Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi hii niwe mchangiaji jioni ya leo, kwenye hotuba muhimu sana ya bajeti hii ya maliasili na utalii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo amekuwa akiijali sana Wizara hii na namna ambavyo anapambana kukuza utalii, lakini upambanaji wake umejidhihirisha wazi kupambana na migogoro na sisi ni mashahidi anaendelea na ndio maana amemuweka waziri makini ambaye kila mtu aliyesimama hapa anaamini matumaini makubwa tunyao juu yako, juu ya utatuzi wa migogoro inayoendelea sehemu mbalimbali hapa nchini. Nikupongeze pia msaidizi wako Naibu Waziri pamoja na watendaji wote wa wizara kwa namna ambavyo mnafanya kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nina mambo mawili; la kwanza, nitaelezea jambo la muhimu sana la kiuchumi linaloendelea ndani ya bonde la Ziwa Rukwa. Mnamo mwaka 2019 Serikali kupitia Wizara ya Madini ilitoa kibali cha Kampuni ya Noble Helium kuja kufanya utafiti ndani ya bonde la Ziwa Rukwa. Bonde la Ziwa Rukwa linahusisha Mkoa wa Rukwa wenyewe, sehemu Katavi na Songwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa wamekuja na wameanza kazi yao tangia 2019, 2020, 2021 na 2022 na utafiti wanaoendelea nao umekuja na matumaini makubwa na sasa kwa utafiti tu wa awali inaonekana kwamba, Tanzania sasa ni nchi ya tatu duniani kwa deposit ya helium ambayo ni gesi adimu, ni critical material ambayo inatumika sehemu nyingi kama mnavyojua siwezi kutaja, kuna sehemu nyingi ambayo gesi ya helium ni muhimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni moja kati ya gesi ghali ambayo inauhitaji mkubwa duniani kwa hiyo sisi kama Tanzania kupitia bonde la Ziwa Rukwa, tumepata bahati kubwa ya kuwa na deposit kubwa na wanasema kwamba helium iliyo ndani ya bonde la Ziwa Rukwa ni green helium, ni pure kuliko yoyote ile inayopatikana duniani sehemu yoyote. Ukienda Marekani amabo wanaongoza na ukienda Qatar ambayo ni wa pili na sasa Tanzania tutakuwa wa tatu. Best helium inapatikana ndani ya bonde la Ziwa Rukwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa katika eneo walilopewa kufanya utafiti takribani kilomita za mraba 1467. Kilomita za mraba 167 ziko kwenye hifadhi na hifadhi hiyo ni ndani ya Ziwa Rukwa ambalo Ziwa Rukwa kwa ukubwa wake 80% inamilikiwa na Rukwa - Likwati na Uwanda Game Reserve, zote hizo zinamiliki maeneo haya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa walianza initiative ya kuomba kibali ili waruhusiwe Kwenda kufanya utafiti maeneo hayo, lakini mzunguko waliopewa zaidi ya miaka miwili, kunaenda nenda rudi. Waliambiwa mara ya kwanza wafanye environmental impact assessment, waka-engage hiyo process, wakatoa taarifa yao, wakapeleka taarifa NEMC. NEMC inka–certify kwamba hamna madhara yoyote na shughuli yenyewe inafanyika ndani ya mwezi mmoja. Baadaye walivyorudisha kwako huko TAWA wakasema hapana, nendeni tena Wizara ya Madini ndio watuandikie.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wameenda Wizara ya Madini basi kumekuwa na kurushiana mipira mingi. Sisi pale tunaenda kupata faida kubwa, tunaenda kuongeza pato la Taifa, tunaenda kupata kipato ambacho installation ikishakamlika tunaenda kuingiza dola milioni 100 kila mwaka, tunaenda kuongeza ajira na mambo mengi yanaambatana na uvumbuzi wa gesi hii ya helium. Sasa huyu mtu ame-invest zaidi ya dola za kimarekani milioni 30. Anapewa mizunguko hiyo na sasa hivi amekodi vifaa vikubwa ambavyo vinagharimu kila mwezi wanalipa zaidi ya dola za kimarekani milioni 100.5. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna vifaa vya airborne survey anavyo pale site kule Rukwa, lakini sababu tu ya kufanya maamuzi. Nakuamini ndugu yangu Mheshimiwa Mchengerwa kamalize jambo hilo wamalize utafiti suala la drilling litakuja baadaye. Tuta–discuss tuone je, kuendelea kuwa na reserve hizi au tuamue ku-drill tuingize mabilioni ya fedha, utakuwa uwamuzi wa Serikali hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niliongea na waziri wa madini Mheshimiwa Doto Biteko na wewe sasa nakuletea rasmi katika mchango wangu, angalieni mkae pamoja hawa watu wanaingia hasara kila mwezi kupoteza dola za kimarekani zaidi ya milioni moja kusubiria maamuzi ya Serikali ni kuwapa frustration wawekezaji wataona kwamba hatuko serious watanzania kwa jambo nyeti kama hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba niliseme kwa namna hiyo, naamini huyu ni msikivu ndani ya muda mfupi tutamaliza, hawa watu tutawa-sort waendelee na kazi yao ya utafiti na baadaye ripoti watatupa kama Serikali tufanye maamuzi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hilo nije na jambo la pili la muhimu ni migogoro inayoendelea na imesemwa na Waheshimiwa Wabunge wengi. Hapa nianze kwanza tena kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa namna alivyoridhia maeneo mengi ya hifadhi na kwangu mimi nilikuwa na mgogoro mkubwa sana pale Uwanda Game Reserve kwenye kata ya Kilangarani, Kata ya Kitete pale Kata ya Kapenta na Nankanga tayari maeneo yale yalirudishwa kwa wananchi. Kumebakia Kijiji kimoja ambacho tuna mgogoro Kijiji cha Nsanga ambapo mipaka haikueleweka kulikuwa na mvutano kati ya wanakijiji wa Nsanga na wale wataalamu mliotuma kwenda kuweka demarcation ya mipaka, hawajaelewana.
