Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Spika, kwanza napongeza kazi nzuri ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ya uboreshaji miundombinu ya elimu na uboreshaji wa bajeti ya elimu. Nampongeza pia Waziri Mheshimiwa Profesa Mkenda, Naibu Waziri Mheshimiwa Kipanga, Katibu Mkuu Profesa Nombo na wataalam wote wa Wizara kwa jinsi wanavyoendelea kuipaisha sekta ya elimu hususan kwa kufanya maboresho ya sera ya elimu na mitaala.
Mheshimiwa Spika, ushauri wangu kwanza suala la elimu ya awali lizingatiwe na kujumuishwa kama ni elimu ya lazima kwani hapa ndipo sehemu muhimu ya kumjenga mtoto.
Pili, kuna tatizo kubwa la uhaba wa walimu katika nchi yetu lakini vibali vya ajira ni vichache. Nashauri Serikali yetu ifanye kila liwezekanalo idadi ya walimu iongezeke kwani zipo shule zina madarasa ambayo hayatumiki kutokana na uhaba wa walimu.
Mheshimiwa Spika, tatu, wakati elimu ya amali itakapoanza ni vyema Serikali ikatumia mfumo wa PPP ili kuweza kupata mazoezi ya vitendo kwa wanafunzi wetu kutoka sekta binafsi. Kwa mfano wanafunzi wataweza kwenda katika garage, hoteli, maduka, vituo vya ushonaji nguo, mashambani na kwingineko ili kujionea na kushiriki kufanya shughuli husika kwa vitendo.
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.