Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nominated
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nikushukuru. Pia nimshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kutujalia afya njema na kuwepo hapa. Nimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa Hotuba nzuri ambayo ametuletea hapa, tuzidi kumwombea Mwenyezi Mungu, amjalie aweze kufanya kazi kwa njia akiwa na afya njema na atubariki sana tumepata bahati nzuri kuwa na Waziri Mkuu msikivu, mpole, mwenye hekima, ana uwezo mkubwa, Mwenyezi Mungu mbariki zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile nipo hapa kumshukuru sana sana Mheshimiwa Rais wangu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, ni mwanamke jasiri ambaye ana upendo kwa kila kona anaonyesha nini anachokifanya na mimi nitazungumza kwa yale ninayoyaona kwa macho yangu kama ushuhuda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania asilimia 67 ni vijana na hawa vijana ni kundi kubwa ambalo inabidi lifanyiwe kazi ili kuweza kuleta uchumi wa nchi. Leo tunaona vijana wanamaliza vyuo vikuu, wanamaliza katika maeneo mbalimbali lakini hawana ajira na Wizara tuliyokuwa nayo hii sasa ya Wizara ya Vijana, Kazi na Maendeleo ya Jamii kuna hitaji msukumo mkubwa sana wa kuhakikisha kuwawezesha hawa vijana baadaye usije ukawa mzigo wa nchi. Nitazungumza kwa ninayoyafahamu, leo hili vijana hawa waweze kupata ajira, wajiajiri wenyewe, Serikali ni lazima ihakikishe inawapelekea fedha na inapeleka fedha kwa wakati ili waweze kusomeshwa na wajiajiri wenyewe baadhi ili kuweza kusukuma uchumi wa nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi nilikuwa katika mkutano wa madini. Tumeambiwa wachimbaji wadogo wadogo ambao ni vijana na wanawake wameweza kuleta pato la Taifa asilimia 40 vis-a-vis wawekezaji wakubwa lakini changamoto waliyokuwa nayo wale wanasema hawana mitaji, hawana vitendea kazi. Sasa kama hawa wanaweza kuleta pato la uchumi mkubwa kwa asilimia 40, unayaachaje makundi haya yasiwezeshwe? Tunakwenda katika bajeti kuna SGL ambayo inabidi iende asilimia 30 iende kwa vijana, walemavu, wanawake lakini nimeshangaa imepelekwa bilioni tisa badala ya bilioni 87.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukajaribu kujadiliana wakasema baadhi ya pesa hizi zinakwenda kwa mifuko (mkopo) board loan, sawa, lakini haiwezekani bilioni 87 zote wapeleke katika mikopo ya wanafunzi, wanaliacha hili kundi kubwa ambalo linaingia mtaani, halina kazi, halina mtaji, wanategemea kuzalisha kitu gani? China, India, Singapore, Malaysia walisimama na vijana na walihakikisha wanasoma katika vocational training centers ili badaye waje waweze kujitegemea wao wenyewe kwa kuweza kufanya kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunaambiwa katika eneo hili hapatengwi pesa ya kutosha, wanasema hawaweki pesa, kama huweki pesa unategemea hili kundi wanalipeweka wapi? Hili kundi litatuletea zogo baadaye maana yake vijana wakikaa baadaye akijiona amemaliza PhD, sina kazi, si ajiriwi, watu wanaajiriwa kwa mafungu ambayo ni ya watu wachache, makundi maalum, hawa vijana ni lazima, naomba hizi pesa tulikubaliana juzi na Waziri wa Fedha, atakuwa shahidi walisema watakwenda kukaa, nataka waje watuambie hapa wametenga kiasi gani angalau basi watupe robo. Katika bilioni 87 wakitupa robo angalau kundi hili la watu 42,000 ambao tumepanga waanze kupata mafunzo liweze kufanya kazi. Si hivyo tunawapa mzigo mkubwa Wizara ya Kazi na Vijana wakati hawana kazi ya kufanya nao na tutahakikisha vijana hawa badala ya kupata mafunzo maalum, itakuwa vijana hawa ni vibaka, ombaomba mitaani na tutaendekeza wengine wajiingize katika masuala ya ushoga. