Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
2
Ministries
nil
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nakushukuru, nitakwenda kwa haraka sana. Naomba Mheshimiwa Waziri awe makini wachukue hizi point, najua watazidadavua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nipongeze Wizara kwa mipango yenye kuleta tija, tunatumaini italeta tija. Lakini nimwambie Mheshimiwa Waziri, jana nilikuwepo pale jioni wakati Mheshimiwa Waziri Mkuu anatoa yale maagizo. Yale maagizo maana yake ni kwamba, bado tunahitaji utambuzi na ufatiliaji wa mifugo, hapa hatuwezi kukwepa; na alitoa yale maagizo ili ukayafanyie kazi ubaki kwenye hicho kiti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, bado ufugaji katika nchi yetu ni kama adhabu. Ni kama adhabu kwa sababu kuna mambo bado tunahitaji tulete mabadiliko ndani ya sekta hii ya mifugo. Nchi imesema ina ng’ombe milioni 36 lakini bado wafugaji wale hawana access kwenye elimu ya mifugo, hawana access kwenye afya za mifugo yao, hawana access kwenye kujua malisho, hawana access hata ya elimu inayotolewa kwenye ufugaji wenyewe. Sasa hayo ni mambo ambayo Mheshimiwa Waziri wanatakiwa wayafanyie kazi; na wanaweza tu kuyafanyia kazi ikiwa kuna ufatiliaji, na ndani ya ufatiliaji ndipo tunapata hizo research, ndiyo maana ya research. Kwa hiyo hapo ndio utapata tafiti za kujua kwamba wafugaji wangu wana elimu, wanafaidika kweli, hawa wafugaji wangu wanajua afya za mifugo yao, magonjwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kuna haya mabadiliko ya tabianchi. Mabadiliko ya tabianchi yanaingia katika kila sekta. Kwa hiyo mfugaji asipokuwa na elimu ya mifugo, elimu ya aina ya maradhi yanayokuja au magonjwa hatufiki huko. Kwa hiyo suala la ufatiliaji, suala la kutambua mifugo ni muhimu, hilo ninamwambia Mheshimiwa Waziri asilipindishe na alifanye kwa uhakika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nini tukifanye sasa hivi, tukishafanya huo utambuzi maeneo muhimu ya malisho hayo wanayoyasema ya chakula yatajulikana, upatikanaji wa masoko pia utajulikana. Lakini pia tutaweza kuzuia ulaghai wa kuingiza wanyama kutoka nje ya nchi pamoja na ulaghai wa kuuza nyama isiyokuwa na ubora.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakwenda haraka, na sasa ninakwenda kwenye hiyo Wizara yenyewe ya Mifugo. Nimuombe, nilizungumza kipindi kilichopita, katika Wizara ambazo zinaweza kusaidia, kama alivyosema Mheshimiwa Mhagama, Wizara zinazoweza kusaidia kuleta ajira hii ya kwake ni mojawapo, wasikwepe. Ile program ya BBT ije kwake kama BBT2 na ile ya kilimo ya Bashe iwe one. Yeye alete BBT2 atafanikiwa. Ni lazima wafungue hiyo ili wahitumu hawa wapate maeneo ya kupata ajira. Kwa hiyo atakapokuja kwenye speech yake ya mwisho aweke mikakati yako tuone kama hili ameliweka, litakuongezea; na hilo ndilo linaweza kusababisha kuongezwa kwa bajeti, wakaona kwamba huyu ana mpango wa BBT2 kwa vijana. Kwa hiyo hapo anaweza akaongezewa hata bajeti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye suala la uvuvi. Wenzangu wamesema, tuna Bahari na maziwa lakini pato linalotokana na huo uvuvi ni 1.7%, hiyo ni ndogo sana. Sasa mimi nataka nitoe ushauri kwenye eneo la uzalishaji wa vifaranga vya Samaki, anzeni kufatilia pale SUA. Kile chuo ukienda pale na mitambo yao utafurahi; sijui kama amewahi kutembelea pale, waende wakaone, wanazalisha vifaranga vya Samaki. Sasa wao wakiwasaidia, wakaungana, kwa sababu chuo ni cha Wizara ya Elimu lakini wale Samaki na mifugo iliyopo SUA ni vya kwake yeye. Waende wakaungane na chuo waone ni namna gani wanaweza kujaribu kutengeneza vifaranga vingi vikasambaza si Morogoro tu vikaenda mpaka mikoa mingine kwa sababu hawa walisema wanazalisha wanasambaza pale Morogoro.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ile ni project kubwa, kwa hiyo wao wawasaidie ili iwe project ambayo ni kubwa zaidi, maana nasikia nchi hii kuna sehemu mbili tu wanazalisha vifaranga vya Samaki. Sasa kile chuo pia kitawasaidia kuwainua wao. Kwamba wanatumia vyuo vyetu, lakini pia hata kile chuo chenyewe kinaweza kikasaidika na kufanya mradi wake ukue zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi baada ya kusema hayo niseme nampongeza, lakini ili bajeti yake iongezeke achukue hii ya BBT2 atakuja kunikumbuka siku moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)