Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa fursa hii ya kuwa mchangiaji wa kwanza kwenye hoja iliyoko mezani, hoja ya Bajeti Kuu ya Serikali. Kwanza nitaanza kwa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya. Kipekee nishukuru sana kwa kipindi hiki cha mwaka wa fedha unaoenda kukamilika, miradi mikubwa sana ikiwepo miradi ya barabara, maji, elimu imefanyika ndani ya Jimbo la Kwela na wananchi kweli wana imani kubwa na Mheshimiwa Rais wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo leo nitalisemea, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Fedha, Naibu na watendaji wake wote ndani ya Wizara na alipokuwa akitoa hotuba yake hapa ndani ya Bunge siku ile kuna mahali nilimsikiliza sana kwa makini hasa pale alipoongelea juu ya matumizi mabaya na ubadhirifu wa fedha za umma. Katika kipengele hiki niwapongeze Serikali kipekee kwa kumpa uwezo CAG kwa kumwongezea bajeti kadri yeye alivyoomba. Jambo moja analofanya CAG wakati wote hata alipokuwa na upungufu wa bajeti, amekuwa akifanya kazi kubwa, shida moja imekuwa CAG ana-table ripoti, lakini sisi ambao tunatakiwa tu-take action tunakuwa hatutimizi wajibu wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu CAG tuliyemwongezea uwezo kwa mfano, ndugu yangu Mheshimiwa Waziri wa Fedha katika vipengele vichache tu ameona jinsi tulivyokuwa hatuko makini katika usimamizi, hasa ulipaji wa fedha kwa wakandarasi hasa kwa fedha zile ambazo tunakuwa tumezikopa au tumezipata kutoka kwa wafadhili. Nitakupa mfano mdogo tu, TARURA na TANROADS kulingana na ripoti ya CAG tumelipa penalty za Shilingi Bilioni 69.5, kwa sababu tu ya uzembe wa watu kufanya malipo kwa wakati. Sasa najiuliza maswali ni uzembe wa makusudi au kuna janja janja inafanyika kwamba wanachelewesha malipo ili interest baadaye tuje tugawane? Nimeyasema mara nyingi, nimechukulia pia mfano ATCL, TANROADS na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, taasisi tu tatu hizo tumelipa interest ya Shilingi Bilioni 95.5 kama penalty ya ucheleweshaji wa malipo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa taasisi chache tu hizi sijaenda kwenye Idara za Maji na sekta nyingine nyingi, fedha za penalty tulizolipa tu kwa hizi taasisi chache ni Shilingi Bilioni 165. Tunapoongelea kubana matumizi maana yake ni nini? Tuanze na mambo haya tuyachukulie hatua ya haraka, kuna system ya malipo ile ambayo ipo pale chini ya Hazina D-funds system, ina-approve level 16, zile ni unnecessary ni wastages, ndio zinatupelekea kwenye matatizo yote haya. Waziri akakae na wataalam wa Wizara ya Fedha waangalie namna ya ku-narrow down hizo level for approval, zibaki hata approval tatu. Kwa sababu, kama mtu amefanya kazi verification imefanyika na ma-engineer fedha ziko Hazina, kwa nini wa-attract interest na penalty za mabilioni ya fedha ya Watanzania? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe Mheshimiwa Waziri kauli yake ile aliyoisoma ndani ya Bunge na hata facial explanation yake ilionesha kwamba tutawakamata, tutawashtaki, tutawafunga akaithibitishe kwa vitendo na amerudia mara tatu hiyo kauli, tutawakamata, tutawashtaki na tutawafunga. Kwa imani yangu nambari tatu inamaanisha utimilifu. Maana yake mtu huyu anaongea jambo ambalo ana uhakika nalo. Kwa kilatini tunasema quod metus maana yake ni jambo lililo timilifu. Namwomba sana Waziri wa Fedha, hili jambo tukiliona tena mwakani tutaona kweli amefanya deliberately (makusudi) ili kuruhusu watu wakapige fedha za Watanzania. Fedha ambazo Mheshimiwa Rais anatafuta kwa jasho, anazunguka huko kote kutafuta fedha, halafu wanakuja kuzipoteza kirahisi tu bila hata justification yoyote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo nishukuru tena ni miradi waliyotuwekea, kwa mfano, kwa Mkoa wa Rukwa nashukuru grid ya Taifa ipo pale ambayo tumelia kwa muda mrefu, lakini commitment waliyoonesha kwenye bajeti kwamba ndani ya muda huu mfupi kwenye utekelezaji wa mwaka huu wa fedha watajenga meli mbili ndani ya Lake Tanganyika. Sisi tunachowaombea wakatekeleze kazi tutawapitishia bajeti kuu hapa. Tulipiga kelele Wabunge wa Mkoa wa Rukwa, Katavi na Kigoma wametuambia kwenye bajeti wenyewe wanakwenda kuleta meli mbili. Kwetu zile meli sio anasa zinakwenda kufanya transformation ya uchumi ambao wananchi wetu wa hii mikoa ime-paralyze, mapato yameshuka kwa sababu ya kukosekana kwa vitu muhimu kama hivi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ninalomsifu Waziri na nimshukuru sana Mheshimiwa Rais wamepandisha bajeti kwenye Sekta ya Kilimo Shilingi Bilioni 758.3. Hii ni one tier, the second tier lazima tuwe na component ya value addition kwenye kilimo. Utaweka Shilingi Bilioni 751 unaweza kukuta mmekuwa detained mkawa tu ni raw materials producers, lakini mnachohitaji ni namna mnavyojipanga kufanya value addition