Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Hesabu za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021

Hon. Haji Amour Haji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makunduchi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Hesabu za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021

MHE. HAJI AMOUR HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, nami namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kunipa nafasi hii. Kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati nikiwa kama mjumbe niliyetoka katika Kamati ya PIC.

Mheshimiwa Spika, kuanzia juzi tumekuwa tukijadili hoja za kamati tatu, ambapo tuna hoja ya PIC, LAAC pamoja na PAC. Bahati nzuri nashukuru sana kwamba kwa kila moja amechangia au tunachangia kwa mujibu wa kuweza kuishauri Serikali; na kwa kweli tunafanya kazi ya kuishauri Serikali vizuri sana na kuweza kusema kwamba, kuishauri Serikali pamoja na kutoa mawazo ambayo kila kamati maana yake yaliyokuwa yamo.

Mheshimiwa Spika, sasa nasema kuna mambo mengi ambayo yamo katika zile ripoti, lakini mimi niweze kujielekeza zaidi katika Kamati yangu ya PIC. Kamati yetu ya PIC ni kamati ambayo ipo kama jicho la Bunge katika kusimamia uwekezaji wa mitaji ya umma. Pamoja na hayo katika uwekezaji wa mitaji ya umma suala ambalo tunalitazama, tunaangalia vitu vitatu katika uwekezaji wetu wa mitaji ya umma. Kitu cha kwanza tunachokiangalia pale ni suala la ufanisi katika mashirika yetu; tunajaribu kuangalia suala la sheria kama zinafuatwa katika hali ya utaratibu katika ile mitaji ya umma katika mashirika yetu; na vilevile tunajaribu kuangalia suala la kibiashara.

Mheshimiwa Spika, sasa katika muktadha huo kamati yetu, kupitia katika uwekezaji wetu, tuna mashirika 237 ambayo ndiyo tunayoyasimamia kupitia hazina. Sasa katika mashirika hayo 237 kuna mashirika ambayo yana hisa chache, kuna mashirika ambayo yana hisa 100 kwa 100 na Serikali na kuna mashirika kama 10 yako nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, sasa katika mashirika hayo kuna mashirika ambayo ni ya kibiashara na kuna mashirika ambayo ni ya kutoa huduma tu kama kawaida, lakini yote yanatumia fedha za Serikali. Sasa kwa muktadha huo maana yake tujaribu kuangalia suala la fedha kwa sababu, sisi tunasimamia mitaji ya umma. Tukizungumzia mitaji ya umma maana yake tunazungumzia suala la fedha, suala la mali zote ambazo zinamilikiwa na Serikali.

Mheshimiwa Spika, sasa hap ani mahali pake. Nadhani kwamba wakati wa bajeti pale tunakuwa tunasema tu fungu limepita au limekubaliwa. Na kwa kweli mafungu mengi tumeyapitisha, lakini utakuta kwamba kwa wakati huu ambapo tunaishauri Serikali, tunapokuja hapa kwa kamati zetu tatu maana yake utakuta kwamba kila mmoja anakuja kuangalia mapungufu yaliyotokana na yale mafungu. Kwa upande wa mashirika ya umma sisi tutakuwa tunaangalia suala la ufanisi, kwamba kuna ufanisi gani, una tija gani katika mashirika yetu? Tunaangalia je, sheria zilizopo maana yake zinafuatwa au hazifuatwi? Na vilevile yale mashirika kweli yanafuata taratibu za kibiashara?

Mheshimiwa Spika, na upande wa LAAC nao wataangalia upande wao kwa upande wa fedha zinazopelekwa katika taasisi za Serikali za mitaa; pamoja na PAC nao wataangalia fedha zile za umma zote kwa ujumla. Sasa leo hii tupo hapa kwa ajili ya kuishauri Serikali. Kuna ambao wanaweza kuishauri Serikali lakini wakati uleule kuna wanaoweza kuisema Serikali, kwa sababu kuna kuisemea na kuisema Serikali.

Mheshimiwa Spika, kwa nini nazungumza kwamba, kuna kuisema Serikali? Ni kwa sababu wakati mwingine kunakuwa na ule ukiukwaji wa zile sheria au taratibu zinakuwa hazikufuatwa. Pale sisi Wabunge tutakuwa badala ya kuisema Serikali maana yake tutakuwa tunaisema Serikali kwamba hatua hazifuatwi wala hazichukuliwi. Sasa kwa hali hiyo maana yake utakuta kwamba Wabunge wote kila mmoja anapokuja hapa kaja na ukali wa namna ambavyo alivyoona katika ule ufuatiliaji wetu au katika kuona kwetu katika haya mashirika maana yake hayaendi sawa.

