Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, tunaipongeza Serikali ya Mama Samia kwa kuendelea kutenga fedha kwenye bajeti kwa ajili ya ununuzi wa korona tano tangu Mwaka wa Fedha 2022/2023 hadi kwenye bajeti hii ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 pamoja na kukarabati korona iliyopo shamba la Kibaranga, Wilayani Muheza kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wadogo.

Mheshimiwa Spika, pamoja na juhudi hizi za Serikali kuwasaidia wakulima wadogo, nasikitika kuwa ukarabati wa korona ya Kibaranga umefikia 80% na kinachokwamisha kuanza kazi ni uunganishaji wa umeme wa TANESCO ambapo miundombinu yote ya umeme ipo tayari, lakini kuna urasimu wa kufanya maunganisho. Namwomba Mheshimiwa Waziri aingilie kati uunganishwaji wa umeme na ikiwezekana Mawaziri wa Kilimo na Nishati wasaidie kuwaondoa wakulima katika mkwamo huo.

Mheshimiwa Spika, pamoja na juhudi kubwa za Serikali kuwasaidia wakulima wa mkonge nchini, kumekuwa na uanzishwaji wa tozo na kodi mbalimbali kwa wakulima bila kufuata taratibu na katika hali inayokinzana na sheria mama za fedha. Kumekuwa na tozo ambazo hazina tija moja kwa moja na uzalishaji wa mkonge, kwa mfano tozo ya zimamoto na kukitokea moto hawafiki kusaidia. Tozo ya OSHA ambayo hutozwa kiwango kikubwa kwa kupima kila mfanyakazi bila kujali wafanyakazi hao wamelipiwa bima ya afya au laa. Serikali ione namna ya kusawazisha au kuziondoa kabisa.