Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Biharamulo Magharibi
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii pia ili niweze kuchangia katika Bajeti hii Kuu ya Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya wananchi wa Biharamulo, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa ziara aliyoifanya Mkoa wa Kagera, hususan Jimbo la Biharamulo. Mambo yetu mengi yamepata majibu live kabisa palepale, kwa hiyo tunampongeza na kumshukuru.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha na msaidizi wake na watumishi wote wa Wizara yake kwa bajeti nzuri inayojibu kiu ya Watanzania wengi, na hususan katika suala la kubana bajeti na hatimaye kuweza kupunguza matumizi ili hizo pesa zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuyasema hayo, mimi nitapenda kuongelea maeneo mawili tu. Eneo la kwanza litakuwa ni lile suala la kubana pesa katika eneo la usafiri na eneo lingine litakuwa ni kwenye Sheria ya Manunuzi. Nikipata nafasi nitaongelea mambo ya regulatory authorities, kama nafasi itakuwa imebaki.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza na sehemu ile ya usafiri; nimejaribu kupitia document hii, maana kuanzia ukurasa wa 15 Mheshimiwa Waziri ameelezea jinsi ambavyo tutafanya saving ya pesa, na mimi naungana naye. Lakini caution yangu ni moja tu; haya magari tunapoyaondoa wapo Watanzania ambao wameajiriwa kama drivers. Ni lazima tuhakikishe tunalinda ajira yao. Tunawapeleka wapi; itabidi sasa Serikali ije na majibu. Kwa sababu walikuwa wameajiriwa, ni wafanyakazi wako kazini, tunavyofanya changes hizi sitegemei wale watu ambao unakwenda kuwakopesha magari na wenyewe watawachukua madereva wenu walewale waliokuwa Serikalini, ni lazima kila mmoja atafanya arrangement yake. Kwa hiyo tuangalie ajira za madereva hawa kwa sababu wana familia, wana watoto na watu wanaowategemea, tusiwakwaze katika hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimeangalia ukirasa wa 48; tunao mpango wa kununua ndege, ndege tano nadhani tumeshazilipia, moja ya mizigo. Nipongeze juhudi kubwa sana za Serikali ambazo zimekuwa zinakuwa applied kwenye Shirika letu hili la Ndege. Lakini nataka ku-declare interest; mimi kazi yangu ya kwanza nilikuwa cabin crew, nilifanya kazi Air Tanzania kama cabin crew, zamani kabla ya kuendelea na masomo na hatimaye nikarejea huko kwingine kama engineer palepale na hatimaye leo niko hapa. Kuna barua ambayo imetolewa na Shirika la Ndege la Air Tanzania kwa wafanyakazi, especially cabin crew. Cabin crew wa Air Tanzania wameambiwa waanze kujitegemea usafiri wa kufika kazini kuanzia tarehe 08, Julai. Sasa barua inasema kila cabin crew member atakuwa anapewa shilingi laki tano.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimefanya kazi ile ya ndege. Tunaweza tukaona wale watu wamekaa pale lakini hao ndio wanao-operate ile ndege. Maana bila wao ndege haitaweza kuruka pale. Unapomwambia mtu unampa shilingi laki tano akatafute usafiri, laki tano ni shingapi?
Mheshimiwa Naibu Spika, utampa mtu pesa leo, ndani ya siku 15 pesa imeshakata, wataanza kuja na bodaboda wale watu ile asubuhi watakabwa njiani. Na anaponyanyuka cabin crew member ananyanyuka na passport na leseni zake zote, akiibiwa mmoja au wawili ni hasara. Kwa hiyo ninaomba tuliangalie.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwa sababu huku Waziri amesema wale ambao wako entitled kupewa magari watakopeshwa magari na Serikali, sasa nina wazo; sidhani kama Shirika la Air Tanzania linao uwezo wa kununua magari yote kwa ajili ya cabin crew. Lakini as long as wamesha-declare kwamba wataweza kuwapa shilingi laki tano kila mmoja, basi Wizara ya Fedha ikae na Air Tanzania; kama inawezekana hawa vijana wakopeshwe hata ni IST tu ya milioni 12, wakopeshwe, wawe wanakatwa kwenye ile allowance ya magari ambayo wameambiwa watapewa, hatimaye waweze kupata usafiri wa kuwafikisha kazini, wafike salama na hatimaye warejee salama. Vinginevyo ndege hizi mnazonunua zikianza kupata delays pale wateja watawakimbia, kwa sababu kila anayesafiri na ndege ana ratiba yake. Kwa hiyo ninaomba hili niliweke hivyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikirejea katika Sheria ya Manunuzi. Nimeona hapa kazi kubwa ambayo Waziri ameiongea, kwamba tunataka tufanye saving. Lakini kuna neno hapa ambalo amelitumia zaidi, kwamba kumekuwa na ishu ya upangaji wa bei, kwa hiyo tunataka tuangalie jinsi ya kupunguza na tuwe na bei ambazo ni elekezi kwa kifaa fulani na kifaa fulani.
