Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Joseph Zacharius Kamonga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ludewa

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Ludewa lina wananchi wenye moyo wa kujitolea sana kwenye maendeleo hivyo wanaiomba sana Serikali iwaunge mkono katika kumalizia maboma ya vituo vya afya. Kata zilizojenga na kuezeka jengo la utawala ni Lugarawa, Ludewa, Luana, Madilu, Lupanga, Ludende, Madope, Lumbila, Mkongobaki, Lupingu, Kilondo na Masasi. Naomba sana Serikali isiwavunje moyo wananchi hawa kwa kuja na mpango wa kuvimalizia japo kwa awamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishukuru sana Serikali kwa kutoa shilingi bilioni 2.6 kwa ajili ya Barabara za Tarafa ya Mwambao kwani Kata nne za Kilondo, Lumbila, Makonde na Lifuma hazikuwahi kuunganishwa kwa barabara, naomba fedha ziongezwe kwenye Barabara za Ludewa - Nsisi; Mbwila - Lifuma; Lumbila - Kijyombo; Mawengi – Kitewele – Kimata - Makonde; na Madunda – Liunji – Ifungu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imetoa fedha nyingi kwenye Barabara ya Itoni – Ludewa - Manda pamoja na shukrani nyingi, tunaomba Lot III inayoanzia Mawengi hadi Makao Makuu ya Wilaya ya Ludewa imaliziwe kujengwa kwa kiwango cha zege ikiwezekana hadi Nkomang'ombe ili kuweza kusafirisha makaa ya mawe mengi na kuongeza mapato ya nchi na wananchi.