambapo mwekezaji au mtoa huduma hajatimiza masharti yake lakini bado sisi tunashindwa kwenye hizo kesi na kulazimika kulipa mabilioni ya fedha za Serikali. Baadaye tunahangaika Kwenda tunaenda kukopa, kuweka tozo, kuwabana wajasiliamali wetu na kuwabana wafanyabiashara walipe kodi, pesa ambazo kimsingi tumeshindwa kuzilinda.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ni manunuzi. Bahati nzuri Weheshimiwa wenzangu walizungumza hapa, akiwemo Mheshimiwa Maimuna Pathan na Mheshimiwa Deus Sangu. Upande wa manunuzi tunapoteza fedha nyingi, miradi mingi haiishi kwa wakati, ina extension na variations za kutisha.

Mheshimiwa Spika, tunafahamu na mwaka jana tulipewa taarifa hapa kwamba hata ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kufikia Novemba, 2021 ilitakiwa maji yaanze kuingia kwenye bwawa kwa miezi mitatu hadi minne na commission ingeweza kufanywa mwezi Juni, 2022. Hata sasa hapa tunavyoongea kuna extension tena ya miaka miwili sijui. Hatuelewi hiyo extension imetokana na nini na gharama ni nani analipa? Mapato ambayo tungepata kwa kuuza umeme nani atafidia? Hata kasi ya usambazaji wa umeme wa REA haiwezi kuwa kubwa kwa sababu kiwango cha umeme kinachozalishwa ni kidogo. Tulitegemea umeme huu ungeweza kuingia haraka kwenye grid. (makofi)

Mheshimiwa Spika, tunaona pia kuna madhaifu ya kiutendaji. Kuna maeneo mengi tumeona ukusanyaji wa kodi umekuwa ni mdogo. Kuna changamoto katika ukusanyaji wa kodi.

Mheshimiwa Spika, moja, mfumo kupitia Tax admiration Act si mzuri sana; na kuna systems ambazo zinakadiria kodi kubwa kuliko uhalisia na pia kuna upungufu wa utaalamu. Wako wataalamu wa upande wa kodi hata mkopo wanaupigia hesabu ya capital gain tax, matokeo yake liabilities kwa wafanyabiashara inakuwa kubwa na hawawezi kulipa, wanahangaika, wanalazimika kufanya objection tunakwenda huko kwenye TRAB na TRAT mnakokusikia.

Mheshimiwa Spika, hii yote ni kutokana na kubadilika na mfumo wa kiutendaji ambapo zamani kulikuwa na a proper tax accessor ndani ya TRA ambaye amefundishwa, ame-undergo intensive training kule TIA au sehemu nyingine ya nchi, akiwa ni mtaalaamu wa ukadiriaji wa kodi kwa sababu amebobea kwenye eneo lile na ni mtaalamu. Sasa hivi mtu yeyote tu, akikaa kule Masasi ofisini au Kalambo anakukadiria tu. Jambo hili limepelekea tax disputes nyingi na objection kuzalishwa.

Mheshimiwa Spika, ningependa sasa kuchukua muda mrefu kujielekeza kwenye mapendekezo. Naomba Waheshimiwa Wabunge mridhie mapendekezo haya ili tuweke kwenye maazimio yetu kupitia Mwenyekiti wetu wa Kamati ya PAC.

Mheshimiwa Spika, la kwanza, ninashauri; ili kuziba mianya ya mapato na matumizi ya Serikali, mikataba yote ambayo inazidi five bilioni iletwe bungeni kupitia kamati, au kamati maalumu tuweze kuihakiki na kui- approve.

Mheshimiwa Spika, la pili, mikataba yote iliyopo kwa sasa, najua kuna juhudi zilikuwa zinafanywa na Serikali kupitia mikataba mbalimbali kuweza kuihuisha, kuiboresha na kuifanya ya kisasa angalau kulinda maslahi ya watu wetu, nayo iletwe tuihakiki na kuiona kama mikataba hiyo ina maslahi na kama haina maslahi tukae mezani tuweze kuijadili upya tuweze kufanya review ya hiyo mikataba.

