Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Madini

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Madini

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipa fursa hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba ya makadirio na mapato ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023.

Pili, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kutayarisha na hatimaye kuiwasilisha hotuba hii katika Bunge lako tukufu kwa ufasaha na umakini mkubwa.

Mheshimiwa Spika, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo nikianza na suala la wachimbaji wadogo; napenda kuipongeza Wizara kwa juhudi zake inayozichukua katika kuwaenzi wachimbaji wadogo. Hili ni kundi kubwa na ni muhimu katika nchi yetu. Kundi hili kwa muda mfupi limeonesha maendeleo katika kuchangiya pato la Serikali.

Mheshimiwa Spika, napenda kushauri Serikali mambo mawikli katika kundi hili; kwanza Serikali ioengeze jitihada ya kuwapatia mafunzo zaidi wchimbaji hawa ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

Pili, nashauri Serikali iwapate bima za afya wachimbaji hawa ukizingatia kuwa kazi hii ni miongoni mwa kazi ngumu na za hatari. Naunga mkono hoja.