Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Hon. Emmanuel Peter Cherehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa fedha nyingi katika ujenzi wa barabara Ushetu hasa barabara ya Uyogo - Ulowa kilometa 30 ambayo ilikuwa ni kero kubwa sana kwa wananchi wa Ushetu na wakulima wa tumbaku sasa imetengenezwa na wananchi wamenituma kuja kumshukuru sana Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Spika, ombi la wananchi wa Ushetu ni ujenzi wa lami kwa barabara yao ya kilometa 54 kutoka Uyogo Nyandekwa hadi Nyandekwa hadi Kahama itengewe fedha ili ujenzi uanze, hii ni ahadi ya viongozi wetu wakuu wa nchi pia hata katika Ilani ya CCM imewekwa pia tunaomba kutengewa fedha kwa barabara ya Mwambomba inayopita Idahina - Nyakende - Ulewe - Ubagwe - Ulowa kilometa 224 na barabara ya Bugomba A - Butibu hadi Nyamilangano kilometa 47. Barabara hizi ni kiungo muhimu sana kwa wananchi wa Ushetu sasa zianze kutengenezwa na zitengewe fedha. Hali ya barabara hizo ni mbaya sana, kuna baadhi ya maeneo hazipitiki kabisa. Naomba Mheshimiwa Waziri barabara hizi zitengewe fedha.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.