Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais wetu kwa kazi kubwa ambayo ameifanya kwenye eneo la afya. Nikushuru wewe, lakini nimshukuru Waziri wetu Mheshimiwa Ummy Mwalimu na kugongea aliyosema Mheshimiwa Musukuma kwamba kwa kweli amekuwa ni mtu ambaye anathubutu kufanya yale magumu ambayo hayawezekani lakini yamefanyika, na watumishi wote wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Katibu Mkuu.
Mheshimiwa Spika, mimi ninashukuru Bunge lako tukufu, ahsanteni sana kwa sapoti mliyotupa lakini asanteni sana kwa mawazo mazuri ambayo mmetupa leo. Mimi niwahakikishie chini ya dada yangu Mheshimiwa Ummy Mwalimu kiongozi wetu. Mimi ninataka kuwaambia kila mlilolisema litakuwa accommodated. Niwatoe wasiwasi, leo mmeona jinsi ambavyo Mheshimiwa Rais wetu amewekeza kwenye miundombinu. Mmeona tukiwa Mtwara, tukiwa Lindi lakini leo hapa mna ushahidi kwamba vimejegwa vituo 3,181 kwa miaka miwili, sio kidogo sana.
Mheshimiwa Spika, ukiangalia kwa muda mfupi sana, emergence depertment zimejegwa 111, zimejengwa sehemu za watoto njiti 123; na leo tunapozungumza hapa kwenye eneo muhimu sana la wakina mama tumetoka kwenye vifo vya wakina mama 530 kati ya wakina mama 100,000 mpaka leo kwa muda mfupi sana tumefika vifo 104 chini ya 100,000 ni hatua kubwa sana na ni uwekezaji uliowekezwa kwenye miundombinu, teknolojia pamoja na uliwekezwa kwenye taaluma ya wataalamu wetu.
Mheshimiwa Spika, ukisikia kwenye taaluma ya wataalam wetu, kila mwaka shilingi 9,000,000,000 zinaenda kwa ajili ya kuboresha taaluma. Ukiona sasa hivi tumeambiwa teknolojia zote ambazo zimewekwa na Mheshimiwa Rais wetu kwenye eneo la afya, suala ni moja, teknolojia imewekezwa; leo Mheshimiwa Rais wetu ametufikisha mahali, sehemu ambayo Muhimbili walikuwa wanakufungua kifua chote ili waweze kukutibu moyo, sasa hivi wanakutoboa sentimita mbili mpaka sentimita nne unatibiwa unarudi nyumbani. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, suala ni kwamba ili utibiwe, Mtanzania apate hiyo huduma, je, ni Watanzania wangapi wataweza kulipia na wao waweze kutibiwa kwa hiyo teknolojia ambayo Mheshimiwa Rais wetu ameiweka.
Waheshimiwa Wabunge, ahsanteni sana leo mmeenda kupitisha na mnaenda kutoa njia ambayo itamfanya kila Mtanzania kwenye hizi teknolojia na miundombinu mizuri ambayo Rais wetu ameenda kuwekeza, Watanzania wote wataenda kupata hiyo huduma. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninachoweza kuwaambia Wabunge wenzangu, ahsanteni sana, ahsanteni sana. Nataka kuwaondoa wasiwasi Waheshimiwa Wabunge wenzangu kwenye maeneo wanayayaona kwamba hatujafika. Ni lini wameweza kuona Mheshimiwa Rais anagawa magari 989 kwa wakati mmoja kwa ajili ya kuja kwenye majimbo yao. Kama haya yamewezekana, hayo mengine ni madogo sana.
Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kuwaambia, mimi na wenzangu tumefuatilia kwa mwaka, exemption zinazofanyika ni bilioni 667, lakini ukifuatilia wengi waliofanyiwa exemption siyo kwamba hawana uwezo. Ila hawana uwezo wa kulipa kwa mara moja hizo fedha. Maana yake leo tukienda kwenye bima ya afya kwa wote wataweza kulipa bima yao. Hizi bilioni 667 zinazotumika kuwatibu Watanzania bure kwa sasa ambazo Serikali inazitoa, zitarudi kwa ajili ya kujenga vituo vya afya na zahanati kwenye maeneo yetu ambayo hakuna zahanati. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, leo tumeona teknolojia kubwa sana ambayo amewekeza Rais wetu. Kule kwenye maeneo yetu tunaambiwa kuna x-ray 199, tunaambiwa kuna ambulance 989, tunaambiwa kuna CT scan, kuna MRI na vitu vingine. Maana yake fedha zinazokuja kupatikana kwenye Mfuko wetu wa Bima ya Afya, maana yake wataalam kule watahakikisha hatutarudi tena hapa Bungeni kupitisha fedha kwa ajili ya kununua CT scan na x-ray. Hii ita-generate fedha na itarudi kwenye eneo hilo na vifaa hivyo vitahudumiwa vizuri na wakati mwingine vikihitajika vingine vitanunuliwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hapa maana yake ni kwamba, tutapata fedha ya kuwekeza kwenye maeneo mengine ya kiuchumi strategic na kuongeza fedha kwenye Mfuko wetu na kumaliza matatizo mengine yaliyoko kwenye mfumo wetu. Ninachokisema ni kwamba, tukipitisha Mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote, nataka kuwaambia hata fedha zinazotoka direct kutoka kwenye Bajeti ya Serikali kuelekea kwenye kutibu watu kwenye mahospitali na kwenye Wizara ya Afya zitapungua na fedha hizo zitaelekezwa kwenye miundombinu na vitu vingine ambavyo Waheshimiwa Wabunge wamesema hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kaka yangu Mheshimiwa Shigongo amezungumzia hapa suala la preventive medicine. Yote ambayo kaka yangu Mheshimiwa Shigongo amesema kwetu sisi tunayachukua, tunayapigia mstari kwa sababu tukitaka kweli kulinda Mfuko wetu wa Bima ya Afya na kupunguza matumizi kwenye eneo hili, ni lazima twende kwenye mwelekeo huo.
Mheshimiwa Spika, nataka pia kuelezea ambacho amekizungumza Mzee wangu Mheshimiwa Sanga, amesema vizuri sana mzee wa mabilioni na mabilioni, lakini nataka nimwambie siyo mabilioni na mabilioni tena. Ni matrilioni na matrilioni. Tumeshatoka kwenye mabilioni na mabilioni, sasa hivi ni matrilioni na matrilioni. Mapinduzi wanayoyaona kwenye afya leo yamefanywa na Rais wetu kwa kutumia trilioni 6.7. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, niwashukuru Waheshimiwa Wabunge na nataka kuwaambia chini ya Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na uongozi wa Mheshimiwa Ummy Mwalimu, sisi Sekta ya Afya yote mnayoyasema yanaenda kutekelezeka, ahsanteni sana. (Makofi)