Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Mashariki

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nichukue nafasi hii nikushukuru sana kwa kunipa hii nafasi ya kuchangia kwenye hii Wizara muhimu, Wizara ya Elimu. Kipekee nimshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambazo anazifanya hususani katika Jimbo la Manyoni Mashariki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri Profesa Mkenda pamoja na Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kazi kubwa wanazozifanya. Mwaka huu manyoni tumepewa chuo cha VETA, na nilikuwa nikiuliza sana swali la VETA, mwaka huu tuna ujenzi wa Chuo cha VETA Manyoni, nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimshukuru vilevile Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Profesa Carolyne, mwalimu wangu wa Chuo Kikuu cha Sokoine. Nimshukuru sana pia Kamishna wa Elimu, Mkurugenzi wa TEA na Mkurugrnzi wa Bodi ya Mikopo. Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo tulikuwa tunapata vilio vingi sana vya vijana wetu lakini kwa kweli mwaka huu mmetutendea haki sana. Kwa hiyo nakushukuru Mheshimiwa Waziri lakini nampongeza sana Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Dkt. Badru vile vile kwa kazi kubwa ambayo ameifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi leo nina hoja mbili. Hoja ya kwanza nitazungumzia kuhusu hii Taasisi ya Elimu ya TEA (Tanzania Education Authority), lakini ya pili muda wangu ukiniruhusu nitachangia kuhusu mfumo wa elimu yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa Taasisi yetu ya Elimu TEA, kwanza nichukue nafasi hii nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kupitia TEA. Tumeona kupitia TEA tumekuwa na programu mbili. Programu ya kwanza ni kupitia ule Mfuko wa Elimu, mmekuwa mkiā€“compliment juhudi zinazofanywa na TAMISEMI kwa kujenga vyumba vya madarasa na kujenga vyoo kwenye shule zetu, na huu ni ubunifu mkubwa sana. Tusitegemee tu TAMISEMI waweze kuweka miundombinu kwenye taasisi zetu za elimu. Lakini Profesa umeliona hili, kuna maeneo ambayo yalikuwa yamesahaulika. Mkigundua lile eneo limesahaulika nyinyi mna-top up kwa kutumia taasisi ya elimu TEA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, hawa wenzetu TEA vile vile wamepewa dhamana ya kuendesha yale mafunzo ya elimu ya ufundi wakishirikiana na VETA na vyuo vyetu vya ufundi. Taarifa niliyonayo ni kwamba zaidi ya vijana 45,000 wameshapata mafunzo haya, na sisi kwa Manyoni tumepata vijana wengi sana. Mpaka kwa sasa hivi nadhani wanafika Zaidi ya vijana hata 400 ambao wamepata haya mafunzo kwa kupitia huu mfumo wa TEA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ushauri wangu ni nini kwenye taasisi hii ya TEA; tumeona impact kwa kupitia hiyo miradi ambayo mnajenga vyoo na madarasa kwenye maeneo ambayo TAMISEMI hawajagusa, lakini tumeona impact kwa kupitia fedha mnazotoa kwa ajili ya kuwapeleka wale vijana wetu wanapata elimu ya ufundi. Ni muda muafaka sasa kuijengea uwezo TEA, kuiongezea nguvu na bajeti ili waweze kuongeza vijana wengi. Pia tunatamani yale maeneo ambayo TAMISEMI haijaweza kupeleka miundombinu kwa kupitia Wizara yako Mheshimiwa Mwenyekiti lakini vilevile profesa ongezeni bajeti ili TEA waweze kufanya mambo makubwa zaidi. Kwa jhiyo kwa upande wa TEA mimi ningeshauri hayo mawili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili ni kuhusu mfumo wetu wa elimu na concept ya kujiajiri. Tupo kwenye mapitio ya mfumo wetu wa elimu, kutengeneza mitaala na vile vile kuhuisha sera yetu ya 2014 ambayo kimsingi haijawahi kufanya kazi. Lakini ningetaka kujiuliza na tujiulize wote sisi kama nchi tunataka nini kwa kupitia elimu yetu ya Tanzania? Nadhani hili ni suala la msingi sana ambalo ni lazima tujiulize.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mawazo ya aina mbili yanayokinzana. Wengi tunafikiri kwamba tunahitaji kuwatoa vijana vyuoni waende wakajiajiri. Lakini tukumbuke vile vile kwamba tunahitaji vijana hawa waingie kwenye soko la ajira, hususani soko rasmi Serikalini lakini hata kwenye private sector. Lakini hoja hii ya kujiajiri vilevile inatafsiriwa toifauti, na hili niliseme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kijana amesoma IT, lakini wengi ukisikia wanaongelea concept ya kujiajiri anakwambia huyu kijana aende akafuge, Profesa ume-invest miaka minne kwa kijana amesoma IT unaenda kumwambia ajiajiri, nadhani that is a very serious mismatch. