Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru tena kwa kunipa nafasi hii ili niweze kujibu hoja mbalimbali ambazo Waheshimiwa Wabunge 77 wamechangia. Kwa muda mfupi huu wa jioni, Wabunge 77 wameweza kuchangia hoja hii na kati yao 20 wamechangia kwa mdomo na wengine 57 wamechangia kwa maandishi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kabla sijaanza kujibu hoja, naomba niwataarifu Wabunge vitu vitatu. Cha kwanza, niko Serikalini sasa hivi kwa miaka 35. Nimeanza kazi mwaka 1984. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, cha pili, natambulika kwa jina la utani Mr. STK (Mzee wa STK) kwa maana ya sheria, taratibu na kanuni na la tatu ni kwamba nimewasilisha fomu yangu ya kwanza Tume ya Maadili mwaka 1998. Vitu vitatu hivyo vinatosha kuwapeni taarifa na mjue mimi ni mtu wa namna gani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, huwa sipendi kusema sana, napenda kutenda. Kwa sababu hiyo basi nitajibu kwa kifupi sana lakini tutajitahidi kuwaleteeni majibu kwa maandishi kwa hoja zenu zote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya muda nitajibu hoja chache ambazo zimetolewa kwanza na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama halafu nitajibu kile ambacho Mheshimiwa Lema aliniomba nijibu na jibu langu ni fupi sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kweli baada ya kusoma ile bajeti mbadala nimesikitika sana, bila CCM nchi hii haina uongozi mwingine. Kwa sababu hotuba yote ina-refer magazeti na inapiga vijembe na hakuna bajeti mbadala. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hivyo ndivyo, bado tuna kazi kubwa sana ya kuandaa Kambi ya Upinzani maana iliyopo ni Kambi ya Upingaji. Kwa sababu kilichoandikwa ni kwamba kutokana na magazeti, tunasikia, huwezi kutueleza hapa yaliyoandikwa kwenye magazeti na uliyosikia, tuambie unayoyawaza wewe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, natambua wako wapiga kelele, natambua wako wajenga hoja wachache na hoja zao walizozisema Serikali itazichukua na itazifanyia kazi maana ni za maana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na Kamati ya Kudumu ya Bunge, mengi yaliyosemwa ni mapendekezo au ushauri mbalimbali na ushauri huo Serikali itauchukua na kuufanyia kazi maana Serikali hii ni sikivu na haipigi kelele, it doesn’t shout. Utawasikia tu wataanza ku-shout, we don’t work like that, we are professionals na ndiyo sababu nina miaka 35 Serikalini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwenyekiti wa Kamati au Kamati inapendekeza kwamba Serikali itoe fedha kwa ajili ya kulipa madeni ya watumishi, wazabuni na wakandarasi katika mafungu yaliyopo katika Wizara yetu. Nilifahamishe Bunge lako, sasa hivi Serikali imeamua kuweka madeni yote kwa pamoja. Kinachofanyika ni kwamba madeni yanahakikiwa na yakishahakikiwa kutoka Fungu Kuu (Treasury) yanalipwa na baadhi ya wafanyakazi pamoja na wakandarasi wa Wizara yangu tayari naadhi yao wameshalipwa na tunaendelea kuhakiki na wale ambao tunaona ni halali tutafanya hivyo kwa kuwalipa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliambiwa NIDA kuna wafanyakazi ambao wanaidai Serikali, tulipoita wale wafanyakazi 50 hawakuonekana kabisa na wengine ukiisoma mikataba yao huwezi kuelewa ndiyo sababu tunafanya uhakiki kwa kushirikiana na Treasury. Pale ambapo tutajiridhisha kwamba huyu kweli anaidai NIDA na ni mfanyakazi halali, watalipwa, pesa iko katika akaunti ya NIDA. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuwezi kuendelea na hali ile ya zamani ya watu kufanya longolongo na msitusukume kuingia katika mambo ambayo hatuyapendi na ndiyo sababu tumeyafanyia kazi. Kwa taarifa yenu tu pale NIDA sasa hivi tuna vyombo vitatu vinahakiki yote yaliyotokea nyuma. Wa kwanza, Controller and Auditor General yuko pale, PCCB wako pale na PPRA wako pale. Hizi ni initiative ambazo Wizara yetu tumezifanya katika kuhakikisha kwamba maeneo yote tuliyokuwa tukiyatilia mashaka tunapeleka vyombo hivyo vitatu ikiwa ni pamoja na Uhamiaji. Tutafanya hivyo maeneo yote tutakayoona kwamba kuna wasiwasi. Mtuamini, sisi ni watu wa Hapa Kazi Tu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo limezungumzwa ni lile la usimamizi wa sheria barabarani. Hili nalo tunalifanyia kazi kwa nguvu zetu zote. Tayari aidha, tumewaondoa baadhi ya askari katika Kitengo cha Usalama Barabarani au tumewafukuza, hakuna maneno. Tunatambua kwamba kuna Watanzania wengi ambao hawana kazi, mtu yeyote tutakayempa kazi na akaichezea atupishe tutapeleka watu wengine chuo chetu kule Moshi, watapata training waje waajiriwe Jeshi la Polisi. Hivyo ndivyo ilivyo na ndiyo sababu nikawapa kwanza yale maelezo ya mwanzo manne. Ni Jeshi la Polisi jipya, ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mpya, tupitishieni bajeti tukafanye kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye hoja mbalimbali zilizochangiwa na Wabunge. Uchakavu wa vituo vya polisi na nyumba na hili limezungumzwa na Mheshimiwa Kangi Lugola amesema atakuletea ile picha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli nilivyotembelea mimi mwenyewe nilisikitika na ndiyo sababu tukafanya juhudi kuhakikisha kwamba tunajenga nyumba za askari. Tunajenga nyumba za polisi 4,136 kwa mpangilio uliopo sasa hivi lakini vilevile tunajenga nyumba 9,500 za magereza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala haliwezi kuchukua mwaka mmoja. Unapoanza kujenga nyumba labda sijui tuchukue wakandarasi wangapi, tunapopanga kuna kitu kinaitwa absorption capacity, tukisema kwamba mbona nyumba ni 4,136 tu, je, tukisema tujenge nyumba 10,000 tutazijenga mwaka mmoja na kwa utaratibu upi?
