Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Spika, awali ya yote nichukue nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya hasa ndani ya jimbo langu la Kwela.

Mheshimiwa Spika, pili nikupongeze sana Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri unayoifanya, hasa kwa ziara yake aliyoifanya jimboni Kwela mwezi Desemba, 2022.

Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia kwa njia ya maandishi kwenye bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu; kwanza nianze kwa kumkumbusha Mheshimiwa Waziri Mkuu juu ya ahadi yake aliyoitoa siku alipofanya ziara Jimboni kwangu, juu ya ujenzi wa hospitali yenye hadhi ya wilaya katika Mji Mdogo wa Laela ambao pia ndio Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.

Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiodhihirika kwamba Hospitali ya Wilaya iliyojengwa kwenye jimbo langu ipo umbali wa zaidi ya kilometa 330 ambapo imekuwa ngumu kufikiwa na wananchi hasa waliopo Ukanda wa Ufipa ya Juu ambao ni takribani wananchi 200,000.

Mheshimiwa Spika, pia naomba nichangie kuhusu mgogoro wa ardhi uliopo kati ya mwekezaji wa shamba la Malonje yaani Efatha Ministry. Mgogoro huu umechukua muda mrefu sana. Nilisema humu Bungeni mwaka jana na Serikali ikaahidi kuchukua hatua, lakini mpaka sasa hamna hatua yoyote. Nikuombe Mheshimiwa Waziri Mkuu utusaidie ili tuweze kumaliza tatizo hili lililochukua muda mrefu.

Lakini pia mgogoro wa Gereza la Mollo lililopo Wilaya ya Sumbawanga na wananchi wa Kata ya Msanda Muungano juu ya kukabidhiwa ekari 495 walizoahidiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani alipozuru eneo hilo. Lakini ni mwaka wa tatu sasa hamna hatua yoyote iliyochukuliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya kukabidhi ardhi hiyo.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.