Mheshimiwa Spika, iko mikataba ya upande wa madini, gesi na upande wa kwenye vitalu vya utalii kule na maeneo mingine ya kimkakati. Iko miradi ya SGR, Stiegler’s gauge na upanuzi wa bandari. Tulienda Tanga, kule kuna vitu vya ajabu sana nafikiri na vingine mlivisikia, ambapo mtu amepewa tenda leo halafu kesho aka- subcontract kwa mtu mwingine kwa bei ya chini ya nusu ambayo analipwa na Serikali.

Mheshimiwa Spika, mimi napenda kushauri sana mikataba hii tuitishe upya, tuweze kuipitia na kuitengenezea frame work ili iwe mikata ambayo ina faida kwetu.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ni la adhabu na tuzo ambazo zinatolewa kwenye taasisi za usuluhishi au mahakama za usuluhishi wa migogoro ya wafanyabiashara na wawekezaji. Iko ICC Internationa Chamber of Commerce pamoja na Ixid ICSID ambako kule tunashindwa mara nyingi.

Mheshimiwa Spika, mimi nilikuwa nashauri kabla ya Serikali haijalipa chochote huko sisi tutoe azimio, Serikali ije Bungeni tukae nao na tujadiliane nao tuone hicho kinachokwenda kulipwa ni nini, kina-make sense namna gani na kama kweli tunaridhia; ili fedha ya umma inapokuwa inatoka kule sisi kama wawakilishi wa wananchi basi tuwe na taarifa nayo.

Mheshimiwa Spika, kuna tatizo kubwa sana kwenye suala la ukusanyaji wa kodi. Tumeambiwa hapa zaidi ya trioni 2.8 hazijakusanywa. Ukiangalia zile sababu kutokana na taarifa za CAG zinaonesha kwamba mfumo wa kodi wa sasa umepitwa na wakati. Aliyekuwa Waziri wa fedha wakati ule ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais, Mheshimiwa Philip Mpamgo, aliwahi kutoa mapendekezo kwamba kuna Presidential Recall Committee on Tax Systems Reforms ambayo ilifanywa mwaka 1992 chini ya Mzee Mtei na haijawahi kufanywa tena. Ili tuweze kuona fiscal policy yetu ikoje, nani tumtoze, vyombo gani, tuendelee na VAT ya asilimia 18 ilhali wenzetu ni asilimia 16 kwenye kanda. Je, mfumo wa TRA upoje? Je, bado ibaki kama ilivyo? Au idara za TRA zibaki kama thematic departments.

Mheshimiwa Spika, kwamba kama Idara ya VAT iwe Idara ya VAT, na isiwe inafanya tax payer na kufanya VAT, Domestic revenue anakusanya VAT hii inaleta mkanganyiko mkubwa sana. Kwa hiyo nilikuwa naomba sana waheshimwa Wabunge tukubaliane, kwamba tuiagize Serikali kama maazimio iweze kufanya comprehensive tax system review ili tuweze kubaini mfumo wetu wa kikodi ukoje ili tupate kodi za kutosha.

Mheshimiwa Spika, hii itatusaidia kuongeza tax effort. Tax hatujilipii ratio ambayo kwa bahati mbaya tangu mwaka 1995/1996 bado tuko asilimia 10 hadi 11. Maana yake ni makusanyo yote ya kodi kulingana na uzalishaji (tax over GDP) ambayo tuko below African average ya asilimia 18. Hii naamini itatusaidia kutengeneza mfumo mzuri na kuitengeneza compliance kubwa, watu walipe kodi wakiwa na furaha kwamba wanachangia kwenye maendeleo kwenye taifa lao.

