Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, na mimi nikushukuru sana kwa kunipa nafasi. Nitakwenda moja kwa moja, na nitachangia sana kwenye eneo la elimu.

Mheshimiwa Spika, eneo lolote au sehemu yoyote ambayo kuna vyuo vikuu hata watu wake katika eneo lile wanakuwa na maendeleo ya kiuchumi, maendeleo ya kisiasa na maendeleo ya kijamii.

Mheshimiwa Spika, Mikoa ya Kusini kwa muda mrefu imekuwa nyuma sana katika maendeleo kwa nyanja zote. Mikoa ya Kusini wakati tumekuwa wote tukisema jamani sisi watu wa Kusini tuko nyuma. Leo hii kama Mikoa ya Kusini ya Lindi, Mtwara pamoja na Ruvuma kukiwa na Chuo Kikuu cha Serikali mambo ya uchumi yatafunguka na watu wa eneo lile wote watakuwa wanapata elimu kutoka vyuo vikuu na mambo yao yatabadilika kama ilivyo kwenye Mkoa wa Dodoma. Wagogo tulikuwa tunawasema watani zangu; zamani ukisema Mgogo wengine wanaona aibu hata kusema mimi ni Mgogo, lakini sasa hii ukisema unatoka Dodoma Mheshimiwa Mavunde anafurahi, kwa sababu Dodoma imefunguka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na mpango wa kujenga Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa, Matogoro, Songea na Mtwara, wakati ule Mheshimiwa Waziri alikuwa Prof. Msola, nimpongeze sana alikuwa mwerevu na mjanja; kikawekwa Chuo Kikuu pale Mkwawa ambacho ndicho Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu. Hata hivyo, wazo la Mtwara likafa kimya mpaka leo ikawa hatujui kinachoendelea, Matogoro – Songea nayo ikafa na hatujui kinachoendelea. Hizi sehemu tatu zilikuwa katika mpango wa kufanya haya maeneo yawe ni vyuo vikuu vishiriki, lakini mipango hiyo ikafa na hatujui kwa nini ilikufa.

Mheshimiwa Spika, niseme tu, kwamba Kusini tunahitaji a Public University full flagged. Mimi ningeomba Serikali jamani sasa hivi ijipange angalau kwa kipindi hiki waache legacy kama iliyoachwa hapa UDOM basi tuache legacy huko Kusini, kijengwe chuo kikuu ili watu wa Kusini nao waanze kufunguka. Tutafanya maendeleo mengine yote; tutajitahidi kilimo na mengineyo lakini bila elimu bado Kusini kule tunaonekana hatujatoka.

Mheshimiwa Spika, nije kwenye suala la pili ambalo naona nilisemee hapa ndani, ni suala hili la watoto wadogo wa chekechea. Hawa watoto wadodo nafikiri na Mawaziri waliangalie. Watoto wadogo wa chekechea wanaamshwa saa kumi usiku, saa kumi na moja magari yanawapitia, wanafika kwenye gari wanazunguka mpaka wafike shuleni labda ni saa mbili.

Mheshimiwa Spika, tunajiangalia sisi kwa sababu tayari tumeshakomaa na tayari tumeshapata elimu vizuri, lakini mimi naangalia, hivi hawa watoto wadogo wanaoamshwa saa kumi wanaandaliwa kwenda shuleni is it fair? Hiyo cognitive development ya hawa watoto kweli inaenda vizuri? Kwa sababu wanasinzia mpaka wakifika kule shuleni, na wakati wa kurudi wanazungushwa mpaka wanafika nyumbani kule yule wa kwanza anakuwa wa mwisho. Wakati mwingine tunasikia mambo yanayotokea ndani ya hayo mabasi wanayozungushwa.

Mheshimiwa Spika, sikatai kwamba tunafanya biashara, lakini sasa wanazungushwa na wakati mwingine wale wanaowazungusha kwenye magari mnasikia wanachowafanyia hao watoto. Sasa hilo nalo tuliangalie, kwamba hivi hii trend ni sawa? Wenzangu wataalam wa Saikoloji na wataalam wa Development ya hiyo brain, je, hicho kinachotendeka ni sawa?

Mheshimiwa Spika, niunganishe na moja linalotokea sasa hivi, mimi naona ni janga la Kitaifa. Kuanzia primary mpaka vyuo vikuu dawa za kulevya zimekuwa ni kawaida, bangi zimekuwa ni kawaida, michezo michafu inayofanywa na watoto wa kiume kwa wakiume imekuwa ni ya kawaida. Serikali tunasema nini? Tunajenga taifa la namna gani?

Mheshimiwa Spika, kuna siku moja kuna mzazi akanipigia simu akasema alienda huko beach, mnaita beach, sijui kwa Kiswahili tunaitaje, ufukweni; kwenda kule amekuta wasichana na wavulana wanafanya vitu vya ajabu vya waziwazi huko kwenye beach. Sizitaji shule maana tunasema tutaharibu biashara za watu; hivi tunaharibu biashara za watu ama tunaharibu Watoto? Mambo yanayofanyika sasa hivi ni ya ajabu, Wizara ya Elimu mpo, Wizara ya Afya mpo, Wizara ya Ustawi wa Jamii upo, Mambo ya Ndani mpo mpaka Utumishi. Tunalipeka hili Taifa wapi? Hivi baada ya miaka kumi au ishirini tutakuwa na watoto au tutaongeza vituo vya Mirembe? Hilo jambo linaniumiza na ni janga la Kitaifa, ni janga. Tutakuwa na watoto wa namna gani ikiwa hata watoto wa primary wanazijua bangi ni za kawaida? Je, tumehalalisha hii bangi? that a thing I want to know.

Mheshimiwa Spika, nije kwenye ukarabati wa vyuo vikuu. Niliongea kipindi kilichopita mpaka nikawa nawaza, hii UDOM niliizungumzia. Waende hao Mawaziri wakaangalie kule. Niliwaza nikasema hiki chuo ninachokizungumzia kingekuwa kipo Sumbawanga au kiko kule Newala labda wangekwenda, lakini kipo hapa karibu, hivi kwa nini hawaendi? Nelson Mandela ule mgogoro wa ujenzi wa kiwanja mpaka leo unaendelea, hawaendi.

Mheshimiwa Spika, ninawatahadharisha tu, ikija hiyo bajeti yao Elimu mimi yaani Shilingi hiyo nimeshandaa na watanifuata mpaka Ruvuma kuja kuichukua. Nelson Mandela, UDOM hapo kuna vyuo vya Afya vya kati, nilisema kule Songea hali ni mbaya, hebu nendeni mkazunguke kule muangalie. Nilisema wakati ule ulipokuwa Mwalimu wangu Ndalichako nilifiki umenielewa lakini ukani-put off kabisa, yaani sijui ulini-neglect kwa sababu ni mwanafunzi wako? I don’t know. Sasa amechukua mwingine, Professor Mkenda sitaki kuja kuniambia tuongozane, mimi sitaki kuongozana tukutane hukohuko, kuongozana sitaki. (Makofi/Vicheko)

Mheshimiwa Spika, jambo jingine nilizungumze kuhusu fedha za research katika vyuo. Nishukuru sana Serikali ni kweli sasa hivi watoto wengi wanapata mikopo, lakini kutokana na idadi kubwa ya watoto wanaopata mikopo fedha za research zikapungua sana.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)