Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
ACT
Constituent
Konde
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. MOHAMED SAID ISSA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia katika bajeti ya Wizara hii ya Uchukuzi. Kwanza leo nimefurahi upo hapo kwa sababu naamini dakika zangu nitazipata zote kwa sababu wewe ni mlezi wa wana kweli kweli. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kukipongeza Chama changu cha ACT-Wazalendo kwa kutimiza miaka 10 toka kuanzishwa, lakini kutimiza miaka kumi bila migogoro, lakini kuwa ni chama ambacho kinakua kwa kasi sana, ni chama ambacho kitakuja kuiondoa CCM madarakani. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Spika, naanza kuchangia sasa. Kwanza naanza na suala la uwekezaji wa kampuni binafsi katika Bandari yetu ya Dar es Salaam. Ni jambo jema sana…
MHE. HAMISI S. TALETALE: Mheshimiwa Spika, Taarifa.
SPIKA: Mheshimiwa Mohammed subiri kidogo, kuna Taarifa. Nani anasema Taarifa?
MHE. HAMISI S. TALETALE: Mheshimiwa Taletale.
SPIKA: Mheshimiwa Hamisi Taletale.
TAARIFA
MHE. HAMISI S. TALETALE: Mheshimiwa Spika, nampa Taarifa muongeaji, inawezekana akawa anaota, aamke. Hakuna chama kinachoweza kukitoa Chama Cha Mapinduzi madarakani. (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Mohamed, umeipokea Taarifa hiyo? (Makofi)
MHE. MOHAMED SAID ISSA: Mheshimiwa Spika, Taarifa yake siipokei kwa sababu, hata yeye aliota kuja kuwa Mbunge na leo ni Mbunge kwa hiyo, chama nacho ni hivyo hivyo. Siipokei. (Kicheko)
Mheshimiwa Spika, naendelea na mchango wangu, tena sijui mnapata tabu ya nini, mimi nawapongeza. Ni very rare kumkuta mpinzani anapongeza, lakini kwa vile nimeona kuna jambo zuri, nawapongeza.
Mheshimiwa Spika, kuna hili suala la uwekezaji wa kampuni binafsi katika Bandari yetu kutoka Gati Na.1 mpaka Na.7 pale. Kwa kweli, jambo hili nimekuwa nalifuatilia kwa ukaribu nimeona kwamba, hii kampuni ambayo imepewa, naamini itakuja kuiokoa nchi hii.
Mheshimiwa Spika, nakumbuka wakati tunaleta mijadala ya kumweka DP World Mheshimiwa Waziri wa Fedha alisema kuwa, hii inakuja kuchangia 62% ya bajeti yetu. Sasa Watanzania tunataka nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaona hapa Mwaka 2023 makasha 600,000 ndiyo ambayo yalikuwa yanapata huduma, lakini sasa hivi yamefikia makasha 800,000. Ni jambo jema na ni jambo la kupongeza.
Mheshimiwa Spika, tuna imani kwamba, ikiingia kampuni binafsi haya mapato yatakuja kufikia kama alivyosema Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Kwa hiyo, jambo hili ni jambo jema, tumuunge mkono Mheshimiwa Rais ili awatumikie Watanzania. Pia, nasema kwamba, kwa sifa nilizoziona hawa DP World natamani wafike Zanzibar ili waende wakahudumie Bandari za Zanzibar. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naacha sehemu hiyo, nakuja kwenye mizigo inayotoka Zanzibar kuja Tanzania Bara. Jambo hili linawakwaza Wazanzibari ama wafanyabiashara wote kwenye upande wa wharfage. Utaratibu ambao una-charge wharfage kwenye mizigo inayotoka Zanzibar tunaona kwamba, siyo sahihi.
Mheshimiwa Spika, tunawashukuru wenzetu wa TRA wao wana differential tax. Maana yake ni ukilipia tax kule Zanzibar ambako tunalipa half of ile duty, ukija hapa unalipa tofauti yake. Hata hivyo, hawa upande wa wharfage mpaka leo wameshindwa kuwasikiliza wafanyabiashara wanaotoka Zanzibar, kwa nini? Kwa hiyo naomba Wizara hii ilichukulie serious jambo hili ili hii wharfage ipungue kwa wale wenye mizigo inayotoka Zanzibar. Hata hivyo, pamoja na hayo sisi watu tunaotoka Zanzibar ambao tunaleta biashara zetu Tanzania Bara tuna jambo lingine ambalo linatusumbua, hili ni jambo la storage.
Mheshimiwa Spika, storage kwa mizigo inayotoka Zanzibar inapewa 24 hours, lakini kwenye charge inakuwa charged sawasawa na ile charge iliyopo kwenye sheria. Jambo hili ni la kutungiwa Kanuni tu kwa sababu, hii mizigo ni loose cargo. Tunaweza tukapunguza wharfage, lakini wakati huo huo saa 24 hazitoshi.