Kwa hiyo, hayo ya nyuma yameshatokea, kilichopo ni kuboresha tukienda mbele na tunasema tunaanza na nyumba 4,136 kwa polisi, nyumba 9,500 kwa magereza na hili halitafanyika katika kipindi cha mwaka mmoja tu. Tumeona mfano wa nyumba za polisi tulizozijenga Kurasini, zinazojengwa Mwanza, tumeona nyumba ambazo tumezijenga kwa Jeshi la Wananchi hazikuchukua mwaka mmoja, lakini tuna mpango huo na tutahakikisha kwamba tunaendelea kujenga kwa kadri uwezo utakavyokuwa unaendelea. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo limejitokeza sehemu mbalimbali ni uhaba mkubwa wa mafuta na vipuri. Ni kweli katika magari yetu ya Polisi, Magereza, Uhamiaji na Zimamoto kuna uhaba wa mafuta na vipuri, hili na sisi tumeliona, tunashukuru kwa vile na ninyi mnaliona lakini tushirikiane kwa pamoja kupeana taarifa pale ambapo kunakuwa na ukosefu wa vifaa hivi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pendekezo lililotolewa na baadhi ya wenzetu ni kwamba mafuta yaende moja kwa moja kwa OCDs yasipitie kwa RPCs, pendekezo hili tunalichukua, tukalifanyie kazi na tukiliona linawezekana kufanyika basi tutafanya hivyo lakini kwanza tulifanyie utafiti tuone kama linawezekana kufanyika. Kama haliwezi kufanyika basi tutaona namna ambavyo tunaweza ku-improve system iliyopo sasa hivi iweze kuwa ya haraka zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mweneyekiti, eneo lingine ambalo limezungumziwa kwa hisia sana ni ulinzi binafsi kutokuwa na sheria. Hili na sisi katika Wizara tumeliona, tumewapa Jeshi la Polisi waweze kuangalia na kuona kama tunaweza kuwa na sheria ya haraka zaidi ambayo tunaweza tukaipitisha ili tuweze ku-regulate huu ulinzi binafsi. Nadhani ni wazo zuri na sisi tunalichukua. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo limezungumzwa ni msongamano katika magereza yetu. Ni kweli, mimi nimetembelea magereza yote Dar es Salaam na mengine mikoani, msongamano kwa kweli ni mkubwa. Kama nilivyosema kwenye bajeti yetu kwa mwaka huu tutakarabati mabweni 49 na tutajenga mengine na tutaendelea kujenga magereza sehemu mbalimbali hasa hasa kwenye maeneo mapya ya utawala kama ambavyo imependekezwa lakini hii itategemea na upatikanaji wa fedha mwaka hadi mwaka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuzungumzie suala la mikataba. Mikataba yote ina matatizo, Mheshimiwa Masoud ndivyo alivyokuwa anasema. Nadhani solution siyo kuleta mikataba hapa kwa sababu hadi leo hii kuna utaratibu maalum kama Mbunge au Kamati ingependa kuona mkataba, utaratibu upo wazi kabisa. Sidhani kama tutakuwa tunachukua mikataba halafu tunakuja tunaigawa humu yote kila mtu aone kwa sababu kila mtu ana nia yake. Lazima itambulike kwamba mkataba kati ya institution na supplier ni mikataba ya watu wawili, sidhani kama wewe ungependa mkataba wako na mtu fulani upelekwe mahali pengine au kwa mzazi wako lakini utaratibu upo hata mkitaka kuona mkataba wa Lugumi, tungeweza kufanya hivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niwaonye na niwaambie ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge haya mambo ya security tunaiweka nchi katika hali ya utata. Tuyafanye kwa utaratibu ambao hauta-disclose information kujua kwamba kumbe polisi wana mkataba na mtu fulani kwa hiyo wana system fulani hao wahalifu watajua system uliyonayo na wataikwepa. Kinachotakiwa hapa, tutumie utaratibu wetu wa kawaida ambao upo hata mkitaka mikataba yote mtaiona, upo na upo very clear.
