Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kuweza kunipa fursa ya mimi kuchangia kwenye Wizara hii muhimu ya maji sote tunajua kwamba maji ni uhai lakini zaidi maji ni uchumi.
Mheshimiwa Spika, nimekuwa nikishauri hapa, na sote tunajua kwamba Tanzania nzima tatizo la maji ni kubwa kwa kweli, kwamba tuje na suluhisho la muda mfupi wa kati na mrefu. Mathalani kwa Mkoa wetu wa Mara majimbo yote takribani asilimia 40 ya wakazi wa kule ndio wanapata maji, tena hapo nimeweka kiwango cha juu sana. Lakini ukiangalia target ya Wizara sasa hivi kwa maji vijijin ni almost asilimia zaidi ya asilimia 70 na mijini zaidi ya asilimia 85 na target kufikia mwaka 2025 wanataka maji vijijini yawe asilimia 85 na mjini yawe asilimia 95.
Mheshimiwa Spika, na hii inatokana na uhalisia kwamba tunakuwa na takwimu ambazo tunazingatia tu miundombinu ya maji iliyotandikwa pale bila kujua uhalisia, kwamba maji yanatoka au la unakuja una-count kwamba maji yanapatikana kwa kiasi hicho. Hii inakuwa ni adha kubwa sana na inasababisha kwa kweli tuendelee kushuhudia Watanzania wakitembea muda mrefu kutafuta maji, na wengine wakiliwa na mamba na kadhalika.
Mheshimiwa Spika, kwenye miradi ya miji 28 mwanzoni Mji wa Tarime ulikuwepo, lakini nimesoma Ibara ya 122 ya hotuba ya Waziri hapa anaeleza kwamba ule mkopo wa kutoka India miji 24 tu ndiyo inaenda kutelelezwa na kuanzia mwezi Aprili na kuendelea. Ambapo Mji wa Tarime Songea na Mafinga na kwingine imeondolewa.
Mheshimiwa Spika, mwaka 2017 aliyekuwa Rais Hayati Magufuli alivyokuwa amezuru Mkoa wa Mara akiwa kwenye viwanja vya TTC aliwatamkia bayana wananchi wa Tarime kwamba maji yanakwenda kutoka Ziwa Victoria kuja pale, 2017, miaka mitano sasa hivi. Na tumekuwa tukiuliza hii miradi tukifuatilia mnatuahidi hapa kwamba mradi unaenda kuanzishwa. Leo mnasema Tarime Mji itapata maji baada ya Serikali kutafuta vyanzo vya ndani. Leo tunavyozungumza Tarime Mji chini ya asilimia 40 pia pamoja ni kwamba mjini hawana maji na haya maji yanatoka Ziwa Victoria tu, ambapo mngekuwa mnavuta pale Rorya wangefaidika Tarime pia ingefaidika.
Mheshimiwa Spika, nataka kushauri hapa; kwa sababu kuanzia mwanzo hii miji 28 ilikuwa inahesabika hizo fedha ambazo zina uhakika zinapatikana kuanzia Aprili mradi unaanza kutekelezeka ianze yote miji 28 wakati huo mkitafuta hivyo vyanzo vya ndani mtakuja ku-supplement huko mbele wakati miji hii 28 yote mmei-take on board, kinyume cha hapo kwa kweli hatutawaelewa, na mtabidi mtuambie ni vigezo vipi ambavyo mnatumia ambavyo vinakuwa na bias, yaani mmefikia vigezo vipi ku-arrive kwamba Tarime isiwepo kati ya miji 24 ambayo mmeamua kuiweka lazima mtueleze wananchi wa Tarime na hiyo miji mingine minne ambayo mmeamua kuiacha ni kwa nini.
Mheshimiwa Spika, lakini pia ukiangalia, nimejaribu kupitia jedwali la IIIA; Mheshimiwa Waziri ameainisha baadhi ya miradi ambayo inaenda kutekelezeka ya maji vijijini. Kuna mikoa inapewa zaidi mpaka bilioni 16. Kwa mfano Mkoa wa Katavi bilioni 16, Kagera bilioni 14, nimeona Mwanza bilioni 13, Mara tunapewa bilioni 1.6 tu miradi ya vijijini. Nimerudia kusema hapa, nimepitia hiyo tatu A, Mara wanapata bilioni 1.6 miradi ya vijijini, majimbo yote 10, kweli! Is this fair? Mnatumia vigezo vipi wakati mnagawanya hizi rasimali za nchi kuhakikisha kwamba tunatatua matatizo katika mikoa yote au majimbo yote ambako tunajua kote kuna matatizo ya maji haya? Mnatumia vigezo vipi? Au ndiyo biasness Mara nayo muinyime hela Tarime muiondoe mradi wa maji na Rorya, ambayo ingefaidika yani mnatumia vigezo vipi ni kwa nini wanakuwa wanabagua.
Mheshimiwa Spika, lakini kingine kuhusu utunzaji wa vyanzo vya maji. Tumekuwa tukishuhudia kuwa vyanzo vya asili vya maji havitunzwi. Mfano Mto Mara ambao unasaidia vijiji kadhaa na kata kadhaa; vijiji vya Korurya Kibusyo kule tunasaidika, lakini vyanzo hivi havitunzwi, Serikali pia haijajenga hata basi visima vya kuweza kusaidia. Wale walioenda kufanya utafiti walisema wakati wanaangalia haya maji, walikuwa wanatembea zaidi ya KM 30 wanakutana na source ya maji, sasa yale maji yakichafuka pale hawa wananchi wanakuwa hawapi alternative ya maji ya kutumia. Sasa tunashindwa kuweka maji ya muda mfupi ya visima, tunashindwa kuchimba mabwawa tunashindwa pia hata kutunza haya maji ambayo Watanzania wanaendelea kutumia wakati huo tukijikongoja kuweza kuwasaidia kupatia maji.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nilikuwa nashauri Serikali iweze kuangalia vyanzo vya asili ambavyo tunavyo, ivitunze wakati huo ikitafuta mbadala wa kuhakikisha kwamba inapeleka maji, tena miradi ya muda mrefu kutoka Ziwa Tanganyika, Victoria. Tuamue na tu-prioritize once and for all; kwamba tunaamua kujenga miundo mbinu ya maji tutatue matatizo ya maji kwa Watanzania. Kama vile ambavyo tumeamua kuwekeza kwenye Wizara ya Uchukuzi na Ujenzi hata hapa tuweke trillions of money ili tuhakikishe kwamba tunachukuwa maji kutoka sources zote ili kuwezesha Watanzania kupata maji.
Mheshimiwa Spika, tusipokuwa na maji safi na salama Watanzania wanaugua, nchi inapata hasara kwa kuwatibu hawa Watanzania ambao wanaugua kwa sababu hatuna maji safi na salama; lakini pia Watanzania wanashindwa kufanya kazi za kuzalisha uchumi wakitembea kutafuta maji. Kwahiyo hii Wizara tuipe kipaumbele cha dhati, fedha zitengwe za kimkakati hii miradi mikubwa mikubwa yote iahakikishe imejengeka ndani ya muda mfupi ili ile hata ilani yenu ya CCM ambayo mmeisema 2025 muweze kuwa mmefikisha asilimia 95, 85 iweze kufikika, vinginevyo inakuwa hatufanyii chochote kile.
Mheshimiwa Spika, mwisho nikuhusiana na maji taka…nitaliandikia…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)