Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
2
Ministries
nil
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia kwenye taarifa ya Kamati ya UKIMWI lakini taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini. Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, lakini nitachangia maeneo mawili kwenye Kamati ya Nishati na Madini, upande wa nishati na upande wa madini na muda ukibaki nitachangia jambo la tatu.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza upatikanaji wa umeme katika Grid ya Taifa nchini, kwa ujumla ukweli uhitaji wa umeme kwenye nchi yetu ni mkubwa sana ukilinganisha na umeme ambao tunao. Labda nitaje vyanzo vya umeme ambavyo vina-feed kwenye Gridi ya Taifa.
Mheshimiwa Naibu Spika, chanzo kikubwa kinacho-feed Gridi ya Taifa kinachoongoza ni gesi asilia ambayo ni asilimia 62 ambayo ni megawati 1,103 lakini kuna umeme wa maji megawati 574 sawa sawa na asilimia 32 lakini kuna chanzo cha mafuta ambayo ni megawatit 88.13 sawasawa na asilimia 4.96 lakini umeme kutokana na tungamo taka ambayo ni megawati 10.50 sawasawa na asilimia 0.57 ambayo inatengeneza jumla ya megawati 1,777 ambayo ni asilimia 100 ya umeme wetu nchini.
Mheshimiwa Naibu Spika, jitihada za Serikali tumeziona kwa sababu mradi wa umeme wa Mwalimu Nyerere unaweza kwenda kutengeneza megawati 2,115 ambayo itaongeza nguvu kwenye Gridi ya Taifa kufikia megawati 3,892.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimetaja takwimu hizi ili tuone namna ambavyo bado tunauhitaji mkubwa wa umeme kwenye Taifa, na ni lazima watu wafahamu kwamba pamoja na miradi, huu ni mradi mkubwa kabisa ambao nimeutaja kwa sababu ni mradi ambao ni flagship ni mradi ambao ni wa kimkakati na ni mradi ambao wote tumetolea macho huko, lakini bado hata tiukipata megawati hizi bado uhitaji wa umeme ni mkubwa sana kwa sababu tunategemea umeme nchi nzima, kuna biashara, kuna maisha ya kawaida ya Watanzania kwa hiyo uhitaji bado ni mkubwa sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ni miongoni mwa watu wanaoamini katika nishati jadidifu ikiwemo mradi wa Mwalimu Nyerere ndiyo maana tunaushikia bango kwamba mradi wa Mwalimu Nyerere ni lazima ukamilike, kwa sababu ukikamilika tunaongeza base- load kwenye Gridi ya Taifa.
Mheshimiwa Naibu Spika, labda niseme kitaalamu ili uzalishe umeme wa nishati jadidifu nyingine kama nishati ya upepo na nishati ya jua ni lazima base-load iwe na umeme ambao ni sufficient umeme ambao ni wa uhakika na ni umeme wa maji pekee ambao ndiyo umeme pekee wa uhakika dunia nzima. Kwa hiyo, kukamilisha umeme wa Mwalimu Nyerere ni kuongeza base-load ili tuweze ku-feed kwenye Gridi ya Taifa kwenye umeme mwingine, kwenye nishati jadidifu kwa sbababu kuna madhara mengi sitayazungumza hapa kuhusiana na sasa hivi chanzo cha umeme ambacho kinaongoza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama sasa hivi tungekuwa tumekamilisha mradi wa Mwalimu Nyerere kama ambavyo ilitakiwa mwanzo, tungekuwa bado hatuwezi kuutoa umeme pale kwenye mtambo Selous Bwawani kuupeleka kwenye kituo, kwa sababu transmission line imefika asilimia 83.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu umeme pale tunaweza tukaona mitambo inafanya kazi lakini kuutoa pale kuupeleka kwenye kituo cha kupoozea umeme kuna line inatakiwa ijengwe iko asilimia 83 haijakamilika. Kwa hiyo, kama ile kudra za Mwenyezi Mungu paap maji yamejaa Mwalimu Nyerere hatuwezi kuutoa ule umeme tutabaki tunauangalia pale. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kituo cha kupooza umeme Chalinze ambapo ndiyo umeme ule unaenda kupoozwa pale, kiko asilimia 47. Kwa hiyo, niseme naomba nipendekeze kwenye maazimio, Bunge hili liitake Serikali kuharakisha ujenzi wa transmission line kupeleka kwenye kituo lakini pia kujenga kituo cha kupooza umeme cha Chalinze, kwa sababu maji mvua zinaendelea kunyeesha tumeshafanya marekebisho huko kwenye vyanzo vya maji ambavyo vina-feed Bwawa la Mwalimu Nyerere, hamadi! bwawa limejaa hatuna sehehmu ya kupeleka umeme, hatuna njia, hatuna mtambo, maji yanaendela kujaa. Kwa hiyo, tuweke pia azimio la kuhakikisha kwamba transmission line na kituo kinajengwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ni Mwanza Refinery, mwaka 2021 Juni, Mheshimiwa Rais Samia alizindua kituo cha kusafisha dhahabu cha Mwanza kwa masikitiko makubwa sana mpaka leo bado kituo hakijapata ithibati na sababu ya ile refinery ya Mwanza kukosa ithibati ni kwa sababu hatuna rasilimali ya kutosha ku-feed ile refinery tuliyoijenga pale.
Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge hili mwaka 2017 lilitunga sheria inaitwa Sheria ya Madini ya mwaka 2017 ambayo sheria hiyo Sura ya 123 kifungu cha tisa, lengo lake ilikuwa ni kwamba dhahabu inayozalishwa Tanzania kabla haijapelekwa nje isafishwe hapa ili kuiongezea thamani, na lengo lilikuwa zuri. Mikakati ya Serikali kwa sababu mtu hawezi kuelewa, kwa siku kile kiwanda kinahitaji kilo 59 sawasawa na kilo 1,770 kwa mwezi kile kiwanda kinahitaji ili kifanyekazi, kinakosa ithibati kwa sababu hatuna rasilimali ya kutosha ku-feed kile kiwanda.
Mheshimiwa Naibu Spika, mchakato ya Serikali wanataka wakanunue dhahabu Congo it is well and good, lakini mimi nazungumza kwa ajili ya Watanzania, vijana ambao tunataka tufaidike na value chain, mnyororo wa thamani, ardhi yetu Tanzania ina dhahabu. Kwa sababu hilo soko la Congo, East Africa yote inaangalia soko la Congo, Rwanda wanaangalia soko la Congo na nchi nyingine, kwa sababu sidhani kama Wakenya nao hawaangalii, soko la Congo ni probability. Hebu tuangalie hapa Tanzania dhahabu yetu kweli haitoshi ku-feed kile kiwanda mpaka tuende Congo? Ni kweli ni initiative nzuri kwa sababu tunataka wauze hapa na maendeleo yataendelea vuzuri nami niwapongeze, lakini GST imekosa uwezo wa kusaidia vijana wetu kiteknolojia, kuwafanya vijana wetu wapate uhakika na sampuli za madini wanazozipeleka pale, kwa sababu eti hatuna certified reference materials, kutoa ithibati, kuthibitisha uhakika wa madini yanayopatikana ardhini matokeo yake tunategemea nchi nyingine zituuzie dhahabu wakati vijana wetu nasi tunataka waendelee!
Mheshimiwa Naibu Spika, tumechoka kuona migodi kule Mwanza yamebaki mashimo vijana wetu wamebaki na umaskini, tunatamani tushiriki kwenye mnyororo wa thamani ili nasi tuendelee na tunufaike. Kwa hiyo niwaombe sana liongezeke azimio la kuitaka STAMICO na GST ishirikiane kwa ukaribu kutafuta mbadala, kutafuta suluhisho la dharura ili GST iwe na uwezo wa kiteknolojia na hizo sampuli zinazopelekwa pale kwenye maabara za GST zituletee majibu ambayo yana uhakika ili vijana wetu wakachukue mikopo benki na hayo majibu ya GST, waende wakachimbe dhahabu, dhahabu iende ika- feed Mwanza refinery kwa sababu mwaka mzima tumeshindwa, ni kitu ambacho hakiwezekani.
Mheshimiwa Naibu Spika, kile kiwanda kinauwezo mkubwa kwa sababu kwa viwango vya kimataifa kile kiwanda kinauwezo wa kusafisha dhahabu 99.9 purity ambao tunaweza tukawa ni kiwanda kikubwa Tanzania na Afrika ikiwezekana hata Afrika Mashariki, kwa hiyo ni kitu kikubwa, haiwezekani tukawa tumepoteza rasilimali mwaka mzima kama hivyo halafu ikabaki hatusemi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ya muda kuna jambo moja ambalo limefanyika for the first time in our country, Mfuko wa Nishati safi ya Kupikia (Cook Fund). Ninaipongeza sana Wizara ya Nishati pia ninaipongeza Serikali kwa ujumla, kwa sababu ni miaka mingi lakini for the first time tumefanya mjadala wa Kitaifa kuhusiana na nishati safi ya kupikia, na kwa sababu mimi ni mama pia napika lakini pia natoka kijijini kabisa ambako tunajua kwamba…
(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)