Mheshimiwa Spika, sasa mimi nije kwa upande wa Kamati yangu ya PIC ambapo pale tumependekeza mambo 11. Moja katika mambo ambayo tumependekeza, mimi nije katika mapendekezo mawili. Pendekezo la mwanzo linahusu mchakato wa upatikanaji wa wajumbe wa bodi kwa wakati, lakini mimi pale badala ya kwamba, kwa wakati nimeingiza neno la wenye weledi. Sasa kwa nini nimezungumza hili kwa kuingiza na neno weledi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu, wakati mwingine mashirika mengi ambayo tumeyapitia humo, maana yake kuna mashirika mpaka hii leo yana kipindi cha miaka miwili yanakuwa hayana bodi. Sasa pale tukipima ufanisi wa shirika au ufanisi wa kampuni pale maamuzi yanakuwa si sahihi na ufanisi wenyewe unakuwa si mzuri. Na hata kibiashara kama shirika lile litakuwa ni la kibiashara maana yake biashara ile itakuwa inakwenda pasipo na maamuzi yaliyokuwa sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa bodi zetu, kwa mujibu wa huo ushauri tulioutoa, ningependa sana kwamba, uangaliwe sana. Na ninajua kwamba, wajumbe wengi sana suala la wajumbe wa bodi wamelizungumza, kila mmoja kalizungumza kwa upande wake na kwa upana wake. Sisi kwa upande wetu tutaangalia kwamba, bodi nyingi zinapomaliza muda wake zisichukue muda, ziteuliwe bodi mpya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan alipoizindua hii Taarifa ya CAG alisema wazi kwamba, kama kuna tatizo la bodi basi mimi sina tatizo hilo endapo tu nitakapoletewa katika meza yangu ndani ya wiki moja nitateuwa. Hapa inaonekana wazi kwamba inawezekana tatizo likawa liko katika zile taasisi zetu kuu, ikiwa ni pamoja na Wizara, maana hapo katika utendaji na ufanisi huo inawezekana pengine kunakosekana ufanisi na ndio maana hizo taarifa haziendi kwa Rais na inasababisha hata mashirika mengi yakawa yanachelewa kuteua bodi.

Mheshimiwa Spika, sasa hoja yangu iko hapa; katika utaratibu wa kuendesha taassisi zetu hizi bodi ndiye msimamizi wa kila kitu katika yale mashirika, ikiwemo mali pamoja na rasilimali zote za shirika au kampuni. Sasa ikiwa kama bodi au pengine taasisi haina mchunga maana yake hapo kitakachokwenda ni kitu gani?

Mheshimiwa Spika, kitakachokwenda hapo ni ubadhirifu katika shirika lile, au ufanisi na tija katika shirika lile inawezekana pengine usipatikane. Kwa mfano, wakati tulipokuwa tumekaa na mashirika yetu kuna Bodi hii ya Maji ambayo imekaa zaidi ya miaka miwili ambayo tunaita kwamba ni Bodi ya Mfuko wa Maji, bodi ile ina miaka miwili, utakuta kwamba anayekaimu nafasi ile ni Katibu Mkuu. Katibu Mkuu ana muda wake si zaidi ya mwaka mmoja, lakini bado mpaka leo taasisi ile, mfuko ule, hauna bodi, sasa hilo ni tatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na ninaweza kusema kwamba, wakati mwingine hii tija au ufanisi tunaoutaka katika mashirika yetu unakuwa haupatikani vile inavyopaswa. Sasa kinachotokea ni kitu gani?

Mheshimiwa Spika, badala ya kuishauri Serikali kwa Wabunge kinachofuata ni kuisema Serikali. Kwa sababu, tutakuwa sasa hatuisemei Serikali, tutakuwa sasa tunaisema Serikali kwa sababu, kila mmoja atakuwa anasema kwa mujibu wa ukali na hatua zake.

Mheshimiwa Spika, sasa nije na suala jingine ambalo katika mapendekezo tuliyopendekeza, Serikali iweke utaratibu wa kuzipatia taasisi zinazojiendesha kibiashara vibali vya kuajiri wenyewe ajira za moja kwa moja. Hilo nalo limekuwa ni tatizo; kwa sababu, uajiri wa Serikali ikiwa ni taasisi ya shirika, ikiwa ni kampuni ambayo inamilikiwa na Serikali uajiri wake, vibali vyake mpaka vitoke utumishi. Sasa, ikiwa shirika ni la kibiashara na linajiendesha vizuri, maana yake kuna haja gani mpaka kwamba vibali vile viwe na utaratibu? Pengine shirika lina mahitaji ya wafanyakazi zaidi ya 20 au 50 na uwezo wa kifedha wanao wa kuweza kuwalipa, kwa nini wanashindwa kupewa ile ruhusa ya kuweza kuajiri?

Mheshimiwa Spika, na tukikosa ufanisi huo wa wafanyakazi ambao ni rasilimali ya watu, maana yake tutakosa ufanisi wa ile kazi yenyewe, kwa sababu ufanisi wa rasilimali watu haupo. Sasa tukikosa rasilimali watu maana yake na tuna biashara na tunataka ufanisi, maana yake hapo ufanisi utakuwa haupo.

Mheshimiwa Spika, niishauri Serikali, yale mashirika au zile taasisi tunazoziona zinajiendesha kibiashara na zina uwezo wa kujilipa au kuwalipa wafanyakazi ni vyema zikapewa ruhusa ya kuweza kuajiri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nije na suala la tatu katika mchango wangu. Wajumbe wengi hapa wamechangia na kila mmoja kachangia hasa katika hali ya ufanisi wa Serikali. Katika suala la ufanisi wa Serikali kuna suala la ufuatiliaji. Hili suala la ufuatiliaji katika hizi taasisi zetu za Serikali linakosekana. Mashirika yetu haya yanaunda mpango kazi (work plan) wa miaka mitano au miaka kumi. Pamoja na kwamba kuna cap eye ziwekwa, lakini kunakuwa hakuna ufuatiliaji. Kwa hiyo, naomba sana suala la ufuatiliaji Serikali iandae tools ambayo siyo unit, iwe ni idara ya moja kwa moja ya monitoring and evaluation kuweza kuzifuatilia taasisi zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naona unaniangalia sana; baada ya kusema hayo nasema, ahsante sana. (Makofi)