Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo

Hon. Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Nashukuru kwa kunipa nafasi namimi pia niungane na wachangiaji waliyopita kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kunyanyua kilimo cha nchi hii. Maana tunajua vipaumbele ni vingi lakini unapoona umeamua kuelekeza pesa polini ukakate mapoli hatimaye upate chakula na urudi mijini watu wafurahie ni uamuzi wa busara na ni uamuzi wa kijasiri lakini pia nimpongeze Mheshimiwa Bashe na msaidizi wake na Watendaji wote wa Wizara hii kwa maono makubwa ambayo Bashe amekuwepo nayo maana amejipambanua kama Mkulima na maono haya yanatimia kwa sababu amepata Mheshimiwa Rais kumshika mkono na tunaona mambo yanaenda na pesa hizi ambazo zinatoka na zinaendelea kwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile pia niishukuru Serikali hata sisi Biharamulo kwa mara ya kwanza katika historia tumeenda kujengewa skimu ya irrigation siyo jambo dogo hili kwa hiyo neema hii na sisi imetuangukia. Ukurasa wa 207 wa Hotuba yako Mheshimiwa Waziri, tutajengewa Mradi wa Mwiruzi hekta karibu karibu 1,300 kwa hiyo hili jambo kubwa kwa wakazi wa Biharamulo tukushukuru. Hata hivyo sasa baada ya hayo nijikite mimi kwenye mambo mawili au matatu, mawili kama muda utapatikana yatakuwa matatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huwezi kutaja zao la kahawa bila kuitaja Kagera kwa sababu history inaonyesha mnamo karne ya 16 wenyeji wa Mkoa wa Kagera ndiyo waliyoingiza kahawa Tanzania wakitokea Ethiopia. Kahawa aina wa robusta na kwenye mauzo mpaka sasa kwenye andiko hili nililonalo la Tanzania coffee industry development strategy ya 21 – 25 la Bodi ya kahawa ukurasa wa 19 nimepitia nikawa naangali uzalishaji wa kahawa na trend ilivyo. Kahawa aina ya robusta kwa sehemu kubwa inazalishwa Kagera na percentage ya uzalishaji ya asilimia 44 so far kati ya asilimia 100 sasa tukija kuangalia expansion na project hii ambayo inafanyika kuna habari ya kugawa miche ya kahawa. Tumeona watu wa robusta tulicho pangiwa katika miche milioni 20 tumepangiwa kuwa tunapewa miche milioni tano tano sasa unajiuliza wewe unaezalisha 44 percent unapewa five million mwenye fifty six anapewa fifteen million sasa hiyo unajiuliza nikuirudisha Kagera chini au kuinyanyua Kagera ili iweze kuendelee kufanya kazi kama kweli unataka kuturudisha kwenye zao la kahawa kama vinara wa kahawa ebu hata miche inayopangwa tupewe forty four percent kama share yetu ambayo tunamiliki katika soko ili hiyo iwasaidie wakazi wa Kagera waweze kunyanyuka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo ukiangialia gharama ya uzalishaji wa hii miche ni kubwa sasa Mheshimiwa Waziri mimi nilitaka nikuombe na nitoe ushauri, wenzetu ya Uganda wanachokifanya wanatumia tissue culture. Tuko kwenye volume mass production ya miche ya kahawa ndiyo inabidi twende nayo. Mheshimiwa Waziri sasa tukuombe najua wewe ni mbunifu, umekuwa kinara wa ubunifu kama ulivyoanzisha BBT rudi maabara nyanyuka na tissue culture hii tukimbizane na wenzetu Waganda itatusaidi kututoa hapa tulipo. Pesa kubwa unayotengwa cha kwanza haitokuwa na magonjwa ya kahawa kwa hiyo itatusaidia tutapata mass production ya miche lakini hakutakuwa na ugonjwa hata tunapo otesha hii miche itastawi na itakuwa kwa ajili ya manufaa ya hao