Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi, mimi naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Kigua kama alivyoitoa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ukiangalia changamoto hii ya mafuta tukianzia Machi. Machi petrol ilikuwa Shilingi 2,459 hii ni kwa Dar es Salaam, Aprili ilikuwa Shilingi 2,642 na Mei ilikuwa Shilingi 3,148, ina maana kumekuwa na ongezeko la asilimia 28. Ukija diesel ilikuwa Shilingi 2,500 natolea kwa Dar es Salaam, Aprili, Shilingi 2,644 na Mei Shilingi 3,258 ongezeko la asilimi 30; mafuta ya taa ilikuwa Shilingi 1,811 mwezi Machi, Aprili ilikuwa Shilingi 2,173 na Mei imekuwa Shilingi 3,112. Sasa hii trend ya kuongezeka mafuta kiasi hiki inakwamisha hata maendeleo ya Watanzania kwa ukubwa, kwa maana nyingine hili ni janga kama lilivyokuwa janga la UVIKO. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tukiangalia Watanzania asilimia kubwa kule vijijini mafuta ya taa ndiyo wanayoyatumia, hii imeleta changamoto kubwa wananchi kwa ongezeko la zaidi ya asilimia 71 ya mafuta ukiangalia toka Machi mpaka Mei. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa mimi ninaliona tatizo hili ukiangalia wale wananchi waliokuwa wakipanda bodaboda kwa Shilingi 1,000 hivi sasa hivi ni shilingi 3,000, wale waliokuwa wakipanda bajati kwa shilingi 5,00 sasa hivi ni shilingi 1,500 inakwenda hadi shilingi 2,000 kwa Mtanzania wa hali ya chini imekuwa ni changamoto kubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ushauri wangu kwa Serikali, kwa sababu kwa sababu nimesema hili ni janga ni kama lilivyokuwa la UVIKO tunaweza kukopa pia mikopo ya bei nafuu ikasaidia kuweza kupunguza changamoto hii. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lingine tukiangalia kama tuliweza kutoa ruzuku kwa pembejeo, basi tufanye hivyo pia hata kwa sekta hii ya mafuta ili tuone jinsi ambavyo wananchi itawapunguzia mzigo mkubwa wa kuendesha maisha yao. Unaona wananchi wanapata shida, kwa kweli hali ni mbaya. Usafiri bei zimepanda mno na kila mtu anakuja na bei zake, kwa hiyo, Watanzania wanapata changamoto kubwa ya mafuta haya yalivyopanda. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo lingine tuweze kuondoa tozo nyingine, tunaweza tukaancha hizi za REA na mambo mengine lakini hizi tozo nyingine tuziondoe kwa muda wa mpito, tukikaa sawa tutakuja kuona huko mbele. Lakini kwa wakati huu, hizi tozo tupunguze ili wananchi waweze kufanya hivyo, lakini Serikali kwa kweli ipate muda wa kuyatafakari haya na kuja na majibu kwa Watanzania.
Mheshimiwa Spika, tumeona kwa nchi ya Kenya, walitoa ruzuku lakini hata jana wameendelea kutoa ruzuku, wametoa ruzuku ya shilingi za Kenya bilioni 34.4 ambayo ni sawasawa na shilingi bilioni 691.2 za Tanzania. Hii inawasaidia wananchi wa Kenya kuweza kupunguziwa ukali wa Maisha yao. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nakushukuru lakini niombe Serikali kwa kweli ikae, itafakari ije na majibu ambayo yatawasaidia Watanzania. (Makofi)