Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Shabani Omari Shekilindi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lushoto

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, kipekee nimpongeze Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatumikia Watanzania.

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Lushoto lina vitongoji vyenye idadi kubwa ya watu na wingi wa nyumba, yaani kitongoji kimoja cha Lushoto ni sawa sawa na vijiji viwili vya maeneo ya mabondeni. Kwa hiyo, tunaomba vitongoji vyetu vihesabiwa kama vijiji kutokana na ukubwa wa vitongoji vyenyewe na wananchi wa Lushoto wanajua umuhimu wa umeme, na ndiyo maana imekuwa ni changamoto kubwa sana kwa Wabunge wa Lushoto.

Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa maelezo mafupi, naomba vitongoji vifuatavyo viweze kupatiwa umeme kwa maana imekuwa ni kero kubwa; kwa Kata ya Gare ni Vitongoji vya Gare Kaya, Zeta, Kwetango, Kwemdee na Kumbamtoni, Kwemabanda. Aidha kwa Kata ya Kwemashai ni Kwemulua na Golani na Kwemagemo.

Mheshimiwa Spika, katika Kata ya Ubiri ni Mziwaishi na Misheni pamoja na Kibago. Aidha katika Kata ya Kilole ni Ula, Kilole Kaya na Kwebarabara.

Katika Kata ya Kwekanga ni Kwemishai, Kwemkashi, Bombo Juu na Kweboma; na katika Kata ya Mlola ni Muheza, Migambo, Mtae na Hondelo A na B na Maweni.

Mheshimiwa Spika, katika Kata ya Malibwi ni Kwawambugu, Zahanati na Kwawambugu B; Ngaloi, Mzizima, Mpalai na Ngaloi A; Ngindoi Ofisini, Mlesa na Mavovo. Aidha, katika Kata ya Kwai ni katika Vitongoji vya Kimunyu, Kwemagemo na Kahalawe; na katika Kata ya Migambo ni katika Vitongoji vya Malunga, Milungui juu, Kwebalasa na Mhande.

Mheshimiwa Spika, katika Kata ya Makanya ni katika Vitongoji vya Kwemshazi Mboghoi na Mbokoi; Kaghambe Kizelui na Lunguza na vitongoji vyake. Aidha katika Kata ya Mbwei ni Kwasemaghera, Pongwe, Kidandi na Kweganga, hivyo ni baadhi tu ya vitongoji katika Jimbo la Lushoto, kati ya vingi vilivyobaki.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo gharama ya gesi ipunguzwe ili wananchi wetu waishio vijijini waweze kumudu kununua gesi.

Mheshimiwa Spika, naunga hoja mkono kwa asilimia mia moja.