Mheshimiwa Spika, nimezungumza na Wabunge wengi humu, wakiwemo wa CCM, wamesema leo watanisaidia kushika shilingi kwa hiyo, nitashika shilingi, sawa eeh? Nitashika shilingi kwa hili kama Waziri hatatoa kauli ya kuwasaidia wafanyabiashara kati ya Zanzibar na Tanzania Bara. Hili jambo siyo sahihi. Haiwezekani watu wanaotoka nchi za jirani wanaopitisha hapa wanapewa siku saba, siku 14 hadi siku 21, halafu sisi watu wa Zanzibar, nchi ambayo tumeungana kwa Muungano wa mfano, leo tunaonekana mzigo ni saa 24 na charge ni ileile. Namwomba Mheshimiwa Waziri na timu yake waliangalie jambo hili ili kuwapa comfort Watanzania wote. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naendelea na suala la hizi meli za abiria. Sasa hivi meli za abiria zinafanya kazi nzuri sana hapa kwetu kati ya Zanzibar na Tanzania Bara, lakini jambo la kushangaza na kusikitisha ni hizi meli zetu hazina afisa wa afya au daktari mle ndani. Tunabeba abiria zaidi ya 600 kwa muda wa saa tatu, wanaingia wagonjwa na wazazi, lakini hakuna daktari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, siku moja imenitokea ambapo alitokea mzazi anataka kujifungua na ndani ya boti hakuna daktari, bahati nzuri nilikuwa nimefuatana na ndugu ambaye ni daktari nikamwomba aende akasaidie. Kama asingekuwepo ingekuwaje? Kwa hiyo, jambo hili namwomba Waziri alichukue ili kila boti au meli ya abiria, kuwe na afisa afya.
Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni suala la ma-container yetu ya biashara ya Zanzibar na Tanzania Bara. Kipindi cha nyuma ma-container yalikuwa yanapitia Kenya yanakuja Zanzibar. Sasa hivi tumekuwa tunaleta ma-container hapa Dar es Salaam, tunafanya transshipment kule, ili kupeleka Zanzibar. Jambo la kushangaza ni kwa nchi nyingine transshipment gharama zinakuwa chini, lakini kwa sisi Wazanzibari gharama ziko juu, sijui ni kwa nini?
Mheshimiwa Spika, lingine ni kwamba, ukishafanya assessment ya yale ma-container kwamba, yanakwenda Zanzibar yanapangiwa kwenda ICD ili kuongezewa gharama na muda, mwisho wake unakutana na vikwazo vingi. Jambo hili siyo sahihi. Tunaiomba Wizara ya Uchukuzi kwa upande wa TPA waliangalie hilo na wasiyapangie haya ma-container yanayokwenda Zanzibar kuyapeleka ICD. Hii ni kero kwetu sisi na biashara zinakwama.
Mheshimiwa Spika, nataka kuzungumzia pia suala la usafiri na upepo huu uliotokea juzi. Huu upepo umeleta janga kwa sisi wasafiri wa kutoka Tanga kwenda Pemba na pia, nataka kuwapa pole wananchi wangu wa Jimbo la Konde. Boti ambayo walikuwa wameweka mizigo yao ilipotea mpaka Nchi ya Kenya na ile mizigo ikapotea. Hivi sasa hawana mtaji tena. Kwa nini Serikali mpaka leo inashindwa kuunda meli ambayo itatoa usafiri wa uhakika kati ya Zanzibar na Tanzania Bara ili kuepusha jambo hili? Hili jambo kwa kweli, linatakiwa lizingatiwe. Kuna wakati fulani nilisema na wananchi wa Tanga walinipongeza sana, siyo jambo la Zanzibar peke yake, ni jambo la nchi nzima.
Mheshimiwa Spika, naenda kwenye suala la kuwapa maisha rahisi wananchi, kwanza narudi kwenye TASAC. Hii TASAC nimeona kwenye Taarifa ya Kamati wamesema kwamba, haifanyi kazi vizuri, pia naunga mkono kwa sababu, hivi vyombo vyetu vilivyosajiliwa kati ya Bara na Zanzibar, kule Zanzibar kuna ZDMA na hapa kuna TASAC. Ukienda upande wa Zanzibar kuna sheria ambazo wanazisimamia vizuri, lakini ukija huku bara TASAC wamefanya ni chanzo cha uchumi, kila wakienda kwenye meli wanaikagua na kuitoza faini. Kwa nini wakati mwingine wasiweze tu kutoa maelekezo kwamba, boresha hiki na hiki? Wao wakishakagua wanatoza faini. Jambo hili siyo zuri. Tunamwomba Mheshimiwa Waziri hizi faini zipungue, wawe wanatoa maelekezo. Wao ni walezi na wazazi, sisi tuko tayari kushirikiana na wao kufanya biashara kati ya Zanzibar na Tanzania Bara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)