Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa na Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha uliuoishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Seriakli za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishi tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezajiwa wa Mitaji ya Umma kuhusu uwekezaji wa mitaji ya umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

Hon. Haji Amour Haji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makunduchi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa na Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha uliuoishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Seriakli za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishi tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezajiwa wa Mitaji ya Umma kuhusu uwekezaji wa mitaji ya umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

MHE. HAJI AMOUR HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ya kuweza kutoa yangu ambayo yapo katika uchambuzi wa Taarifa zetu ambazo tunazijadili leo kuanzia asubuhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja katika taarifa ambazo tulizonazo tuna taarifa ya Mahesabu ya Umma, Taarifa ya LAAC na kuna Taarifa ya PAC. Mimi nadhani kwamba nijielekeze zaidi kwenye taarifa inayohusiana na Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni Mjumbe ambae nipo katika Kamati ile ambayo moja kabla ya yote hayo nipende kumshukuru Mheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuyajali mashirika yetu haya na kuweza kukaa nayo kwa pamoja kutafuta namna ya ufanisi na tija ya mashirika yetu alikaa nayo katika kikao kimoja pale Arusha, ambapo pale kulikuwa na mazungumzo mengi na kuweza kuyajenga yale mashirika kama ni semina.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja katika shughuli ambayo tunaifanya katika Kamati ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma ni kwamba kuangalia ufanisi wa mashirika yetu ya umma pamoja na tija yake. Tunavyojua kwamba moja katika vitu viwili hivi lazima kwamba vinakuwa vinaendana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye ufanisi au kukosekana kwa ufanisi maana yake kutakuwa kutakosekana kwa tija katika mashirika yetu. Katika taarifa zetu tulizozipitia katika mashirika yetu ya umma tumejaribu kuangalia mashirika mengi sana kwa sababu kwenye Kamati yetu ya Mitaji ya Umma tuna mashirika karibu 287 ambayo ndiyo tunatakiwa kuyajadili na kuyajengea hoja katika ufanisi na tija katika mashirika hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja kati ya mambo ambayo yalikuwemo katika mashirika yetu tumejaribu kuangalia tija pamoja na ufanisi wa mashirika yale, katika mashirika na tija ambayo ipo katika mashirika yetu yamejigawa katika makundi matatu. Kuna kundi la mashirika ya umma ambayo yanatoa gawio na kwa mujibu wa sheria, kuna makundi na kundi la mashirika ya umma ambayo yanatoa asilimia 15 na kuna kundi la mashirika ambayo yanatoa ziada na kuna kundi la mashirika ya umma yanatoa kwa mujibu wa vile ambavyo wanajihisi namna ya kutoa katika Serikali, ndicho ambacho tulikibaini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukilinganisha mlingano wa takwimu ya mwaka jana na mwaka huu wa fedha maana yake ukitizama katika mashirika yenye kutoa gawio kuna mashirika 66. Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wangu wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji wa Umma, alitaja mashirika 66 ambayo kati ya mashirika 66, mashirika 25 tu ndiyo yaliyotoa gawio. Hiki ni kitu ambacho ukiangalia upande mwingine ukiangalia kwamba, ule ufanisi na ile azma ya kuweza kuyajenga yale mashirika yetu maana yake maana yake hayajafikiwa katika hali nzuri. Pamoja na kwamba mashirika 25 ndiyo yaliyotoa gawio na kupata shilingi 37,528.000.000 na kuendelea bado ukiangalia mashirika yote 66 yenye kutoa gawio maana yake hapo tungekuwa tuna fedha nyingi sana katika ukusanyaji wa mapato yetu. Kimsingi nitasema kwamba kazi bado tunayo ya kuweza kuifanya, maana yake hili ambalo tutasema kwamba mashirika 25 waliotoa na ukilinganisha mwaka jana maana yake mashirika haya kidogo tumejitutumua kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa mashirika yale yanayotoa asilimia 15 kwa kiasi fulani nayo si haba maana yake kwa sasa hivi yametoa karibu asilimia 70. Lakini kuna tatizo ambalo ni la kiutendaji na kiufanisi katika haya mashirika yetu, kwanza tulichokigundua katika mashirika yetu kuna kitu ambacho kimekuwa kinagomba kwa mashirika yetu. Kwanza hawaangalii namna ambavyo zile K.P.I zilizowekwa na Msajili wa Hazina hawazizingatii ipasavyo, kwa sababu utakuta kwa mfano kama taasisi ya maji kwamba kigezo walichowekewa kwa mfano kama upungufu wa maji maana yake usizidi au katika umwagikaji wa maji maana yake usizidi asilimia 25. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utakuta kwamba katika K.P.I zao maana yake wapo zaidi ya hapo. Kuna baadhi ya mashirika mengine maana yake hata ule utendaji wao unaonekana dhahiri kwamba hauko vizuri na kwa sababu kuna baadhi ya mashirika tumeyakuta katika hata ule mpango mkakati wao hauko vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tumelikuta hata shirika, kuna baadhi ya mashirika ambayo tumekuwa nayo tumelikuta hata ule mpango mkakati hakuna. Sasa katika kupima zile K. P.I maana yake utakuta shirika lile hujui hata ulipime namna gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niweze kumpongeza Msajili wa Hazina kwa jitihada zake kubwa ambazo anazozichukua katika namna ya kuweza kutafuta mwarobaini wa kuyafanya mashirika yetu yawe ya kibiashara, kwa sababu pamoja na yote hayo maana yake kuna mashirika ambayo wakati mwingine yanapatiwa ruzuku, lakini ile ruzuku wanayopatiwa maana yake hakuna tija yoyote inayorudi katika Serikali. Kuna mashirika yale ya kibiashara moja kwa moja maana yake yanafanya biashara zaidi ya zile ruzuku wanazopewa na Serikali yake hakuna kitu chochote. Ufanisi pale unakuwa unakosa na tija inakuwa haipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumegundua kwamba kuna baadhi ya mashirika hata wale Watendaji wake wa Bodi ukiwapima hawawezi kupimika. Mimi ninaiomba Serikali pamoja na yote hayo lakini kuna haja kubwa sana ya Msajili wa Hazina kuweza kukamilisha mchakato wake wa sheria ili waweze kuja hapa Bungeni lengo kubwa ni kuweza kuwahakikishia kwamba mashirika yetu ya umma yanafanya vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na yote hayo nasema kwamba nampongeza sana TR kwa kazi yake kubwa anayoifanya, nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kuweza kuyajali mashirika yetu na kwa namna ambavyo anavyokusudia kuyafanya kwamba yaweze kuleta ufanisi na tija. Natumai kwamba mabadiliko yoyote yatakayokuja ya sheria yatakayotoka kwa Msajili wa Hazina yatakuwa ni mabadiliko yenye kuleta tija na ufanisi kwa mashirika yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo naunga mkono hoja taarifa za Kamati zetu zote tatu ambazo zimewasilisha taarifa zao hapa, Ahsante sana. (Makofi)