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitegemea Profesa utuambie kwamba huyu kijana akajiajiri kwenye area his of specialization. Kama amesoma IT tuje na micro business ambazo atatumia ujuzi wake wa IT; na mimi hapo ndipo nilipotaka niweke hoja yangu. Kwa nini nasema hivyo; ni kwamba hawa vijana wengi tunapowahamisha kwenye areas of their specializations, matokeo yake wanakuwa hawana matamanio ya kukaa kwenye zile field. Atakaa kwa muda tu baadaye atakata tamaa. Atatamani siku zote arudi kwenye eneo ambalo alilisomea, kwa hiyo ni eneo ambalo mimi nadhani tunahitaji vilevile kuliangalia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini eneo lingine ambalo nilitaka kuliangalia vilevile ni suala la mapitio ya huu mtaala. Kwenye mapito ya mtaala mmesema kwamba mnataka kuanza kuondoa mtihani wa darasa la saba. Sasa Profesa Mkenda tunaenda kuondoa mtihani wa darasa la saba, tutawapimaje walimu wa shule za msingi? Tunawezaje kuhakikisha kuna accountability kwa walimu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ningeshauri; ule mtihani wa darasa la saba bado ni muhimu unatakiwa uendelee ili tuweze kuwapima uwajibikaji walimu . Tunapoutoa maana yake mwalimu ataona hamna maana yoyote yeye kufundisha wala kuingia darasani kwa sababu hakuna kipimo chochote. Kwa hiyo bado ningeshauri kwamba ule mtihani uendelee ili tuweze kujua ni vijana gani na vijana wa aina gani ambao tunawapeleka huko juu kwa ajili ya kusoma kwa upande wa sekondari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine, tumekuja na hoja nzuri sana, tunataka ku-integrate masomo ya amali na ufundi sekondari; na niliongea siku moja tulikuwa na kikao chetu pale, mimi nikasema kwamba sawa, ni wazo jema tunataka kupeleka sekondari vijana wetu wapate elimu ya ufundi; lakini Profesa bahati nzuri wewe umefundisha Chuo Kikuu cha Dar es salaam mimi nimefundisha Chuo Kikuu cha Dodoma. Lengo la elimu ya msingi ni kutoa general knowledge. Inamuandaa mtu ili baadaye akienda vyuoni aende akasome masomo ambayo yatampa ujuzi, yatampa skills. Kwa hiyo katika level ya shule za msingi na sekondari hatutengenezi skills, pale tunamuandaa mtu ili baadae anapoenda chuoni aweze kuwa na knowledge ya kutosha ili tumjengee skills.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ok, tumekeja na concept kwamba tunataka sasa katika level ya sekondari hawa vijana wafundishwe ujuzi ili weweze kutengeneza let say washone nguo, waweze labda kutengeneza keki na vingine, ni jambo jema, lakini bado mimi nikasema kwamba sasa hivi Serikali inawekeza kwenye VETA, kwa nini sasa tusifikirie badala ya kusema kwamba tutapeleka mzigo mkubwa sekondari ambao vijana wengi tunawaandaa kwa zile general knowledge, kwa nini tusiweke nguvu kwenye VETA ambazo mmezianzisha ili wale wanaoshindwa darasa la saba, wameshindwa kuendelea sekondari hawa iwe lazima kwenda kwenye hivi vyuo vya ufundi? Na kwamba wale watakaoshindwa kutoka form four Kwenda form five hawa ndio iwe lazima Kwenda kwenye vyuo vya ufundi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine tukumbuke, sio kila mtu lazima awe fundi bado tunahitaji wahasibu, tunahitaji watu wa manunuzi. Kuna watu watastaafu, kuna watu Mungu atawachukua, kuna watu wataacha kazi kwa hiyo haitafika siku kwamba hii nchi yote inahitaji mafundi tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado tunahitaji walimu , mainjinia, madaktari na watu wengine. Kwa hiyo mimi niliona, ni kwamba tunapofanya mapitio ya ule mtaala tuangalie kwamba sawa tunaweka masomo ambayo yatakuwa na ubunifu lakini tusisahau kwamba katika level ya sekondari si level inayomuandaaa mtu kuwa poroductive, hapana. Level ambayo inamuandaa mtu kuwa productive ni level ya Chuo Kikuu tu, na ndiyo maana tunataka wakitoka pale wa- accelerate Kwenda vyuoni tuimarishe vyuo vya VETA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu ni nini; kwanza mimi nashauri mtihani wa darsa la saba uendelee, uendelee kwa sababu tunahitaji kuwapima walimu uwajibikaji wao. Tukiondoa mtihani wa darasa la saba haitakuwa na maana ya kuwa na walimu shule za msingi, hawatawajibika. Hilo ni eneo la kwanza. Lakini la pili, kwa wale ambao hawatabahatika Kwenda kidato cha kwanza na kwa wale ambao hawatabahatika Kwenda kidato cha sita kutokea kidato cha nne, sasa hapa ile elimu ya ufundi ndipo iwe ya lazima. Kwa sababu hawa hawawezi Kwenda hata vyuo vingine vya kati hawa sasa tuwarudishe kwenye vyuo vya ufundi ambavyo tumevijenga, na iwe ya lazima huo ni ushauri wangu wa pili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine, niliwahi kuongea huko nyuma, na Waheshimiwa Wabunge wengi wamelaalmika hapa, kwamba kuna tatizo sana kwenye competences za walimu wetu. Lakini tatizo, Profesa, na umefundisha Chuo Kikuu cha Dar es salaam, ukifuatilia wanaoenda kusomea ualimu ni mtu aliyepata four, three ndio wanaoenda kusomea ualimu. Wale waliopata division one na two wanaenda kusoma kozi zingine, iweje wewe ulipata three umtengeneze mwenzako apate division one? Kwa nini tusibadilishe mfumo, kwamba wale waliofaulu zaidi kwa division one na two ndio watufundishie watoto wetu? Lakini wale tumewaacha wamekimbia wameenda kusoma wanakuja kufanya masomo ya business. Kwa hiyo ni eneo mimi nadhani mnahitaji kuliangalia kwenye sera yetu, kwamba vijana waliofaulu zaidi tuweke motisha ili waone ualimu ni mzuri, waweze kurudi kufundisha kule watutengenezee brains zingine huko katika nanii zetu. Lakini lingineā€¦

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Chaya.

MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo nakushukuru, naunga mkono hoja.