katika kilimo. Hapa Waziri hakwepi kwenda kuwezesha DFI zetu ninaposema DFI ni Development Financial Institutions ambazo tunazo mbili. TIB Development na Tanzania Agricultural Development Bank, zote hizi zimepita katika misukosuko mikubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na TIB Development wamekuwa na promise nyingi katika kuiwezesha hii benki implementation has been easier said to than done. Nitatoa mfano, nilikuwa napitia Mpango wa Miaka Mitano wa Pili ule waliji-commit kwamba wataweza kui-capitalize hii benki kwa Shilingi Trilioni moja. Mpaka ninavyoongea muda huu wameweza kupeleka Shilingi Bilioni 67 sawa na asilimia saba miaka yote hii. sasa tunakwenda wapi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ili tuje tuweze kupata production sector ambazo zinaweza kwenda ku-add value kwenye kilimo, benki zetu kubwa tunazoweza kutegemea ni hizi development; TIB Development na Tanzania Agricultural Development Bank. Mwaka 2014 bado Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba waliji-commit kwamba kila mwaka wataipelekea TIB Development Shilingi Bilioni 30 na lengo lilifika kwamba watakapofika mwaka 2023, watakuwa wamepeleka Shilingi Bilioni 270. Mpaka leo ninavyoongea hata senti moja hawajapeleka kwenye benki hii. Situation ni mbaya, maana yake sisi tunakimbilia tu kwenda kufanya financing kwenye financial institution ambazo ni za nje, its good, lakini tungeweza ku-fund hizi benki hii mikopo mingine tungeweza kuichukua kwenye benki zetu za ndani; na maana yake tungeweza kuzuia kitu kinaitwa capital flight ambayo sasa kwa kufanya hiyo mikopo ya nje tunapelekea capital flight yetu na haitusaidii sana kama Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwombe sana Dkt. hawa watu TIB Development wameomba fedha kwenye Benki ya BADEA ya Falme za Kiarabu 10 million USD, tayari wale wamesha-commit 5.5 billion wametuletea. Tangu mwaka 2017 Bilioni 7.5 hawaja-approve zitoke, maana yake mmepelekea tuanze kupata commitment fee, tunalipa penalty. Tumelipa mpaka sasa hivi zaidi ya Dola za Kimarekani 60,000 na kitu, tunalipa penalty bure wale wanasubiri, hatuja-withdraw kama tunataka fedha zile au hatuzitaki? Hii ni burden kwa Watanzania na unaposema kwamba tukabane matumizi, hayo ndio matumizi ambayo tunalipelekea Taifa hasara. Kwa hiyo, nimwombe Waziri hivi vitu wakaangalie namna ya kwenda kumaliza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia benki hizi kuna namna nyingine ambayo tunaweza tukazi-finance. Kama Serikali wameshindwa kupeleka Fund, wameshindwa ku-finance kwa mtaji wa ndani, wameomba ombi la kufanya cooperate bond kuuza; na mteja wao wa kwanza ni Mashirika yetu kama PSSSF na Insurance Companies ambao watachukua takribani Shilingi Bilioni 135. Tuwaruhusu wakafanye hivyo ili wa-capitalize ile benki iwasaidie Watanzania, failure to do so tunaweka vitu vingi, hatuwezi kuvifanyia kazi. Hata hii TIB, Benki ya Kilimo namshukuru Mheshimiwa Rais sasa kutoka Shilingi Bilioni 60 sasa amepeleka zimefika Shilingi Bilioni 268. Issue iko hapa ile benki inahitaji core-capital ambayo walau huwa tunachezea Trillions ili Bilioni 751 hii waliyoiweka iweze kufanyiwa reflection. Hamuwezi mkaenda kutengeneza irrigation system kubwa halafu production ya ile irrigation itakuwa nini, lazima kuwe na benki itakayowa-finance wale watu watakao-operate zile irrigation systems, rather to do so brother tutafeli. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwombe tu Waziri, very soberly, tuangalie namna ya kurudi tutafute solution ya benki zetu hizi mbili ambazo ni Development Financing Institution na ndio engine ya development katika Taifa lolote lile. Waziri anajua amefanya research mahali pote anajua namna zinavyo-operate, tuwaachie wataalam watuletee mawazo, wanasema tukipeleka benki guarantee tutakwenda kupelekea deni la Taifa likawa sio himilivu. Iko hivi, namshukuru juzi nimemsikia Mheshimiwa Bashe amekwenda kwenye Benki hii ya BADEA ya Uarabuni amechukua fedha, badala ya kuzileta moja kwa moja kule kwenye project, tuzipitishie kwanza kwenye benki zetu hizi za kilimo, halafu kutoka kwenye benki zile ndio ziende kwenye hizo projects. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, impact yake itakuwa kubwa, kwanza tutakuwa tume-revive benki zetu, lakini pia tutakuwa tume-contribute katika kukuza uchumi wa wananchi wetu. Niombe sana Mashirika mengi yana-operate under negative core capital, hatuna sababu, kama Serikali hatuwezi kuya-capitalize hayo mashirika ya umma, tuyafute yanayoendeshwa kwa hasara hayawezi ku-provide dividend Serikalini hayana maana tuyaondoe. Watanzania tuna mambo mengi sana ambayo yanahitaji kufanyika… (Makofi)
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Deus.
MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja. (Makofi)