Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tumbatu
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. JUMA OTHMANI HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwako kwa kinipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba hii ya Makadirio na Mapato ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknnolojia ya Habari kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kutayarisha na hatimaye kuiwasilisha hotuba hii katika Bunge lako tukufu kwa ufasaha na umakini mkubwa. Hii ni miongoni mwa Wizara muhimu sana katika nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo; nikianza na usikivu hafifu katika baadhi ya maeneo nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Serikali yetu inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi zinazochukuliwa kwenye tasniya hii ya habari, hivi sasa ulimwengu uko kiganjani. Wananchi wote wanahitaji kupata habari ya kila kinachotokea nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, bado mpaka leo kuna maeneo katika nchi yetu hawapati habari. Bado usikivu wa habari katika maeneo yao si wa kuridhisha. Ushauri wangu katika jambo hili kwa Serikali ni kujitahidi kurekebisha hali hii ili wananchi wa maeneo husika wapate haki ya kujua matokeo yanayotokea katika nchi yao na ulimwenguni kwa ujumla.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa redio jamii, naipongeza Serikali yetu kwa kutoa uhuru wa habari. Uhuru huu umewasukuma wananchi katika maeneo kadhaa kufungua redio za kijamii. Redio hizi zinasaidia sana katika maeneo hayo. Lakini bado redio hizi uwezo wake ni mdogo sana, haukidhi matakwa ya redio hizo katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu katika jambo hili kwa Serikali ni kuiomba iweze kuweka mpango maalum wa kuzitambua na kuzisaidia redio hizi ili ziweze kukidhi malengo yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.