Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Hon. Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, ahsante nami niweze kuchangia kwenye Wizara hii ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Kwanza nianze kwa kushukuru kumekuwa na ufuatilio wa muda mrefu wa kutaka kulipwa fidia kwa wananchi wa Kata ya Nyamisangura kwa maana ya Mtaa wa Bugosi, lakini na wananchi wa Kata ya Nkende kwa maana ya Mtaa wa Kenyam kwa takribani zaidi ya miaka 13. Kwa hiyo, tunapenda kushukuru sana kwanza nianze kumshukuru aliyekuwa Waziri wa Fedha ambaye sasa hivi ni Makamu wa Rais, lakini aliyekuwa Waziri wa Ulinzi ambaye sasa hivi ni Rais wa Zanzibar na aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha kwa kweli Dkt. Ashatu Kijaji nimekuwa nikiwasumbua sana enzi hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini hatimaye pia niwashukuru mama yangu hapo Mama Tax Waziri wa Ulinzi, nimshukuru Katibu Mkuu Dkt. Faraji Mnyepe lakini pia nimshukuru Meneja wa Estate Kanali Kamuhambwa na Mhasibu wa Wizara kwa kweli Meja Ndombwe. Nimekuwa nikiwasumbua sana wamekuwa wakitoa ushirikiano wa kutosha lakini vilevile Wizara ya Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba pamoja na Katibu Mkuu Tutuba. Wananchi wanawashukuru sana kwa sababu wameweza kupokea kiasi cha shilingi 2,182,000,000 ambapo wananchi zaidi ya 211 wamepewa fidia. Lakini kuna wananchi sita ambao walifanyiwa tathmini, lakini zoezi la uhakiki lilipokuwa kupita pale hawakuwepo kwa bahati mbaya sana, kwa hiyo, wao hawakuweza kupata fidia yao kwa kipindi hiki, lakini tathmini walishafanyiwa. (Makofi)

Kwa hiyo, ningeomba Wizara iweze kupeleka jopo la kufanya uhakiki, ili waweze kuwahakiki wale wananchi sasa waweze kulipwa fidia yao, wananchi sita bado wamebaki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini vilevile kuna wananchi wawili ambao wenyewe hawakufanyiwa kabisa tathmini, walisema kwamba maeneo waliyopo yanakaribia mtoni kwa hiyo hawawezi kufanyiwa tathmini, lakini wananchi hawa ambao ni Samuel Mwita Maveiko pamoja na Marwa Mlimi walikuwa wemepanda miti pale na hiyo miti imefikia kuvunwa na kuweza kutengeneza mbao, lakini wamekataliwa wasivune miti ile na cha ajabu wanajeshi wenyewe wanavuna ile miti. Kwa hiyo, kama hawawalipi fidia basi wawaache wavune mazao yao waweze kuondoka kwenye lile eneo. Ningeomba sana Wizara muweze kuhakikisha kwamba mnawaruhusu wananchi hawa wanavuna yale mazao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia yale amaeneo ambayo tumewaachia sasa yako mjini na kuna barabara kama vile ilipo Lugalo pale, wananchi wa Kata ya Bumela, Mwema, Susuni, Nyandoto wanatumia ile barabara, lakini pia wananchi wanaotoka mjini kwenda kulima huko mashambani wanapita pale. Tungeomba sana waweze kupunguziwa zile adha ambazo wanakutananazo, waweze kufanya kama ambavyo wanafanya kwenye miji mingine ambayo unakuta kuna jeshi lakini barabara inapita katikati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na kwa kumalizia ni kuhusu kwa kweli, kuna malimbikizo makubwa sana kwa wanajeshi ya likizo hawajalipwa. Tunaomba takribani miaka 10 walipeni hawa wanajeshi haya malimbikizo ya likizo ili waweze kujikimu. Wengine mpaka wanafariki hawajalipwa haya malimbikizo yao ya likizo. (Makofi)