Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji

Hon. Anna Richard Lupembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nsimbo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji

MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa naomba nimshukuru Mungu ambae ametupa afya njema na uzima leo tuko hapa tukiendelea kujadili mambo ya maendeleo ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpongeze Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa ambayo anaendelea kuifanya kupitia Wizara ya Maji. Tumeona kazi kubwa, Miradi mikubwa ambayo tumeiona katika nchi yetu ikiendelea kujengwa na wananchi wakiendelea kufaidika na maji hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpongeze Waziri Aweso, kwa kazi kubwa ambayo anaifanya usiku na mchana anawahangaikia Watanzania. Naomba nimpongeze Naibu Waziri wa maji Mhandisi Maryprisca nae vilevile anafanya kazi kubwa sana kuzunguka na kuhakikisha matatizo ya maji yanapotea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpongeze sana Katibu Mkuu, Kemikemba, kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha miradi yote na pesa zote zinakwenda kwa ajili ya miradi mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpongeze Naibu Katibu Mkuu, Cyprian Luwemeja, kwa Kazi kubwa, tunajua alifanya kazi kubwa sana DAWASA na Rais kamuona sasa aje kusaidia wizarani aweze kukimbia na yale aliyoyafanya makubwa DAWASA sasa aweze kuyafanya katika miradi yote ya nchi nzima. Naibu Katibu Mkuu, Cyprian, hongera sana kwa kazi kubwa, watanzania tunakutegemea utahangaika kuhakikisha watanzania tunapata maji safi na salama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpongeze Meneja wangu wa Mkoa wa Katavi pamoja na Meneja wa Wilaya, wanafanya kazi kubwa. Lakupendeza zaidi wanapenda kushirikisha, wanashirikisha Wabunge, hakuna kitu wanweza kufanya wao bila kuwashirikisha Wabunge. Ninaomba niwashukuru sana na niwape pongezi kubwa kwa sababu ushirikishwaji ndio unaofanya mambo yanakuwa mazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze waziri pamoja na Katibu Mkuu, kupitia maelekezo ambayo wamewapa watendaji wao wote katika nchi nzima. Tuseme tu kutokana na maelekezo haya, Managers wote wa mikoa pamoja na wilaya tunafanya nao kazi Vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Jimbo langu la Nsimbo, miradi yote ambayo niliyopewa na kama kuna changamoto wananishirikisha kwa ukaribu tunafanya kazi kwa pamoja. Naomba niwapongeze sana Meneja wa Mkoa pamoja na Meneja wa Wilaya, kila jambo lazima wanishirikishe na miradi yote ya Mkoa wetu wa Katavi lazima watushirikishe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nishukuru hapa karibuni gari limekuja katika Jimbo langu la Nsimbo, visima vimechimbwa. Nilikuwa naomba nishauri, kazi kubwa inafanywa na watendaji na visima vinachimbwa na tumeona mara nyingi visima vingi vikichimbwa vinaachwa muda mrefu. Vinaweza vikakaa hata miezi sita pengine visima vinakaa mwaka mzima.

mhesh ninaomba nitoe ushauri wangu, basi sasa hivi tuchimbe visima kwa sababu wananchi wanaona visima vinachimbwa wanakuwa wana matumaini ya kuwa tunapata maji kesho, lakini hatimaye kile kisima kinakaa muda mrefu, ile hali tena inapungua. Ninaomba nishauri tuchimbe visima, muda huo huo tuvijenge ili wananchi waweze kupata maji safi na salama. Tusikawie kwa sababu tayari mmeshafanya utafiti, watu wa bonde wamepita wameona na mmekuja kuchimba mmeona maji. Basi tuchukue hatua sasa ya kujenga ili wananchi wale waweze kupata maji safi na salama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, natokea Mkoa wa Katavi, suluhisho la maji ndani ya Mkoa wetu wa Katavi, tupate maji kutoka Ziwa Tanganyika. Kwa sababu yale maji ndiyo yatakayofanya maeneo yetu ya Mkoa wetu wa Katavi wakapata maji safi na salama. Lakini naomba nikupongeze Mheshimiwa Waziri, umesema kuwa tutatumia sasa hivi maziwa, tutatumia mito kuhakikisha watanzania wanapata maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nikupongeze sana ili basi hatua hii tuichukue haraka. Tunajua hii miradi ni mikubwa ambayo itachukua muda mrefu ili wananchi waweze kupata maji. Tunakutakia kila la heri kuhakikisha maji haya ya maziwa yanafika sasa kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nichangie kuhusu miradi mbalimbali mikubwa inayopita katika maeneo yetu. Miradi hii mikubwa inaweza ikapita katika vitongoji na vijiji. Ninaomba sana miradi hii inayopita katika maeneo mbalimbali inasafiri, tunaomba yale maeneo ya vijiji na vitongoji husika ambako mradi ule unapita, wale wananchi waliopitiwa na ule mradi wapate maji. Kwa sababu tunapita wale wananchi wanakuwa hawana maji, matokeo yake uharibifu unatokea. Lakini tukiwapatia maji vitongoji vile vinavyopitiwa na mradi ule pamoja na sehemu nyingine kuna wafugaji, wafugaji wale wanaona bomba lile kubwa limepita na hawana maji, ile mifugo inahangaika matokeo yake wanapasua yale mabomba ili wanyama wale waweze kupata maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninaomba kuishauri wizara, tuhakikishe yale maeneo ambayo miradi ile mikubwa inayopita kama kuna wananchi wanaishi pale, kuna mifugo, tujenge mabwawa na wale wananchi waweze kupata maji safi na salama ili ule mradi tuulinde na yale mabomba tuweze kuyalinda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna changamoto ya mabomba makubwa na viwanda vyetu havitoshelezi. Leo hii ukiwauliza wakandarasi wanakwambia kuwa tuko kwenye foleni tunahitaji mabomba. Kuna miradi mingi mikubwa imechelewa kwa ajili ya malighafi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nilikuwa naomba, kwa sababu tumekwishaona kuna malighafi mbili, kuna mabomba ya plastic na mabomba ya chuma na mabomba yale ya chuma makubwa kupitisha miradi mikubwa mikubwa viwanda vyetu havitoshelezi. Nilikuwa naomba aidha tushawishi wawekezaji waje kwenye nchi yetu wawekeze ili tuweze kupata mabomba kwa ajili ya malighafi au basi tuainishe nchi ambazo tunaweza tukapata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niunge mkono hoja naomba nipongeze kwa kazi kubwa ya Mheshimiwa Waziri, pamoja na safu yake yote. Ahsante sana. (Makofi)