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumetembelea maeneo mbalimbali, tumekwenda Tengeru Meru. Vijana wana degree zao wameamua kutengeneza greenhouse zao, wale vijana sasa hivi wanauza mboga, wanauza matunda, wanapeleka maua nje ya nchi. Matokeo hayo ni kwa sababu wamepewa incentive, tujifunze Halmashauri ya Meru nini wamefanya kuwasaidia wale vijana ili halmashauri zingine Tanzania nzima wajifunze ili kuhakikisha vijana waliopo kule wanapata mafunzo na wanapewa greenhouses ili wawatoe katika umaskini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kundi maalum la watu wenye ulemavu; toka mwaka 2015 tunazungumza mpaka leo hawajaweka bajeti hata senti tano katika Kifungu cha Vijana na Mikopo. Leo walemavu nina PhD za walevu zaidi ya sitini hawana ajira, nina masters za walemavu hawana ajira, nina degree za walemavu hawana ajira, basi hata fungu lao la hela hawawekewi allocation ya funds hata kidogo. Walisema watatupa bilioni tatu, mpaka leo napata kigugumizi kusema kuwa hata senti tano haijawekwa. Mimi ni mlengwa, ni mlemavu niliyepata ulemavu nikiwa hapa Bungeni, naona maumivu makubwa ambao wanapata watu wenye ulemavu katika kuwa kwanza hawaajiriwi, wanawaona kama siyo haki yao ya kuajiriwa, lakini hata hii mikopo yao ya kuwasaidia hili waweze kujiendesha wenyewe nayo ni kigugumizi. Hii ni Wizara na hii kama ni Wizara wote watu wa Wizara wananisikiliza, hili kundi maalum la watu wenye ulemavu na hizi bilioni tano ambazo Waziri wa Fedha alisema atazitoa, naomba zifanye kazi na zitolewe ili hawa watu isije ikawa baadaye ni mzigo na kulaumiwa wanaitwa ombaomba sijui maskini, lakini si maskini hawa wana akili tosha na wana uwezo tosha wa kufanya kazi. Mfano Mbogwe, STAMICO tena Wizara ya Madini inasimama na watu wenye ulemavu wamewapa vitalu, wanachimba dhahabu, kwa maana moja hata mlemavu ukimwezesha anaweza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitazungumzia barabara Mkoa wa Lindi, ni toka tumepata Uhuru na Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanzania hii alikuwa Mheshimiwa Rashid Mfaume Kawawa, anatoka Liwale. Barabara ya kutoka Nangurukulu mpaka Liwale mpaka leo ni kigugumizi, hakuna jibu linalotolewa na Serikali, tumedanganywa sana kuhusu barabara ya Liwale, barabara hiyo ya Liwale hata kumuenzi Mheshimiwa Rashid Mfaume Kawawa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Nchi hii. Barabara ile haitengewi, watu wa Liwale leo wanakwenda huko kwa siku mbili anatoka hapa anakwenda mpaka Lindi, Lindi Nachingwea, Nachingwea anakwenda mpaka Liwale. Naomba nipate majibu kwa nini Barabara ya Lindi ya Nangurukuru – Liwale mpaka Nachingwea imekuwa kigugumizi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, nitazungumzia masuala ya kijinsia. Ukisikia neno demokrasia ndani kuna jinsia, Tanzania ni Nchi huru, Tanzania tuna utamaduni wetu, Tanzania tuna culture yetu sasa hatutaki kuingizwa katika mambo ambayo wao wanayataka kwa ufirauni wao ili kutuletea Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kitabu cha Quran nitazungumza kwanza huko, wanasema “Walaa taqrabu zinaa, innahu kana faahishatan wa saa sabiila” akasema tena “Azaniyatu wazanii fajilidu kulla wahda miatu-l-jadda” hakika vitabu vyote Biblia na Quran vinakataza zinaa, lakini siyo zinaa tu, ikija huko ndiyo hatari kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitaje miji ambayo ni hitarishi sasa hivi ambayo inaangamia kwa ajili ya ushoga. Kwanza Zanzibar, watalii wanaokwenda Zanzibar wako huru wanakuja wanaume kwa wanaume, wanalala mahotelini, tunataka Zanzibar ionyeshe mfano. (Makofi)
MWENYEKITI: Mheshimiwa Riziki Lulida, ahsante sana.
MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.