wananchi hilo nikuombe uliangalie halafu tupewe share yetu ya forty four percent ukishamaliza kuzalisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile pili hata migomba Mheshimiwa Waziri. Migomba ya Kagera tumeta ugonjwa sana wa mnayauko rudini maabara ulitupeleka Kibaha maabara nzuri sana pale iliyojengwa rudi pale weka tissue culture hata kwenye habari ya migomba ili iweze kutusaidia kwa hayo nikuombe uweze kutusaiodia ili sasa Kagera turudi kwenye hadhi yetu ya kahawa na migomba hatimaye uchumi huu ambao Mama Samia anaunyanyua na sisi uweze kutugusa. Iko habari ya Tumbaku Mheshimiwa Waziri, niliongea hapa kwa ajili ya wakulima wa tumbaku wa Biharamulo tunapeleka tumbaku kilomita 250 kwenda kuuza kwenye Mkoa wa Kitumba wa Kahama. Tunakuomba wakulima wa Biharamulo wana wasiwasi kwanza kama vile kuwapeleka Kahama wanaanza kuwa na wasi wasi kama wanaenda kuibiwa. Kwa sababu wanasema ikishafika pale akapangua grade hawezi kuibeba airudishe nyakaura au airudishe Kalenga au airudishe Nyanza matokeo yake anakubaliana na bei pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti sasa nimuombe Mheshimiwa Waziri atakapokuwa anamaliza naomba tumbaku ya Biharamulo inunuliwe Baharamulo isitoke nje ya Wilaya yetu. Hilo nakuomba utusaidie na uweze kuisimamia lakini Mheshimiwa Waziri niliomba pia habari ya mbolea ya ruzuku ya tumbaku najua World Bank na IMF wanapinga hiyo hasa kwenye mbolea ya NPK tusaidie tafuta jinsi ya kusaidia maana wakulima wote ni wa kwako. Tafuta jinsi ambavyo unaweza najua wewe ni intelligence sina haja ya kukufundisha lakini naamini liko jambo unaweza ukafanya hata wakulima wa tumbaku wakanufaika hujawahi kushindwa jambo Mheshimiwa Bashe, hilo naomba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tuliomba pia kwenye habari ya mbolea wamesema hapa wenzangu mbolea isiyo na ubora. Tangu Serikali ya Awamu ya Nne kumekuwa na malalamiko makubwa sana juu ya quality ya mbolea inayozalishwa hapa nchini sina haja ya kutaja kiwanda. Sasa nikuombe hata wewe mwenyewe at some extent nimekusikia ukiongelea habari ya mbolea isiyo na ubora mpaka ukaifutia ruzuku, sasa tuombe huwezi kufikia huko mtaani hili ni Bunge wananchi wale waliyopelekewa mbolea isiyo na ubora wamepata hasara na ile mbolea wameilipia. Utakapokuwa una wind up tusikie kauli ya Serikali juu ya mwenendo mbovu uliyopigiwa kelele wa kiwanda hiki tupate kauli humu ndani. Wananchi wa Tanzania wanaopewa mbolea feki au mbolea mbovu isiyo na quality waendelee kuumia au mbadilishe mtafute jinsi ya kuwasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile pia katika kitu kingine ambacho niliomba na nilijibiwa kwenye Bunge la mwezi wa pili tunaomba mbolea isogezwe karibu. Mimi nina watu leo wako Kalenge kilomita 70 na unamwambia aje Biharamulo Mjini kuchukua mbolea mifuko miwili au mifuko mitatu kwa sababu mlitujibu kwamba mnapeleka katika ngazi ya AMCOS tunaomba mbolea safari hii zifike vijijini na wananchi wazipokee kulekule kwao hiyo itawasaidia wananchi wasihangaike na hatimaye tutawapunuguzia hata uchovu na usumbufu mwingine wa pesa ambao wanakuwa wanaupata pale wanapoenda kuchukua mbolea mjini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuyasema hayo na kwa sababu ya muda naomba kuunga mkono hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunisikiliza. (Makofi)