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nina uzoefu sana kwenye hivi vitu, especially unapoenda kufanya technical procurement. Leo kwa mfano unataka kununua excavator, kuna excavator ya China, kuna excavator ya Caterpillar na excavators nyingine; utakapotaka kupanga kwamba tuwe na bei elekezi, hizi mashine zinatoka nchi mbalimbali na zina quality tofauti, huwezi kuwa na bei elekezi kwenye hili jambo; na tutatengeneza wizi mpya. Mimi nikishajua naleta mashine ya Kichina, labda excavator ya Caterpillar ni dola 180,000 yangu mimi ni dola 120,000, nitapandisha bei itafika 165,000 as long as najua sijavuka pale, tutaanza kuuziwa hivi vitu kwa bei ya ajabu.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninachoomba, kama wafanyakazi wetu tunashindwa kuwa-control tutafute mechanism nyingine. Sidhani kama sheria ina shida, shida iliyopo ni hawa hawa watu wanaotuhudumia huko. Hata ukibadilisha sheria kesho ni hao hao watakuja na mambo mengine.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ninachoomba ni kwamba vitu kama restricted tendering, vitu kama single source, hivi ndivyo vitu ambavyo vinasababisha matatizo yote haya. Kwa nini nayasema haya; nime-refer hapa kwenye hotuba ya Waziri, ukurasa wa 44 wa hotuba yake amesema Serikali imeanza mchakato wa kutafuta mkandarasi wa kujenga kipande cha Tabora – Kigoma, kilometa 514 kwa dola bilioni 2.1.
Mheshimiwa Naibu Spika, dola bilioni 2.1 nimekwenda kuzi-convert hapa kwenye shilingi. Baada ya ku-convert kwenye shilingi ni sawa sawa na shilingi trilioni nne na bilioni 851 kwa rate ya 2,310. Hili jambo limekuwepo hapa; lakini niki-refer kwenye system ya TANePS, iko hapa, nimeifungua iko live, I can declare it here. Uki-refer kwenye system ya TANePS kwa sababu hapa Waziri anasema mchakato umeanza, lakini unapoingia kwenye system ya TANePS walifanya single source ya hiki kitu. Ukifungua CCECC ambaye ame-single yeye peke yake ana trilioni sita bilioni 698.
Mheshimiwa Naibu Spika, difference ni nini; difference kati ya Waziri anachokisema hapa na yule ambaye tayari amesha-tender kwenye system ni trilioni moja milioni 847; difference. Waziri anasema 2.1 billion ambayo ni sawasawa na 4.8, lakini aliye-tender kwa single source na trilioni sita; difference ya 1.845 trillion. Hapo huwa tunaanza na sala na tunasema Mungu atusaidie kufanya maamuzi kwa walio wengi. I don’t see kwamba hapa kuna maamuzi ya walio wengi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ninachoomba, hili jambo tulichukue. Kwa sababu Waziri amesema ni hivyo na mchakato unaendelea, yule ambaye ame-tender kwa single source ana asilimia 38 extra zaidi ya ile ambayo Waziri amesema. Hata ukisikia mtu ana-negotiate unaweza ukashusha asilimia 38? Sidhani. Tumekuwa kwenye biashara wote na wote tunajua.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ninaomba hili jambo kama Taifa na kwa maslahi ya wengi, tuliangalie, tusije likatuangusha. Kwa sababu kinachoonekana hapa, huyu mtu kama hata alikuwa anatengeneza faida biashara za billions of money, you can’t put a profit of more than 15 percent.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo huyu mtu kama estimate ya Serikali inatuambia ni 4.8 trillion, yeye ana 6.6 trillion, hata uki-negotiate naye ashushe ile asilimia 38 bado ana profit kiasi gani mule ndani akubali kufanya ile kazi; he’s not a fair business partner. Hawezi kuwa fair business partner wa extent hiyo halafu tukategemea tunakwenda kufanya naye kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ninaomba hili jambo Serikali iliangalie. Kama ni hiyo tender kwa kweli tui-revisit, tuweze kufanya kitu kikae open kwa sababu hizi restricted na hizi single source ndizo zinazoleta matatizo yote haya. Hili jambo nalisema kwa uchungu nikiona kwamba wote tunasimamia maslahi ya walio wengi.
Mheshimiwa Naibu Spika, hapa unaongelea bajeti za Wizara ya Miundombinu, Wizara ya Mifugo na nyingine, bado hazijatosha tukiunganisha Wizara tatu. Kwa hiyo ninaomba kama inawezekana, kwa sababu Mheshimiwa Waziri amelitamka mwenyewe humu, a-revisit hiki kitu, kama inawezekana mchakato uanze upya ili tuweze kupata hiki kitu kwa bei ambayo Waziri ameitamka humu. Kwa sababu kama Waziri ametamka 2.1 billion tukaja kufanya hii kazi kwa 6.6 I don’t think kwamba itakuwa ni sawa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ya muda; naona umeshawasha mic hapo; mimi naomba niishie hapo, niunge mkono hoja. Lakini nilisema; naangalia muda wangu hapa, bado nina dakika moja, maana na mimi nilikuwa nime-set hapa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukurasa wa 150 wa bajeti ya Waziri amesema wanategemea kufanya changes kwenye Sheria ya Mawasiliano. Lakini kitu kimoja ambacho nataka nim-caution Mheshimiwa Waziri; hatuwezi kupeleka kila kitu TBS. Maana imefikia hatua kila tunapokuja humu tunarundika TBS; kukagua magari nje ya nchi TBS, kufanya hivi TBS. TBS wana uwezo gani?
Mheshimiwa Naibu Spika, leo unawanyang’anya TCRA kazi ya kukagua vitu vya kwao na kuunda regulations zao unataka upeleke TBS. yaani nitoke mimi TCRA ninayoijua taasisi yangu vizuri nikajifunge au nikaondoe Sheria ya TBS. Sidhani kama hiki kitu kiko sawa. Kwa hiyo ninaomba tukiangalie, amendment hii kwenye Finance Bill nadhani nitakija kuichangia vizuri ili tuweze kuisaidia Serikali…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
NAIBU SPIKA: Ahsante.
MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naunga mkono hoja