Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Edward Olelekaita Kisau

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiteto

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi. Kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa afya njema na leo tuko hapa salama, lakini pili nimpongeze Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nyingi alizofanya na ameonyesha nia njema sana kwa kuunda ile Tume ya Haki Jinai. Vilevile Mheshimiwa Dkt. Samia ameleta sheria nyingi hapa tuzibadilishe ili ziweze kuwa na manufaa kwa Watanzania walio wengi. Vilevile nimpongeze Waziri wa Sheria na Katiba, Mheshimiwa Dkt. Balozi Pindi Chana kwa kazi nzuri ambayo anafanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Naibu Waziri kwa kuteuliwa, yeye ni mtu humble sana. Kuna siku nimepiga simu saa nane ya usiku nikiwa airport na akapokea. Aendelee hivyo hivyo. Nimpongeze Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mheshimiwa Jaji Dkt. Feleshi, very humble na Mheshimiwa Jaji I still enjoy ile time I appeared before you. Kwa kweli wewe ni mtu mwema sana sana na I still think nchi yetu imempata Attorney General mzuri sana, very humble. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Katibu Mkuu wa Wizara hii. Hii Wizara ina watu wema sana, nadhani kwa Makatibu Wakuu ninaowafahamu I think Dkt. Mary Makondo ni very humble. Sijui dini yake, lakini nikimwangalia ni kama ameokoka hivi, ni mpole sana. Vilevile DPP, DPP ni mpole sana, very nice, very nice team.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kama walivyosema Kamati, tunaomba Serikali iendelee kutenga fedha nyingi sana ili iiwezeshe Wizara ya Katiba na Sheria kuendelea kuwahudumia Watanzania. Tumesema kila wakati kwamba utawala bora na sheria ndiyo nguzo yake, ndio msingi wa mambo yote. Kwa hivyo tukiwawezesha wataweza kutimiza jukumu lao vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Mheshimiwa Ole Gabriel na Jaji Mkuu kwa kusimamia miradi ya Mahakama vizuri sana. Nchi yetu na nasema kama Wakili kwa mara ya kwanza na I feel very jealousy nikiona Mahakama zetu zilivyo nzuri sana; ina misingi mizuri sana na miundombinu ni mizuri sana. Ukitembelea hizi Mahakama ambazo ni integrated justice system utafikiri ni hoteli fulani hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachowaomba tu sasa ni kwamba Watanzania walio wengi wanahitaji huduma hizi za Mahakama. Kwa hivyo kama walivyokuja kwenye Kamati na kuleta plan ya kwenda kila wilaya na tarafa, plan hiyo iendelee.

Mheshimiwa Mwenyekiti mwaka jana na mwaka juzi walizungumza hapa na walisema Kiteto watajenga mahakama ya wilaya kwa bajeti ya 2024/2025. Kwa hivyo nimekuja kusema kwamba hii ndiyo 2024/2025, Kiteto na maeneo mengine ambayo hayana Mahakama tunataka Mahakama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, kwamba utawala wa sheria ndio msingi wa kila kitu nchini. Ripoti ya Kamati ya mwezi Februari tulizungumza na nanukuu ukurasa wa 51: “Kuhakikisha kwamba inatekeleza maamuzi yote ya Mahakama ili kulinda haki za raia ikiwemo kurejesha mali zilizotaifishwa iwapo mtuhumiwa ameshinda kesi na hatua zote za rufaa zimekamilika”. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulisema pia kuhusu Ofisi ya DPP kushirikiana na taasisi zingine za upelelezi, ukamataji na utaifishwaji ili mali za watuhumiwa waweze kurudishiwa baada ya kushinda kesi zao. Mimi hapa nimezungumza mara kadhaa kuhusu kesi ya wananchi wangu wa Kiteto. Kesi yao ya mwisho ilikuwa ni kesi ya Mahakama ya Rufani Na. 356 ya mwaka 2018 ambayo hukumu yake ilitolewa Juni, 2020. Mfugaji mmoja, ng’ombe wake walikamatwa halafu alishinda kesi zote mpaka Mahakama ya Rufaa lakini mpaka leo bado hajapata haki yake na hili Mheshimiwa Waziri analifahamu kidogo kwa sababu alivyokuwa maliasili nadhani nililisema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii maana yake nini kwa mwananchi wa kawaida? Unapopelekwa Mahakamani na ukashinda kesi? Kwa mwananchi wa kawaida kabisa wa kijijini kule Orkesumet kule, anatamani akae nyumbani Serikali imletee ng’ombe wake ama fidia; kwa sababu ameshashinda. Hii ya kukaza hukumu sijui na kufanya nini, hizi ni kazi za mawakili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nia ya Mheshimiwa Rais ni kwamba Watanzania wapate haki zao. Sasa nilikuwa naangalia kesi hii utashangaa sana, ng’ombe wamekamatwa walikuwa mia mbili takriban na sitini na tano, wamekaa miaka mitatu wakati wa kesi, wako Mahakamani. Siku wanashinda Mahakama ya Rufani wale Waswahili wamekwenda wamepiga hesabu wakakutwa na ng’ombe 96. Sasa wao wakachukua wale 265 toa 96 waliobaki halafu wakatengeneza fomu za ng’ombe wote wengine waliopotea, yaani 169. Mheshimiwa Attorney General na Mheshimiwa Waziri wa Sheria wawaambie hawa watu, law is not mathematics, it is about principles, it is about conformity, it is about justices. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mtu mmoja tu anaiingizia hasara Serikali. Ng’ombe wamepotea, mwananchi hana na hivyo Serikali itashtakiwa, halafu kuna mtu mmoja tu amefanya haya. Sasa Mheshimiwa Attorney General utashangaa sana; nilikuwa naangalia wametengeneza kitu kinaitwa livestock deaths certificates ya wale ng’ombe 169. Sasa hii fomu hii kwa mara ya kwanza na mimi ni mfugaji, napata magonjwa ya ng’ombe hapa ambayo sijawahi kuyaona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, history of sickness anasema high fever. Sasa sijui ni malaria? I don’t know. Halafu treatment given anaandika given, hapo kaishiwa. Kwa sababu if you produce documents 169 sasa itafika mahali utakuwa una-reproduce hata maswali yaliyoandikwa hapo. Treatment given anasema given, fomu nyingine unachukua treatment given local. Halafu hawa ni watu wa Serikali, halafu wapo na wameandika majina yao hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Attorney General na Wizara ya Katiba na Sheria, I think it should be fair tusimamie utawala wa sheria na wale wanaotuchezeachezea we must take them to task. Haiwezekani, yaani Serikali nzima ama Wizara nzima, hawa wote, all of us, hata sisi tunaotunga Sheria hapa tuonekane hatusimamii eti kwa sababu kuna mtu mmoja tu ambaye ni mvivu, anafikiri sheria ni balance sheet, kwamba unachukua ng’ombe 265 unatoa 69 halafu unasema wengine wamekufa, haiwezekani!

