Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa hotuba yake ya bajeti iliyojaa mambo muhimu ambayo yanaleta matumaini kwa Watanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niipongeze Serikali kwa kutoa takribani shilingi bilioni 12 kulipa fidia kwa watu binafsi na taasisi zinazozunguka maeneo ya Bunge, wazo hili ni muhimu sana kwani linaenda kupunguza kero kwa Waheshimiwa Wabunge ya kukosa ofisi za kutendea kazi. Aidha, utwaaji huu wa maeneo utasaidia vyombo vyao vya usalama kuwa mahali salama. Ili zoezi liwe na tija nashauri zile taasisi za Serikali ambazo bado hazijaondoka zitafutiwe maeneo mbadala haraka.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri ni vema kwa Serikali kutafuta eneo kubwa zaidi nje au mbali tukiamini idadi ya Watanzania inaongezeka na Waheshimiwa Wabunge watakuja kuongezeka.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.