Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Hon. Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa naomba nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupatia afya njema na amani na furaha katika kipindi chote hiki cha mijadala ya Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Vilevile nitumie nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuniamini na kuniacha katika Ofisi yake yeye kumsaidia. Pia nitumie fursa hii kumshukuru Waziri wangu ambaye amekuwa mlezi, mwalimu na kwa muda mfupi Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama ambaye nimefanya naye kazi kwa kweli nimejifunza mengi sana, namshukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie fursa hii vile vile kuwashukuru wananchi wa Jimbo langu la Chamwino hapa Mkoani Dodoma kwa kuendelea kuwa na imani na mimi kama Mbunge wao na niendelee kuwaahidi kwamba sito waangusha na nitaendelea kuwatumikia vema siku zote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika shukrani mwisho lakini si kwa umuhimu, kwamba in a particular order pia nimshukuru mke wangu kipenzi Subira na wanangu kwa kuendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho naendelea na shughuli mbalimbali za siasa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile niwashukuru wajumbe wa Kamati ya USEMI wakiongozwa na Mwenyekiti wetu, Mheshimiwa Abdallah Chaurembo; Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa Denis Londo; na wajumbe wote wa Kamati ya USEMI kwa kuendelea kutupa miongozo mbalimbali, ushauri mbalimbali na kufanya nao kazi vizuri siku hadi siku. Mwisho kabisa niwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa ushirikiano wao na kutushauri inapobidi na vile vile kwa michango yao ambayo walikuwa wanaitoa katika kipindi hiki cha bajeti yetu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nikienda kwenye hoja ambazo zimezungumzwa sana humu na Waheshimiwa Wabunge, nitajikita katika kuzungumzia hoja kubwa ambayo imegusa kila Jimbo la Mbunge humu ndani na katika nchi yetu, ni suala zima la TASAF. Katika kuzungumzia TASAF nitaanza kwanza kuelezea ili tupate uelewa wa pamoja wa namna ambavyo walengwa hawa wanapatikana, kwa sababu kwenye michango ya Wabunge nimeona sintofahamu ya walengwa hawa wanavyopatikana. Mfumo ulivyowekwa wa kuwapata walengwa wa kaya hizi ni kwamba wanatambuana wenyewe katika mikutano yao ya Serikali ya Kijiji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wanapoitana wanaanza utambuzi wa kujua nani anastahili kuwa katika mpango huu wa TASAF na nani ana uwezo wa kutosha wa kutoingia katika mpango huu wa TASAF. Baada ya utambuzi ule, ndipo waratibu wale katika ngazi zile wanachukua majina yale na kuweza kuyaingiza kwenye mfumo na majina yale kisha kwenda Makao Makuu na sasa kuwa authorized na malipo kuanza kufanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nipende tu kulitaarifu Bunge lako kwamba mpango huu wa TASAF unaanzia chini kwenda juu na si juu kwenda chini. Kaya hizi tunazozizungumzia ni 1,277,000, nchi nzima, ni kaya ambazo kabla ya mpango huu wa TASAF kuanza zilikuwa hazina uhakika wa milo mitatu kwa siku. Mpango huu umekuja ili kuweza kuwapa safety net ya maisha yao kuweza kuwanyanyua na kuwapa uhakika wa kula yao na uhakika wa kesho yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndio maana huwa tunasisitiza na kuwaomba Waheshimiwa Wabunge wawe mabalozi wa mpango huu wa TASAF na kila wanapokwenda Jimboni waweze kuzungumzia mpango huu. Pia kuhimiza wale walengwa yaani kaya zile kuhakikisha kwamba wanazitumia fedha hizi kufuga, fedha hizi kulima ili pale wanapopata uwezo wa kuwa na mifugo mingi, ndipo sasa wataweza kununua bima ya afya na kuweza kukidhi mahitaji mbalimbali ya siku. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mpango huu umekuwa na mafanikio makubwa sana. Kwa dakika tano sitoweza kuzitaja au sitoweza kutaja mafanikio yote ya mpango huu wa TASAF, lakini mpango huu umekuwa na mafanikio makubwa ambapo ukitembelea maeneo mbalimbali nchini, ukawasikiliza walengwa na kuona vile walivyokuwa wakiishi kabla ya kuingia kwenye mpango na baada ya kuingia kwenye mpango, utaona jambo lililofanywa na Serikali ni jambo kubwa sana. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)