Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maji

Hon. Zuena Athumani Bushiri

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maji

MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Spika, nami naomba kuchangia hotuba ya Wizara ya Maji na nianze kwa kuipongeza Serikali ya Chama cha Mapinduzi kupitia Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya kuhakikisha anamtua mama ndoo kichwani.

Mheshimiwa Spika, naomba nichangie katika Wakala wa Maji Safi na Mazingira Vijijini (RUWASA); niongelee tatizo la maji katika Wilaya ya Same Jimbo la Same Mashariki katika Vijiji vya Maore, Kadando na Muheza. Vijiji hivi vimekuwa na tatizo la maji kwa muda mrefu sasa baada ya intake kusombwa na mafuriko ya mvua yaliyotokea Desemba, 2021. Mradi huu wa maji ulijengwa tangu mwaka 1967 idadi ya watu ikiwa ndogo sana, hivi sasa idadi ya watu imeongezeka sana.

Mheshimiwa Spika, niiombe Serikali ipeleke pesa za ujenzi wa intake na kukarabati miundombinu ambayo imekuwa chakavu kutokana na muda mrefu tangu ilivyojengwa.

Mheshimiwa Spika, nichangie pia kuhusu uchimbaji wa visima nchini. Maji ni uhai; kutokana na kauli hiyo niipongeze Serikali kwa kuchimba visima vya maji kwa maeneo ambayo hayana vyanzo vya maji. Ni naishauri Serikali iongeze bajeti katika eneo hili la uchimbaji wa visima ili kupunguza changamoto ya maji na kuwafanya wanawake wafanye kazi za uzalishaji badala ya kutumia muda mwingi katika kutafuta maji.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo naunga mkono hoja.