Mheshimiwa Spika, kuna hii tabia ya Serikali kukaa na fedha za wafanyabiashara kwa sababu imeshindwa kulipa kwa wakati kutokana na zabuni au ukaguzi wa imports duty na refunds. Mimi ninasema, kama Serikali inatoza faini na penalties kwa mfanyabishara kuchelewa kulipa fedha Serikalini basi sasa kwa uwajibikaji Serikali nayo ijitoze faini na riba kwa mfanyabiashara endapo tutachelewesha malipo kwao. Kwa sababu tunachelewesha malipo kwao tuna-hold working capital zao; hili linasababisha ku-paralyze private sector.

Mheshimiwa spika, nilikuwa natamani sana, tumeliangalia sana shirika la TANESCO. Shirika la TANESCO lina mzigo mzito ambao umetokana na mfumo uliopo sasa hivi. Napendekeza tufanye upya mapitio ya Sera ya nishati ya umeme ili tufanye divestiture ndani ya TANESCO. Tunajua TANESCO inajihusiha na masuala ya uzalishaji, usafirishaji pamoja na usambazaji wa umeme, lakini tumeruhusu independent power producers kwenye uzalishaji peke yake halafu wanalazimika kumuuzia TANESCO. Kwa hiyo TANESCO hata kama hajajiandaa analazimika kununua na kuingia power purchases agreement na kutengeneza mzigo mkubwa ambao TANESCO sasa hivi tunauona.

Mheshimiwa Spika, mapendekezo yangu, kama ambavyo ilikuwa TTCL zamani tukaruhusu Vodacom, Tigo na wengine waingie, tufanye divestiture, turekeboishe sera zetu ili turuhusu na wengine waje wawekeze. Kama ni Symbion aweke mtambo wake azalishe, asambaze umeme wake, atafute wateja wake aendelee ili TANESCO iendelee kubaki salama kutokuingiziwa mzigo mzito kama ambavyo ilivyo hivi sasa.

Mheshimiwa Spika, tumeona pia suala la bodi ya mikopo. Mimi ningependa kuungana na Mheshimiwa Japhet Hasunga, alitoa pendekezo hapa jana. Napendekeza Serikali angalie uwezekano wa kuunda mfuko wa taifa wa kugharamia elimu ya juu na si bodi ya mikopo; ambao na utakuwa ni mfuko wa pamoja. Watoto wote wa Tanzania wanastahili kusoma.

Mheshimiwa Spika, nitoe mfano mmoja, nilipata bahati kipindi fulani kwenda kusoma Kijerumani CDTC center pale Koloni (Cologne) Ujerumani; tukawa na watoto wadogo kama 20 hivi tunasoma nao pale. Nikawauliza, walikuwa wanaongea kifaransa, wale Watoto wanatokea nchi ya Gabon. Serikali ya Gabon imetengeneza utatibu kwamba, kila mwaka the best science students form six wanapelekwa Ujerumani kusoma electrical engineering, mechanical engineering, civil engineering kwa gharama za Serikali for Seven-years, kila mwaka. Gabon haitakuwa sawa sawa na sisi baada ya miaka 20. Kwa nini sisi tuone hasara kuwasomesha watoto wote? Kwa nini tulazimike kumbagua huyu, sjui mzazi wake yukoje, mzazi wake hana mguu mmoja kwa hiyo tumpe.

MheshimiwaSpika, mimi ninapendekeza tuanzishe mfuko wa taifa, tutafute vyanzo, vyanzo vipo ili kila mtoto aweze kupata elimu.

Mheshimiwa Spika, tuna tatizo kubwa sana la Local content ambalo jana hata Mheshimiwa Kigwangala alilizungumza. Ni namna gani tutawawezesha watu wetu? Tunafurahia sana kuona orodha ya mabilionea wa nchi nyingine? Tunatakiwa sasa kuwatengeneza wa kwetu, tuwaamini wafanyabiashara wetu tuwatafute tuwatengeneze.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa nashauri sana Serikali ije na Local content law ili tuweze kupitisha hapa tukainisha maeneo mbalimbali ambayo tunaamiani tunaweza kuwasaidia Watanzania wetu…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Kengele ya pili imeshagonga Mheshimiwa.

MHE. GEOFFREY I. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, napenda kuunga mkono hoja, ahsante sana.