Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hoja kuhusu Halmashauri za Miji na Wilaya Kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kutatua Tatizo la Upungufu wa Magari ya Zimamoto pamoja na Vifaa Vinavyotumika Kuzima Moto na Uokoaji

Hon. Tarimba Gulam Abbas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kinondoni

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hoja kuhusu Halmashauri za Miji na Wilaya Kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kutatua Tatizo la Upungufu wa Magari ya Zimamoto pamoja na Vifaa Vinavyotumika Kuzima Moto na Uokoaji

MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi kuchangia hoja hii muhimu.

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nimpongeze Mheshimiwa Tarimo kwa kufanya kazi ya kubuni kuleta hoja hii, ahsante kwa kufanya kazi ya Kibunge na hiyo ndio kazi ya Kibunge.

Mheshimiwa Spika, vilevile nimpongeze Mheshimiwa Kassinge umenifilisi, lakini mimi nina nyama zaidi ya hizo ambazo umezitumia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, huwezi ukaiepuka halmashauri yoyote ile ya mji kwa sababu halmashauri ni planning authority kwa mujibu wa sheria. Wao ndio wanaopanga mji, barabara na njia za maji. Wao wanaweka hata maeneo fire hydrants inapotakiwa iwe, unaiepuka vipi halmashauri? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, si lazima halmashauri itoe fedha, kinachohitajika hapa ni kuhusishwa kwa halmashauri katika taratibu nzima za upangaji wa miji. Najua Mheshimiwa Rais ametupatia magari mengi sana ya zimamoto, hata Dar es Salaam ametupatia, lakini hebu iangalie ilivyo, kwa mfano mzuri nawapatia mifano mitatu tu. Magomeni Mapipa pametokea moto ambapo siyo mbali hata kilometa moja na kilipo Kituo Zimamoto, bado hawakuweza kutusaidia, nyumba ziliungua zote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukienda kule Soko la Mchikichini hali kadhalika hawako mbali na Kituo cha Zimamoto. Ukaenda Soko la Kariakoo hawako mbali na vituo vya zimamoto. Pia Dar es Salaam barabara zipo finyu, msongamano wa magari ni mkubwa, lakini hata magari ya zimamoto yakifika katika eneo la ajari fire hydrants hazifanyi kazi. Wanafanyaje kazi ya kuweza kusaidia kuzima moto?

Mheshimiwa Spika, niwape takwimu tarahe 15 Mei nilivyokuwa nachangia kwenye bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani nilizungumzia masula ya zimamoto peke yake na katika mambo yale niliwakumbusha utafiti uliofanywa mwaka 2013 kwamba utafiti ule unaonesha fire hydrants katika Jiji la Dar es Salaam zilikuwa 2,600 na 1,268 hazifanyi kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, zilizokuwa zikifanya kazi mwala 2013 ni 74 tu, sasa hivi zinazofanya kazi ni 108. Taratibu za uwekaji wa fire hydrants ni futi 500 na zisizidi futi 800, hizo hazipo.

Mheshimiwa Spika, sasa hata kama ukiwa na magari ya kutosha, gari zikienda pale zikazima moto na wanapozima moto maji yamemalizika inabidi waondoke wakatafute maji, yaani unataka kuniambia moto umekaa pale unawasubiri fire waje pale walete maji? Hapana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana fire wakimaliza kuzima, wamezima moto tu, lakini uokoaji haupo. Mali zinateketea, hivyo ili kuweza kuisaidia fire mimi naunga mkono hoja nzima ya Mheshimiwa Tarimo kwa sababu kama nilivyosema planning authorities lazima zihusike, watu wa maji lazima wahusike, fire hydrants ni kitu muhimu sana na umuhimu wake ni kwamba hata maji yanapokuwa na pressure ukifunga lile bomba la kuzimia moto hata gari huhitaji. Wakati mwingine maji yale yanaweza kutumika kuweza kuzimia moto. Kwa hali hiyo mimi nimelitaja tu hilo eneo la fire hydrants, lakini ni dhahiri kabisa hoja hii ni muhimu na Serikali iichukue, ifanyie kazi ili kuweza kuokoa watu wetu, miji na mali zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na naunga mkono hoja, ahsante. (Makofi)