Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza sina budi kumshukuru Mama Samia ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Alhaj Hussein Mwinyi - Rais wa Zanzibar, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu ambaye tayari ameweka hotuba yake ya bajeti mezani na Watendaji wake, pamoja na Mheshimiwa Spika na Naibu Spika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza na TASAF. TASAF imefanyakazi nzuri kwa Zanzibar, kwanza nitaizungumzia Unguja kwa sababu mimi ndiyo niliko TASAF kuna Shehia 126 zote zimefanya kazi nzuri wameweza kutoa ruzuku vizuri, wametoa ruzuku za vijana au watoto waliokuwa chini ya umri wa miaka 18 ambao wazee wao hawajiwezi, wametoa ruzuku kwa watoto wa chini ya miaka mitano kwenda kliniki, wametoa ruzuku kwa watoto wa kimaskini ambao wanaosoma Sekondari na Primary, wamewasaidia walemavu kwa ruzuku, wamewasaidia hata wajasiriamali, TASAF kwa Zanzibar tunaishukuru Serikali ya Muungano imesaidia vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile imechukua vijana wanaofanyakazi ofisi ya Makamu wa Rais Zanzibar ambao ndiyo wanasimamia TASAF wamewapeleka masomoni ili kwenda kuongeza ujuzi waweze kusimamia mazingira ya TASAF. Jambo likiwa nzuri likinafanywa na Serikali ya Muungano ikishirikiana na Serikali ya Zanzibar inabidi kulishukuru na kuliangalia vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba itakapokuja TASAF nyingine ya nne ifanyekazi vizuri zaidi ya hii iliyofanya sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja na changamoto za Muungano ambazo Mheshimiwa Waziri Mkuu ziko kwenye ukurasa wake wa 72. Kwanza Muungano ni tunu kwa Tanzania na Muungano wetu unaendelea vizuri, lakini kwenye changamoto walituambia kwamba 11 tayari zimefanyiwa kazi na zishamalizika kabisa na Serikali zote mbili hoja hizo Tisa tayari wamekubaliana kwa kuandikiana na tayari zimeisha. Mbili ziko katika utendaji lakini mimi bado naona hakuna tunalolifanya kwanini niulize.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto hizi Wabunge tuliopo humu ndani msimamishe mmoja tumuulize hakuna hata atakayeelezea nini na nini kimetendeka na kwa sababu gani, baada ya kuisha kuzifanya au kutanzuliwa zimo katika makaratasi au mafaili, hazijasambazwa kama kutengenezewa vipeperushi au kutengenezewa vitabu au kwenda ofisini kwa viongozi wakati unamsubiri kiongozi ukakuta juu ya meza yake pale vipo ukawa unasoma au mashuleni mwetu, kwa sababu kuna vijana humu siyo wazalendo hizi changamoto kila siku wanazirejea hizo hizo kwa sababu hawazijui.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utakuta kila siku bandarini gari yangu imekamatwa kwa sababu hatuelewi nini kinachoendelea, sasa ninaomba Ofisi ya Waziri Mkuu changamoto zote ambazo mlikubaliana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ziweze kuwekwa bayana kila mmoja azijue, vijana waliopo vijiweni, vijana waliopo shuleni, na vijana ambao watatumia hizi changamoto wakati wakitaka manufaa yao kuzorotesha au kufarakisha nchi anatumia hizi changamoto. Mheshimiwa Waziri Mkuu tuwe waungwana kwa kuweza kuzisambaza kila mmoja azipate. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la ukurasa wa 44 na 45 unazungumzia viwanja vya ndege na usafiri wa anga. Suala hili ni zuri na amesema ndege zetu zitatimia 16 ni jambo jema lakini kuna kitu kidogo ningeomba kiangaliwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unajua hizi ndege zina route na route zake mpaka Zanzibar zinafika lakini mkae mkijua Zanzibar kuna Wabunge, wafanyabiashara, wafanyakazi wa Serikali na Wafanyakazi wa Chama wanakuja direct Dodoma. Sasa wakati mtu unataka kuja Dodoma kwa ndege lazima ukasubiri ndege Dar es Salaam ndiyo ufike Dodoma. Kwa nini route moja tusiifanye kwenye wiki direct Zanzibar to Dodoma unaitoa Dar, Dar inakuja Zanzibar, Zanzibar to Dodoma au unaitoa Mkoa wowote…

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Fakharia Shomari. Ahsante muda wako umekwisha.

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Ahsante naunga mkono hoja na mimi nilikuwa nishamaliza.