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tunapiga kelele, tunaandika kwenye magezeti, we are putting our country at risk. Nichukulie tu mfano huu mkataba wa AFIS, sasa hivi kila mtu anajua kwamba Tanzania wanatumia mashine fulani za kutoa finger prints. Sasa ukishafanya hivyo mtu aliyekuwa anataka kutenda jambo bovu ataji-protect. Hivi sasa hao wanaotenda mabovu wakianza kuvaa gloves, don’t you see that you are putting your country at risk?
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nachowaomba jamani tukihitaji mikataba au tukihitaji kujua facts tufuate utaratibu wa Kibunge badala ya kwenda ku-shout na kupeleka haya mambo kwenye magazeti. Hakuna mtu anayeficha kitu, after all sisi wenyewe tunapenda sana kupata ushauri wa watu ambao ni the right channel, lakini tutumie utaratibu ulio sahihi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nashangaa sana, ndiyo sababu hamjaniona hata siku moja nimejibu chochote kwenye magazeti, lakini we shout a lot kwenye magazeti. Hilo nawashauri kama Wabunge wenzangu ninyi mna responsibility ya kulinda usalama wa nchi yetu. Kama Wabunge tumieni the right channel ku-request information mnayoihitaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo limezungumzwa na watu wengi sana ni maslahi ya askari mbalimbali. Kweli mimi nakubaliana nalo. Ukiangalia hotuba yangu kuna maeneo mbalimbali ambayo tunajaribu kuboresha maslahi ya askari na hili kwa kweli mimi nitalipigania kwa sababu wanafanya kazi katika mazingira mengine siyo mazuri sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu ambacho nataka nikiseme, kuna jambo limesemwa na upande huu kwamba askari wanatumiwa na Chama cha Mapinduzi. Jamani mtakapomaliza hapa si mtakwenda kwenye mikutano ya hadhara, niambie askari achana nao, ninyi hamuwatumii askari kwenye mikutano yenu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi unajua huwa ni mkweli kupita kiasi na nasimamia Wizara hii kwa kufuata STK, nitahakikisha kwamba sheria, taratibu na kanuni zinafuatwa, basi.
Sasa kama mimi ni mwaminifu au nini lakini ukweli unabaki pale pale, tufanyeni kazi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni. Askari yeyote ambaye hatafuata sheria, taratibu hata kanuni nimesema consequence atakazozipata. Kama kuna askari ame-misbehave mwambie Mkuu wa Wilaya, RPC au OCD wake na kama unashindwa namba yangu iko wazi nipigieni, uwe Mbunge wa CCM, CHADEMA, CUF na hilo mnalitambua, Mheshimiwa Masoud unalitambua. Mheshimiwa Masoud anatambua kwamba mimi sibagui kwa sababu Jeshi letu la Polisi linalinda usalama wa raia na mali za Watanzania wote. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suggestion kwamba tuongeze boti za doria hasa baharini. Hilo na sisi tumeshaliona na siyo baharini tu, wale wenzetu wanaotoka Mkoa wa Kagera, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa wana tatizo hilo. Kwa hiyo, tunaliangalia comprehensively tuone ambavyo tunaweza kutatua tatizo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Msigwa anasema alibambikwa kesi, kama kweli alibambikwa kesi njoo niambie. Wewe ni Mheshimiwa una-access ya kuniona wakati wowote tuone ni kwa namna gani tunaweza tukalirekebisha hili.
yaliyokwishazungumzwa na yameshajibiwa na mwenzangu, lakini moja ambalo amelisisitiza ni kwamba tuwe na vituo vya kutosha katika maeneo mbalimbali. Ni kweli kama nilivyosoma kwenye hotuba yangu tunakwenda polepole, lakini ni kwa kulingana na uwezo tuweze kujenga vituo katika maeneo mbalimbali hasa Wilaya mpya au maeneo mapya ya utawala.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Lwakatare amezungumzia suala la kubambikwa kesi nimeshalijibu.
Mheshimiwa Khatib nadhani nimekusikia na tuna mpango wa pamoja wa kutembelea maeneo aliyoyasema, tumeshaongea, nitaenda hata kwako, usifikiri siendi upande wa CUF naenda tu, wote ni raia. Mbunge yeyote ambaye ana nia ya kwenda na mimi tujadiliane, tuone tukiwa na nafasi tutakwenda tu tuone kwa sababu nia ni kuhakikisha kwamba nchi nzima inakuwa salama na kuna usalama. Kwa sababu anapotoka Mheshimiwa Khatib pale siyo wote ni CUF, kuna wengine ambao ni CHADEMA, kuna wengine ambao ni CCM na Serikali yetu kama ambavyo Mheshimiwa Rais wetu anavyosema ni Serikali ya Watanzania wote na yeye ni Rais wa Watanzania wote na mimi ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ya Watanzania wote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani niishie hapo kwa kusema naomba kutoa hoja.