Mheshimiwa Mwenyekiti naomba hili ni jambo dogo tukali-sort hili suala la mipaka na migogoro ya mipaka tuimalize kwa style hii kwenye hifadhi ya Uwanda Game Reserve. Lakini baada ya pale sasa vioja ndio vilianza na hapa naamini kwamba askari wetu wa hifadhi wengi, wale wasiokuwa waadilifu walitamani migogoro ile iendelee kwa sababu wanaonekana ni beneficiary wa migogoro ile. Nasema hivyo kwa sababu nitaanza mwezi wa pili, jambo hili tumelimaliza Desemba Mwaka jana, mwezi wa pili tu fujo zikaanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mweneo yale ambayo Mawaziri walipita wakawapa wananchi, askari tabia zao wanaenda wanamvamia mwananchi wanaswaga ng’ombe wanaingiza kwenye hifadhi. Sasa mwananchi mmoja pale Nankanga anaitwa Nasuminzi ali-resist, alivyo–resist, askari wakaamua watumie nguvu kubwa wakamtandika risasi mguuni na baadaye nilitaarifiwa mwezi ule wa pili, nikawaambia nendeni polisi mkaripoti na ng’ombe wakawa wamenyang’anya. Baadaye iulivyofika ile issue kule polisi, tukaendelea na mazungumzo, baadaye busara ikatumika ikabidi wakae waelewane, yakaisha yule mwananchi akapewa ng’ombe, wakasema tutamsaidia matibabu, mpaka leo waliahidi watamtibu hawajafanya hivyo kwa masikitiko makubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wamempiga risasi kwa kuswaga ng’ombe wenyewe mle ndani na mimi nililetewa na tumeshirikishana na vyombo vyote vya usalama kuona namna ya ku–handle hii situation na sisi tumegeuka kuwa Wizara kwa namna fulani ku–suppress baadhi ya mambo ambayo tunaweza tukamaliza katika level zetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, haijaishia hapo kuna mzee mmoja alikuwa na baiskeli anatembea tu, wakamkuta wakasema bwana wewe unasenya kuni humu ndani wakamtandika viboko, wakamchana chana mgongoni nalo hilo tukataka tena kuli-solve wakampa tu shilingi 200,000 za kwenda kufanya matibabu. Nikadhani labda kwa mambo haya kwa sababu tuna-resolve haya mambo katika level ya chini tutayamaliza, naona wenzangu hawaelewi sisi ni wawakilishi wa wananchi na siwezi kukubali kuona mwananchi anaumia nikaka kimya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 26 Mei, kuna mambo mengine ya hovyo yametokea kule. Wameenda pale tena wanavizia hawa watoto wadogo wadogo, askari wanaenda na gari tena kutumia magari yetu ya Serikali, mafuta yetu, silaha zetu, wakaswaga ng’ombe kule ndani ya hifadhi. Walivyoswaga ng’ombe wakakamata wale ng’ombe wakasema sasa mtalipa. Wale wananchi nina orodha hapa na namba zao za simu nitakukabidhi Mheshimiwa Waziri ili tuanze na mambo haya yanayotuchafua na yanamchafua Mheshimiwa Rais. Wamelipa pale 26,920,000 na hizi hazina control number, wala hazina risiti. Watu wamechukua wameweka mfukoni na ndio maana nimesema kuna watu wanafurahia hii migogoro kwa sababu inawanufaisha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ndani ya tukio la doria moja tu mnaingiza 26,920,000 kuna utajiri wa namna hiyo? Doria moja ya usiku mmoja. Hawajaishia hapo! Risiti hawajatoa, wameenda wananchi sasa hivi wanavuna, wiki iliyopita nilitengeneza timu yangu kama Mbunge ofisi yangu, nikajihakikishia haya mambo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wameenda kule site wamekuta wananchi wameanzisha task force nyingine ya kuwanyang’anya mipunga, meeneo yale yale tuliyokubaliana walime. Walilima mwezi wa kumi na mbili na mimi ndiyo nilienda kuwatuliza wananchi kwamba limeni tu tayari na Mheshimiwa Rais kaweka sawa. Wamelima wanawaona, wamepalilia wamewaona, wameanza kuvuna wiki iliyopita wanataka mpunga tena wanachukua wanamnyang’anya mwananchi hapa mpunga, wanauza hapa anaona na hela wanatia mfukoni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mnadhani kutakuwa na amani Mheshimiwa Mchengerwa? naomba pale utume timu maana yake na sisi tunajipanga kama hamtachukua hatua tutajua namna yaku-deal na wale watu. Hatuwezi kukubali dhuluma, Serikali yetu hii haipendi dhuluma, wala hamkumtuma mtu akafanye dhuluma na nimekuwa nikiwa-engage mimi ni mtu mvumilivu sana na mstaarabu sana. Nimewa-engage taratibu twende tuelewane lakini naona hawa wenzangu hawanielewi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba tuma timu na uzuri watu wako menejimenti yako yote iko hapa. Ndani ya siku chache wawarudishie watu mpunga wao wote, nina majina hapa na wanajua na hizi hela hizi ambazo hazikukatiwa risiti 26,920,000 tujue zimeenda wapi? Nani amechukua? Na amechukua kwa sababu gani? La sivyo mzee! Nakuamini kabisa lakini nataka nisite baadaye jumatatu kushika shilingi, lakini naamini jambo hili weekend hii tutalimaliza likae salama. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo ninakushuluru na ninaunga mkono hoja. (Makofi)