Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Peramiho
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
WAZIRI WA NCHI, OFIS YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, na mimi nianze kwa kuungana na Waheshimiwa Wabunge, lakini Waheshimiwa Mawaziri wenzangu kuzipongeza sana Kamati na kipekee nimpongeze sana Mwenyekiti wa Kamati wa USEMI, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hakika naomba nikiri Kamati hiyo imetusaidia sana Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kutekeleza majukumu yetu sawasawa. Kwa kweli tunawashukuru na tunawapongeza na ninaahidi kuendelea kuwapa ushirikiano wa karibu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kiujumla nilipongeze sasa Bunge na Waheshimiwa Wabunge na niendelee kutuma ujumbe kwa wananchi wa Tanzania kwamba Bunge letu hili na Waheshimiwa Wabunge wamekuwa wakishauri mambo ya muhimu na mambo ya msingi na pale yanapofanyiwa kazi yameweza kuzaa matunda mazuri na yatatoa relief kubwa sana kwa maisha ya kila siku ya wananchi.
Mheshimiwa Spika, leo Wajumbe wa Kamati na Taarifa ya Kamati ya USEMI ilizungumzia kuhusu mfumo wa recruitment kwenye ajira hapa nchini. Hata wakati wa bajeti, Bunge lako tukufu lilitupa maelekezo Serikali kuangalia ni kwa kiasi gani tunaweza tukawarahisishia watoto wa Kitanzania kufikiwa na huduma hii ya usaili katika maeneo waliopo, kuliko kuwakusanya hapa Dodoma kila siku na kusababisha hasara kwa wazazi. Wakati mwingine watoto wamekuwa wakija hapa mara nyingi, anafanya interview sita, hajafanikiwa, anapoteza fedha na anaendelea kuitia umaskini familia yake.
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan na ndani ya Wizara yetu tumesikiliza kwa makini hoja hiyo na tumekwisha kuiripoti ndani ya Kamati na tumefanya maamuzi yafuatayo; jambo la kwanza, ile database ya kutunza matokeo ya watoto waliofaulu tumei-upgrade kutoka miezi sita mpaka mwaka mmoja. Kwa hiyo, sasa ina uwezo wa kutunza majina ya watoto waliofaulu kwa mwaka mmoja. Lengo lake ni nini? Mtoto leo anaweza kuja kufanya interview labda ya nafasi ya procurement, anashindwa kupata hiyo nafasi kwa ushindani kwamba labda nafasi zilikuwa tatu, yeye amekuwa wa nne ama amekuwa wa tano, anaingizwa kwenye database. Kwa hiyo, kukitokea nafasi nyingine ya procurement yule aliyeshinda achukuliwe badala ya kumrudisha tena kuja kufanya interview na kumsababishia usumbufu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kwa kuifanya database ikae mwaka mmoja itasaidia kuwakusanya wale waliofaulu na kama kuna nafasi zinatokea na zinawahitaji wale waliofanya usahili kwenye nafasi hizo hizo itoshe tu waliokwisha kufaulu wachukuliwe kuliko kurudishwa kurudishwa kurudishwa.
Kwa hiyo, sasa tulichokifanya pamoja na kuipeleka database kutoka miezi sita mpaka mwaka mmoja, tumefuata taratibu zote na tumeshatangaza kwenye Gazeti la Serikali, Mwanasheria Mkuu alishapitia kwa hiyo kila kitu kipo tayari. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mwezi wa kwanza mwaka huu na mwezi wa pili, usaili wowote utakaofanyika jumlisha wale ambao walionekana walifaulu nyuma na wakawekwa kwenye database tunataraji sasa watoto wa Kitanzania 1,769 watachukuliwa kutoka kwenye database na hawatasumbuliwa tena kurudi kuja kufanya usahili. Kwa hiyo, sasa database yetu itaanza kutumika. Kwa hiyo, tumetekeleza agizo hilo na tutaendelea kulisimamia. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwenye ajira; tumshukuru sana Dkt. Samia Suluhu Hassan, alipoingia tu kwenye Serikali yake ya Awamu ya Sita, Waheshimiwa Wabunge nadhani tumpongeze. Kwa mwaka 2021 mpaka Januari, 2023 tumekwishakutoa ajira 56,059 kwa fani mbalimbali. Hizo ni ajira mpya, lakini naomba niseme kwa mwaka 2022/2023 ajira zilizotolewa asilimia 53 zimeenda kwenda sekta ya elimu na sekta ya afya na zote hizo zimeenda kwenye primary health na kwenye primary education, kwa hiyo asilimia 53 zimeenda huko. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini ninyi Waheshimiwa Wabunge mlitupitishia bajeti, mwaka 2022/2023 tumebajeti ajira nyingine 30,000 na ajira hizo 30,000 Mheshimiwa Rais amesema kipaumbele kiwe ni elimu, kipaumbele kiwe ni sekta ya afya.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Rais na Serikali wanajua kabisa kwamba jambo hili ni la msingi na hivyo tutaendelea kulisimamia kuona maelekezo ya Bunge lakini na matamanio ya Mheshimiwa Rais ya kupunguza tatizo la ajira. