Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kusini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
2
Ministries
nil
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi ya kuchangia hoja ya Mheshimiwa Jacob Tarimo kuhusiana na hoja iliyopo mezani ya halmashauri zetu hasa za miji, majiji na manispaa kuingia MoU na Jeshi la Zimamoto kwa lengo la kushirikiana katika utatuzi wa majanga pamoja na mioto ambayo mara kwa mara imekuwa ikitokea katika miji yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika…
SPIKA: Mheshimiwa Kassinge, moto hauna wingi… (Kicheko)
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Spika, naomba nirekebishe kwamba MoU ambayo itaingiwa na miji yetu, manispaa na majiji kwa upande mmoja na Jeshi la Zimamoto kwa upande mwingine kwa lengo sasa la kushirikiana katika kutatua majanga pamoja na moto ambao umekuwa ukitokea mara kwa mara. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nianze tu kwa kuunga mkono hoja hii na naunga mkono hoja hii nikiweka msisitizo kwamba moto na majanga ni sehemu ya vitishio vya usalama katika maeneo yetu, lakini jukumu la ulinzi na usalama Kikatiba, Mamlaka zetu za Serikali za Mitaa zimepewa jukumu hilo la ulinzi na usalama na kwa maana hiyo Mamlaka zetu za Serikali za Mitaa ikiwemo miji, majiji na manispaa kwa namna yoyote ile iwayo huwezi ukazitenganisha na jukumu la msingi la ulinzi na usalama wa watu katika maeneo yao. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini jambo la pili ni kwamba Jeshi letu la Zimamoto limekuwa likipata changamoto ya miundombinu isiyoridhisha pale ambapo majanga ya moto yamekuwa yakitokea, lakini jukumu la upangaji miji kisheria ni jukumu la miji yetu, manispaa zetu na majiji yetu na kwa maana hiyo huwezi ukazitenganisha Mamlaka za Serikali za Mitaa na Jeshi la Zimamoto katika maeneo ya kupanga miji. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, miongoni mwa changamoto ambazo zimebainishwa na baadhi ya wachangiaji ni upungufu au kutokuwepo kwa kabisa kwa fire hydrants katika miji yetu, lakini ni nani atakayeainisha maeneo haya ya fire hydrants? Ni jukumu la pamoja sasa kati ya halmashauri zetu pamoja na Jeshi la Zimamoto kutenga maeneo ya fire hydrants ili Jeshi la Zimamoto liweze kupata wepesi pale majanga yanapotokea. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nikubaliane na baadhi ya wachangiaji kwamba halmashauri zetu hazifanani kimapato, lakini niweke wazi hapa kwamba MoU ambayo itaingiwa haitailazimisha kila halmashauri zichukue hili jukumu la kusaidiana Jeshi la Zimamoto, itategemea uwezo wa halmashauri husika, lakini pia itategemea halmashauri inadhani ishirikiane na Jeshi la Zimamtoto katika eneo la hili. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mwisho niseme kwamba kumekuwa na misconception kidogo kuhusiana na mapato ya halmashauri ikidhaniwa kwamba bajeti za halmashauri zinakusudiwa zile tu ambazo ni kwa ajili ya mapato ya ndani persée, hapana. Halmashauri ambazo zitaingia MoU na jeshi hili kwa kununua vifaa au magari zitakuwa na avenues mbalimbali za kutafuta vyanzo vya mapato ikiwemo grants kutoka kwa wahisani mbalimbali na kwa maana hiyo tusipate hofu ya kudhani kwamba halmashauri tutakuja kuzibebesha mzigo kwa kusaidiana na Jeshi la Zimamoto. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mwisho naomba kuunga mkono hoja hii. (Makofi)