Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Spika, nianze kwa kuunga mkono hoja.

Mheshimiwa Spika, napenda kuishukuru Serikali kwa juhudi kubwa zinazofanyika katika uwekezaji kwenye miradi ya kimkakati, nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa namna anavyotekeleza majukumu yake, huu ni uwekezaji mkubwa sana ambao kukamilika kwake utaifanya nchi yetu kuongeza kasi ya ukuzaji uchumi.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa ushauri kuhusu utwaaji wa maeneo katika mitaa mitano ya Manispaa ya Ilemela yaani Myaa wa Kihili, Mhonze, Nyamwilolelwa, Shibula na Bulyanhulu ambapo mpaka sasa idadi ya wananchi imefikia 3,700 waliofanyiwa uthamini mpaka sasa katika mitaa miwili, je, itakapokamilika, ulikilinganisha na idadi ya watu 1,404 iliyokuwa imetajwa awali.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu ni vyema uamuzi wa awali wa kutwaa eneo la mita 700 kutoka eneo la njia ya kurukia ndege ulikuwa muafaka sana kwa sababu zifuatazo, kwanza kupunguzwa kwa eneo linalotwaliwa ingepunguza gharama kwa Serikali na idadi ya wananchi wanaotakiwa kuhama wangepungua sana. Mpaka sasa idadi iliyofikiwa ni zaidi ya mara mbili hata kabla mitaa yote haijakamilika kufanyiwa uthamini. Mtaa iliyofanyiwa uthamini mpaka sasa ni miwili bado mitaa mitatu idadi inaweza kuzidi.

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ni kuomba route ya ndege Mwanza – Dodoma na Dodoma hadi Arusha, na Dodoma - Mbeya - Dodoma ni vyema ikaanzishwa ili kuwapunguzia gharama wananchi.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.