Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023

Hon. Ussi Salum Pondeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chumbuni

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023

MHE. USSI SALUM PONDEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi leo hii kuwa miongoni mwa wale ambao wanachangia katika hizi ofisi zetu zote nne ambazo Wizara zimewasilisha. Nichukue nafasi hii pia kuwapongeza Wenyeviti wote wa Kamati hizi ambazo wamewasilisha Wizara zao, lakini leo nina mchango mdogo tu ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niwakumbushe au niwahimize waendelee kuweka msisitizo kwa Mabalozi wetu wa nje na taasisi za Kimataifa ambazo zipo nchini ambazo bado hazijafungua ofisi zao ndogo katika sehemu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kule Zanzibar. Jambo hili ambalo hata Ilani ya Chama chetu cha Mapinduzi imezitaka pia Balozi hizi kuhakikisha zinafungua ofisi ndogo na taasisi hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama haitoshi katika Wizara hii ya Mambo ya nje kuna mambo ambayo nilikuwa nataka niwashauri zile Balozi zetu za nje ambazo nyingi zina viwanja vikubwa lakini bado hazijajengwa, ningependa zijengwe zile ofisi ambazo zina hadhi ya Tanzania kama ilivyo na hadhi hivi sasa. Tusiwe na viwanja vyetu lakini tukajega nyumba ili mradi ofisi lakini tujenge ofisi ambazo zina hadhi kama Tanzania ilivyo na hadhi kwa wakati huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ningewapongeza Wizara ya Mambo ya Nje katika moja ya jambo ambalo wamelifanya zuri lakini hawajamaliza na inshaallah watamaliza ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Nairobi, kitu kama kile vikiwepo 12 ndani ya dunia hii basi watu wote wataweza kujua Tanzania ikoje na ina thamani kiasi gani. Niwapongeze sana Wizara ya Mambo ya Nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanja hivi vyote vikiweza kujengwa majengo ambayo yana hadhi ya Kimataifa, kuna mchangiaji mmoja amepita amesema tujielekeze vilevile katika uwekezaji wa utalii wa mikutano. Tunao uwezo wa kujenga majengo yetu katika Balozi zetu tukaweza kutumia yale majengo sasa tukawa na conference mle ambazo zitatumika kwa kukodishwa lakini hata kwa uwekezaji ambao vilevile utaendelea kuleta matunda ambayo yatainufaisha nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa machache ambayo umenipa nafasi hii napenda nichuke nafasi nimpongeze Mama Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi kwa jinsi ambavyo wameweza kuitangaza Royal Tour ambapo mimi kama mmoja wa wanufaika kule kwetu Zanzibar, hivi sasa kutokanana ile tour ambayo imeweza kuitangaza Tanzania ilivyo, Zanzibar sasa hivi ndiyo jambo letu kubwa ambalo tunalitegemea la utalii lakini Zanzibar sasa hivi tumekuwa hatuna msimu, kwa siku zinashuka ndege nyingi za Kimataifa na hela nyingi za kigeni zinaingia ndani ya nchi yetu, kwa hiyo napenda nishukue nafasi hii niwapongeze na ikiwezekana basi tuangalie sisi kama Bunge lakini na wajumbe wegine ikitupendeza tumshawishi mama kwa uzuri wake na alivyo na taswira yake, kwa nini tusiweke picha yake katika noti ya Tanzania, ikitupendeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja zote nne ambazo zimewekwa lakini pia nakupongeza kwa kunipa nafasi, ahsante sana.