Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Afya

Hon. Anastazia James Wambura

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Afya

MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Spika, napenda kutoa hongera sana Waziri Mheshimiwa Ummy Mwalimu na Naibu Waziri Mheshimiwa Dkt. Mollel kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Wizara ya Afya. Pia hongera kwa Mheshimiwa Rais Mama Samia kwa kuongeza idadi ya vituo vya afya katika nchi yetu kwa muda nfupi.

Mheshimiwa Spika, nina ushauri katika eneo la upatikanaji wa dawa, ufanyike ukaguzi wa kushtukiza katika vituo vya afya mara kwa mara ili Wizara iweze kujua ukubwa wa tatizo na kuwabaini wanaofanya ubadhirifu katika eneo hili.

Mheshimiwa Spika, miongozo ya Wizara ya utoaji dawa katika vituo vya afya ipitiwe upya na kuangalia ile inayogongana na ya NHIF na kuiweka sawa ili kuondoa usumbufu wakati wa madai ya fedha ya vituo vya afya na NHIF.

Kuhusu huduma bure kwa akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano itolewe maelezo ya kubainisha hiyo bure inahusisha vitu vipi au gharama zipi ili ieleweke wazi kwamba Serikali inahusika katika maeneo yapi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.