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini tumeendelea kuwa- challenge wenzetu kwenye Regional Secretariat mwaka 2022 tumebadilisha muundo wa Regional Secretariat. Tumempa kazi Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulika na Utawala na Rasilimali Watu kuangalia suala zima la ajira pale kwenye eneo lake. Suala hili la ajira, sasa hivi ndani ya Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, tumeanzisha mfumo wa HR Assessment (Human Resource Assessment). Tunataka kuangalia hivi haya malalamiko ya ukosefu wa watumishi yanafananaje tumeanza kupata hiyo picha. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tukiangalia job weight ya mfanyakazi mmoja ya mfanyakazi mmoja mwingine zinatofautiana. Kuna baadhi ya wafanya kazi unaweza ukaangalia majukumu yao ukilinganisha na wengine, majukumu yao hayalingani kama vile inavyotakikana. Kwa hiyo, tumefikiri kwamba tufanye assessment ya kutosha, je, wataalam tunaowahitaji ni wa namna gani? Na hawa wataalam tunaowahitaji kwa zama hizi za Serikali tulionayo, mapinduzi ya nne ya viwanda yanayoendana na TEHAMA, tufanye nini? Kwa hiyo, tumeamua sasa tuboreshe muongoz wa HR Planning, watu wa plan matumizi ya rasilimali watu kwa kadiri ya mahitaji halisi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tumeamua tena kutengeneza mwongozo wa HR Succession Plan, masuala ya urithishaji, mtu mmoja kwenda kwenye nafasi nyingine yaweje. Tukiweza kuitumia rasilimali watu tuliyonayo na Regional Secretariat wakatusaidia kuwaangalia waliopo kwenye mikoa yao tuna uwezo wa rasilimali ndogo hii hii tulionayo ikaanza kutusaidia kupunguza uhaba wa watumishi wakati tukiendelea kubajeti na ku-control wage bill ambayo tunayo ndani ya Taifa letu.
Mheshimiwa Spia, lakini kwenye eneo la TASAF; tumeona TASAF inakwenda vizuri ingawa kuna challenge ndogo ndogo na Kamati imetushauri hapa. Eneo linalotupa changamoto hasa ni namna gani wale ambao wamekwisha kuwa na maisha bora wanaweza kuondoka na wakaingia wengine. Hapa tunapata shida, lakini tunashukuru, wanufaika wa TASAF 1,992 wako tayari kuondoka kwenye mpango wa TASAF, wanasema tayari maisha yao yako bora, wanufaika 200,000 tunawafanyia assessment.
Mheshimiwa Spika, na hapa nitoe wito kwa Waheshimiwa Wabunge na halmashauri zetu zote tunaomba sana huko kwenye halmashauri, Wakurugenzi wasiwaondoe wanufaika wa TASAF bila kuwasiliana na sisi. Wasubiri, tuna miongozo, hatujamaliza kufanya tathmini. Tuna mikataba ya kufanya tathmini mpaka tujiridhishe, tusije tukamuondoa mnufaika leo, kesho anaingia kwenye wimbi la umaskini, anadai tena kurudi kwenye mpango wa TASAF. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo tunaomba…
SPIKA: Dakika moja Mheshimiwa Waziri, malizia.
WAZIRI WA NCHI, OFIS YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, kwa tunaomba mtusaidie sana.
Mheshimiwa Spika, lakini tumepokea ushauri kuhusu TAKUKURU Rafiki na namna gani tuataendelea kuzuia rushwa kuliko kupambana nayo. Hiyo tunaifanyia kazi, tume-present kwenye Kamati mpango mpya wa TAKUKURU Rafiki, tuna uhakika utatusaidia sana.
Mheshimiwa Spika, kwenye eGA tumechukua ushauri wa Kamati kwamba ni lazima tuanzishe incubations center. Naomba niwaambie Waheshimiwa Wabunge tayari tumekwisha kuianzisha na tayari vijana 222 wameshapita kwenye incubation center, vijana 59 wanaendelea. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba tu nikupe taarifa hata mfumo wa TEHAMA unaotumika Bungeni vijana hao 59 wameshiriki kuuandaa na kuweza kufanya utumike pamoja na mifumo mingine mingi.
Ninaomba tu niseme kwamba tutaendelea kusimamia haki na stahiki za watumishi, walimu wamezungumzwa sana hap. Ninaomba nikuhakikishie Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, imekwishakupandisha madaraja watumishi 264,491 wengi wao wakiwa ni walimu na hiyo ni kuonesha appreciation ya Serikali kwa walimu wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini tumeendelea kulipa malimbikizo ya mishahara, tumeendelea kufanya re- categorization.
Mheshimiwa Spika, lakini unakumbuka pia tumeshughulikia umri wa bima ya afya kwa watoto na wategemezi wa watumishi wa Serikali, lakini vilevile tumeshughulikia masuala ya kuondoa retention fee…
SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Waziri.
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, kwa hiyo tunaendelea watumishi wa umma iliwaweze kufanya kazi vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba kushukuru kwa nafasi hii, Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuwajali watumishi na kuangalia kero za kiutumishi ili utendaji kazi uweze kuwa na tija kwenye Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ahsante sana, nakushukuru. (Makofi)