Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

Hon. Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na namshukuru Mungu kwa kunifanya niweze kuzungumza hapa leo. Kipekee kabisa nawashukuru wanawake wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa kupendekeza nifike huku Bungeni kuwasemea, na nikishukuru Chama changu cha Mapinduzi kuruhusu jambo hilo likawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo ni mengi, muda ni mchache, lakini naomba kwa dhati kabisa nimpongeze sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea bajeti hii ambayo imekuwa ni bajeti yenye furaha katika Tanzania yote na kila mtu anasherekea. Mimi pia nimesimama kuipongeza bajeti hii pia kwa kuleta mapendekezo machache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Mheshimiwa Waziri na timu yake na wote ambao wamehusika kwenye hii bajeti na niunge mkono pendekezo kutoka katika Kamati yangu ya Bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sensa yetu ya mwaka 2022 imetufungua na kutuonesha mambo mengi wananchi wa Tanzania tuko milioni 62 na ushee. Na niseme kwamba bajeti hii iliyoletwa hapa mbele yetu imekuja ili sasa ipatiwe au trilioni 44 na ushee ziweze kupitishwa kwenda kutekeleza mengi. Mimi niseme rasmi kabisa kwamba naunga mkono tuweze kuipitisha kwa pamoja na kwa uzito mkubwa. Hii ni kwa sababu ametusomea Waziri wa Fedha; kwamba tunakwenda sasa kukuza uchumi, kuzalisha ajira na pia kupunguza umaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna maeneo mengi ambayo naweza kuyagusa lakini ningependa nizame kwenye eneo la kilimo, uvuvi na ufugaji. Niombe sasa twende kufanya kilimo chenye tija na uvuvi wenye tija pamoja na ufugaji wenye tija. Wenzetu Israel wanazalisha kwenye ekari moja tani 20, 000 za ndizi lakini sisi tunazalisha mikungu kadhaa inayohesabika. Sio hiyo tu lita 40 za maziwa kutoka kwenye ng’ombe mmoja sisi tunazalisha lita tatu zikizidi sana lita tano. Sasa tuna wasomi kutoka SUA na kwingineko; ni wapi tunapokosea? teknolojia haipo. Nimwombe sana Waziri wa Fedha aweze kusaidia anapotoa fedha hizi ziende nyingi kwenye research ili watu wengi waweze kwenda kujua nini kinafanyika na wenzao na research hizo zishuke sasa, zikasaidie wale wanawake wanaofuga na wale wote wanaofuga twende kwenye ufugaji wa tija. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ule ukurasa wa kitabu cha bajeti ule ukurasa wa 108. Kuna ile roman three, inaleta ukakasi kutoza ushuru wa bidhaa wa kiwango cha shilingi 20 kwa kila kilo moja ya saruji inayotoka nje ya nchi na inayozalishwa ndani ya nchi. Najiuliza hivi hii inayozalishwa ndani ya nchi wanaaminia kweli nasema hivyo kwa sababu gani? nyumba sio hitaji la luxury man slop kwenye hiyo rank of needs alisema food, shelter anda clothing. Sasa hii ni shelter hatutaki mwananchi wa Tanzania alale nje. Nilikuwa naomba hili pendekezo ni zuri kwa sababu saruji inachafua au pia siku nyingi sana hawajagusa, Serikali haijagusa ni kweli haijagusa lakini mbona kuna maeneo mengi ambayo tungeweza tukafidia jambo hilo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwarudishe nyuma mwaka jana tulisimama hapa tukasema magari ya Serikali yasingurumishwe wakati viongozi wameshuka, wamejirekebisha; sasa hivi magari ya Serikali yakisimama yanazimwa. Lakini kuna maeneo mengine hayo hayo kwenye Serikali yangeweza pia kuangaliwa. Kwa sababu gani? gari linakaa mpaka linachakaa hatuoni marekebisho mazuri. Je, vipuri vinavyowekwa ni vizuri? Yaani naomba Serikali nayo pia iangalie kwenye maeneo yanayowahusu. Wewe cost conscious kama wataweza kubana matumizi huko hakuna haja ya kumtoza maskini au mtu ambaye hana uwezo. Hizo fedha zote hizo shilingi 1,000 kwenye mfuko wa saruji mtu ambaye hajajenga nyumba. Kuna familia au kuna culture ambazo mtu hawezi kwenda kuzikwa kaburini bila kuingizwa kwenye nyumba yake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, bado kuna nyumba za mitembe ziko huku Dodoma kuna nyumba za full suit ziko Kilimanjaro. Hivi kweli mtu miaka yake 70 aliyopewa na Mungu aishi kwenye dunia kama hii kwenye utawala mzuri kama wa Dkt. Samia Suluhu Hassan bila kuwa na nyumba nzuri, nyumba nadhifu, nyumba ya matofali. Mimi naomba sana huu ujenzi wa nyumba uonekane ni hitaji na siyo luxury. Tupangishe kwingin,e kupo mahali pengi. Na niombe sana Serikali iangalie pia watu binafsi wanawezaje kubana matumizi na kwa nini wao washindwe. Naomba sana hilo ni ombi naomba kuwasilisha.

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja tena.