Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nina hoja zifuatazo; kwanza Mkoa wangu wa Iringa tuna wafugaji na wavuvi kwenye Bwawa la Mtera. Bajeti ya mwaka 2021/2022 Wizara iliahidi mikakati ifuatayo:-
(a) Kutengeneza vichanja vya kukaushia dagaa na Samaki;
(b) Wataongeza uzalishaji wa barafu na kujenga cold rooms. Hadi sasa wananchi wavuvi mkoani kwangu wanasubiri cold rooms kwa ajili ya kuhifadhia Samaki; na
(c) Mliahidi kununua boti za uvuvi, hatujapata bado.
Mheshimiwa Naibu Spika, mifugo mingi malisho yake ni changamoto kiasi kwamba mazao yake yanakuwa kidogo. Ushauri wangu:-
(a) Wizara ihimize uandaaji wa malisho ya mifugo. Tuelimishe wananchi kilimo cha majani kwa mifugo na tuwawezeshe wafugaji kuwa na malisho ya mfano.
(b) Wizara itafute soko kwa wavuvi na wafugaji wetu ili wavue na kufuga kisasa.
(c) Wizara itoe mafunzo, ihimize wananchi kuwa katika vikundi na kuwawezesha ufugaji wa mifugo na samaki pia mshirikiane na Halmashauri zetu katika mikoa yote ili kuinua wananchi na kuwaunganisha na taasisi za kifedha.
(d) Wizara itengeneze vichanja kwa ajili ya kukaushia Samaki.
(e) Wafugaji wakubwa kama ASAS Iringa azidi kupewa wataalamu ili aweze kufanya vizuri zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.