Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Biharamulo Magharibi
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Spika, nachukua nafasi hii kukushukuru na kushukuru Waheshimiwa Wabunge wote waliopata nafasi ya kuchangia. Wamechangia takribani Waheshimiwa Wabunge 16 na michango yao karibu yote ilijikita kwenye yale maazimio yetu matatu ambayo niliyasoma hapa mwishoni. Kwa hiyo, nawashukuru sana kwa michango ambayo mmeitoa ya kumpongeza Mheshimiwa Rais katika maazimio haya matatu ambayo nimeyasoma hapa, ni michango mikubwa sana.
Mheshimiwa Spika, nadhani Watanzania ambao tunawawakilisha katika Bunge hili, sisi kama Wawakilishi wao ni mashahidi. Haya ambayo Waheshimiwa Wabunge wameyasema ni dhahiri Mheshimiwa Rais anayaishi na wao wanayaona kwa vitendo.
Mheshimiwa Spika, labda nigusie tu kidogo kwa wale waliochangia katika habari ya kudumisha demokrasia. Nadhani karibu wote wameogelea hii nyanja ya demokrasia na wote ni mashahidi tunaona, shughuli za siasa zimeanza na zinaendelea. Hali kadhalika vile vikosi vya maridhiano ambavyo vinaendelea na kazi, vyote vinaenda vizuri. Kwa hiyo, tumshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa hiki alichokianzisha. Maana kama wasingempa ushirikiano wale watu, tusingekuwa tumefika hapa.
Mheshimiwa Spika, pia ipo habari ya kukuza diplomasia ya kiuchumi. Hili jambo ni nyeti sana, wote tumesikia jinsi Waheshimiwa Wabunge wamechangia. Kuvutia wawekezaji kama Wabunge walivyosema, kama mazingira kwako siyo mazuri; na pia unapotafuta wawekezaji kwenye biashara, unaponyanyuka kuna baadhi ya watu utakutana nao unapata confidence ya kuja huku, kwa sababu mataifa mengi ya Afrika hayajulikani. Kwa hiyo, kazi kubwa anayoifanya Mheshimiwa Rais ya kuzunguka huku na huku, ndiyo tunaona matunda kama haya.
Mheshimiwa Spika, wote ni mashahidi, mwaka jana 2022 kwenye Dubai Expo mikataba iliyosainiwa pale mbele yake ilikuwa ni mingi na mizunguko yote ambayo amekuwa akiifanya tumekuwa tunaendelea kupokea neema kama hizo, na kama tulivyosema kwenye maelezo, hata ujio wa Makamu wa Rais wa Marekani pia umetufungulia fursa nyingine kwa vipengele ambavyo nimevitaja.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, pia hiyo ni sehemu na ni juhudi kubwa sana za Mheshimiwa Rais ambazo amezifanya, lakini kwenye sehemu ya tatu au sehemu C ambayo niliisema, kulikuwa na habari ya kumuunga mkono Mheshimiwa Rais. Sasa nadhani wale wote ambao wameongelea Ripoti ya CAG, wote ambao wameongelea yale mambo yanayoendelea hapa sasa, hatumuungi mkono tu atekeleze, ni pamoja na kumlinda. Sasa kazi kubwa ambayo anayoifanya Mheshimiwa Rais kama haitapata protection ya Bunge kama ambavyo mmesikia Wabunge wanaongea, kesho na keshokutwa inaweza isionekane. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nawashukuru Wabunge wote ambao wamechangia wakipaza sauti zao kwamba sasa kupitia Bunge hili tupate nafasi ya kuyalinda mazuri yote haya ambayo anayafanya Mheshimiwa Rais. Mazuri haya tutaweza kuyalinda kwa kuhakikisha kwamba yale yote ambayo yanapitishwa ndani ya Bunge yanasimamiwa na yanatekelezwa.
Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha, kwa dhahiri kabisa amesema yeye mwenyewe kwamba hata Bajeti ya CAG imeongezeka na bajeti ya ukaguzi wa ndani imeongezeka. Sasa kazi kubwa ambayo anaifanya Mheshimiwa Rais, Bunge tunapopitisha bajeti ambayo imeongezeka kama hivyo, maana yake inampa freedom CAG na wakaguzi wa ndani kuweza kufanya ukaguzi mzuri wa hizi fedha ambazo tunazipitisha kwa niaba ya Watanzania na fedha ambazo Mheshimiwa Rais anazihangaikia usiku na mchana ziweze kuja kuwasaidia. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa kumalizia, niwashukuru Wabunge wote ambao wamechangia, ninaamini mengine sasa yanabaki mezani kwako kwa ajili ya utekelezaji kwa sababu ni Maazimio ya Bunge. Yale yote ambayo yameombwa na baadhi ya Wabunge nadhani umeyasikia, muda ukiwadia, kwa sababu Ripoti ya CAG bado haijaja humu, ndiyo maana sikuiongelea katika azimio hili.
Itakapofika, ikishapokelewa ikawa mali ya umma ikapita ndani ya Bunge, nadhani Kiongozi wetu wa Mhimili atajua jinsi gani ataenda nayo.
Mheshimiwa Spika, baada ya kuyasema haya, naomba kutoa hoja.
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika, naafiki. (Makofi)