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Tume ya Haki za Binadamu. Tume ya Haki za Binadamu ni Tume ya kikatiba na ni muhimu sana kwa nchi yetu. Tuiwezeshe, ipate fedha za kutosha ili iweze kufanya kazi zake. Kama ilivyokuwa envisaged na Katiba article 129 na 130, walete ripoti hizi tuwe tunaziangalia na ku-debate hapa, nadhani itakuwa ni muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya DPP nia yao ni kwenda kila wilaya ili haki isimamiwe. Sasa, hatuwezi kuwataka waende huko kama tusipoweka resources za kutosha ili waajiri watu wa kutosha na sheria zisimamiwe vizuri sana. Sasa tunazungumza habari ya sijui ni 16% ya watumishi wanaotakiwa ndio walionao. Tume-progress kwa sababu miaka miwili, mitatu iliyopita ilikuwa ni 10%. Ina upungufu mkubwa sana na hakuna namna nyingine yoyote, ni kuwezesha resources hizi zipatikane ili waweze kusimamia sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na Program ya Mama Samia Legal Aid. Sisi tunamshukuru Mheshimiwa Waziri kwa sababu Manyara ilikuwa kati ya Mikoa na Kiteto ilikuwa beneficiary wa programu ya Mama Samia Legal Aid. Wamekwenda vijiji vingi sana na tuliona manufaa ya Mama Samia Legal Aid. Watanzania wanahitaji na ndiyo maana hata tukiwaona kwenye mikutano ya wanasiasa ama ya siasa huko Watanzania wamejaa na wanalalamika sana. Kwa hiyo hii programu ya Mama Samia Legal Aid pengine ingesaidia kupunguza matatizo ambayo Watanzania walio wengi wanayo huko majimboni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna wakati nilizungumza hapa kuhusu ng’ombe kutozwa laki moja kwa kichwa na Wizara ya Maliasili na Utalii. Hii Wizara Mheshimiwa Dkt. Ndumbaro alikuwa ni wakili, Mheshimiwa Mchengerwa wakili, Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana ni wakili na sasa Mheshimiwa Angellah Kairuki ni wakili. Halafu kuna watu tu wanakaa kaa tu huko, wanafikiri ni mathematics tu, halafu wanatoza shilingi 100,000 kwa kichwa cha ng’ombe ilhali hakuna hata sheria moja inayo-support.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulizungumza sana hapa na Mheshimiwa Attorney General na Mheshimiwa Waziri Mkuu pia alitoa ripoti hapa, akasema nendeni huko. By the way, Tume ya Haki za Binadamu nao wameandika ripoti yao na wamesema this is illegal. Sasa huyu ni nani anayefanya mathematics tu? Tulizungumza hapa na Bunge lilisema kuhusu mwisho wa faini minimum na maximum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa siku hizi wamekuja na njia nyingine, Desemba mwaka jana wananchi wangu waliwakamata. Sasa kwa sababu wanajua maximum ni ten million wanawalazimisha watu kugawa ng’ombe kwa makundi mawili ili wa-impose fine ili hata kama ni mtu mmoja ndiye analipa, analipa milioni kumi kwa milioni kumi. Law is not about mathematics, Mheshimiwa Attorney General we need your authority.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, Mwenyezi Mungu awabariki na naunga mkono hoja. (Makofi)