Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mikumi
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia bajeti kuu na mpango huu wa maendeleo. Nianze kwa kumpongeza Rais wetu, Mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya pamoja na timu yake ikiongozwa na Waziri wetu wa Fedha pamoja na Watendaji wote Wizarani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo makubwa sana ambayo yamefanyika katika kipindi cha mwaka wa fedha tunamalizia. Katika Jimbo la Mikumi kuna mambo makubwa yamefanywa kwenye ujenzi wa miundombinu, upanuzi wa kiwanda pale Illovo, ujenzi wa vituo vya afya, ukarabati wa zahanati, ujenzi wa barabara katika maeneo ambayo hayafikiki. Haya yote yanaonesha commitment ya Rais wetu, Mama yetu Samia Suluhu Hassan katika kufanya rural transformation na rural empowerment. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti hii ni muhimu sana kwangu na kwetu. Kwa sababu wakati tunajadili bajeti hii, dunia inapita katika mabadiliko makubwa. Hali imebadilika, inflation tunasikia kila mahali kwa maana ya mfumuko wa bei. Bei ya bidhaa imepanda kila mahali na kuna uncertainty ambayo inaendelea katika maeneo mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna namna ambayo tunaweza tukasema kwamba changamoto na mabadiliko haya ambayo yanaendelea duniani yanaenda kupita. Kwa kifupi ukiangalia katika jicho la tatu, mabadiliko haya ambayo yanaendelea duniani, kisiasa na kiuchumi yanaendelea na yataendelea. Kama tutasimama kusubiria yaishe, hayaishi leo wala kesho. Ni suala la Serikali yetu sasa hivi kujipanga, kuona ni namna gani inaenda ku-fit katika mabadiliko haya ya dunia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, upandaji wa mafuta, upandaji wa mbolea, upandaji wa bidhaa na kuongezeka kwa gharama ya maisha. Changamoto hizi zinaenda kuendelea kwa muda mrefu kwa sababu wakubwa wetu ama wakubwa wa dunia hii ambao kimsingi wana-influence hata uchumi wetu hawaoneshi dhahiri kwamba wana nia ya kumaliza changamoto zao leo au kesho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, sisi ambao ni waathirika wa mabadiliko haya, tunapaswa kujipanga na bajeti yetu ijikite huko kuona ni namna gani tunaenda kujibu changamoto zinazotokana na mabadiliko ambayo yanaendelea duniani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kwa kusema kwamba, kama tunataka kuendelea ni lazima tujikite kwenye kuunganisha vijiji vyetu na miji mikubwa. Lazima tuangalie kila opportunity ambayo inaweza kutoa fursa kwa wananchi wetu kutoka katika hali ambayo wanayo kwenda kwenye hali bora zaidi. Katika hili naomba nisisitize umuhimu wa barabara ya Kilosa kwenda Mikumi kupitia Masanze, Zombo, Ulaya, Muhenda na Mikumi. Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa Mkoa wa Morogoro lakini uchumi wa Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tuna ujenzi wa reli ya mwendokasi, ni imani yangu reli hii pamoja na royal tour ambayo Mama yetu ameweza kuifungua nchi yetu katika soko zima la utalii inaenda kuongeza idadi kubwa ya utalii ambao wanaweza wakaja katika Mbuga ya Mikumi. Ni vema sasa tukaangalia barabara hii kwa jicho la tatu. Kwamba kama haitafanyiwa kazi, juhudi hizi ambazo zinazoendelea haziwezi kwenda kutupa matokeo chanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tuna mradi wa REGROW ambao unaenda kuangalia utalii Kusini, ni vyema tukaangalia mradi huu unaenda kubadilisha maisha ya watu wetu namna gani? unaenda ku-impact maisha ya watu wetu kwa namna gani? Kwa hiyo, ni vizuri tukafanya social welfare analysis kuona kwamba uwekezaji mkubwa unaenda kufanywa through REGROW, unaenda kubadilisha maisha ya wananchi wetu mmoja mmoja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ardhi. Ardhi ni mtaji, ardhi ni muhimu sana kwa nchi ambayo inaendelea. Lakini naomba nizungumze kwamba pamoja na kazi kubwa ambayo imefanywa katika kuendeleza ardhi zetu, kupima ardhi yetu. Kwa mfano, Mikumi tumepokea Shilingi Milioni 250 kupima viwanja zaidi ya 1,000 jambo ambalo ni mapinduzi makubwa katika Mji wetu Mdogo wa Mikumi. Jitihada hizi naomba ziendelee katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vema sasa pamoja na kupima kila eneo, lakini ni vizuri tuka-review kodi zetu. Kodi ambazo zimeambatana na ardhi si rafiki. Matokeo yake wananchi wengi badala ya ku-comply na sheria wamekuwa wa kwanza kukwepa. Katika hali ya kawaida wananchi wengi wa Tanzania ambao wananunua viwanja na nyumba, hawashawishiki kubadilisha umiliki wa awali na hawashawishiki kubadilisha umiliki wa awali kwa sababu ya gharama ambazo siyo rafiki katika ubadilishaji umiliki wa hizi document.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, katika Wilaya ya Kilosa, mashamba ambayo ni zaidi ya hekari 100 ambayo yamesajiliwa hayazidi matano katika mashamba mengi, katika hali hii Serikali inapoteza mapato mengi ambayo hayana sababu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la kilimo. Kilimo ndiyo uti wa mgongo, kilimo ni siasa, kilimo ndiyo kila kitu. Lakini ukienda katika mashamba mbalimbali ya nchi hii, ukiona shamba zuri basi shamba hilo linamilikiwa na mwekezaji ama shamba hilo linamilikiwa na Serikali. Shamba kwa mfano kama Mbigiri ni shamba jipya kabisa, tunasikia kwamba mwaka jana wameongeza hekta zaidi ya 700, wametengeneza mabwawa manne ambayo yanaweza yaka¬-host lita zaidi ya 1,700,000 za maji, mabwawa ambayo yanavuna maji na kuruhusu maji kuingia mashambani, mitaro mikubwa na mifereji ya kuingiza na kutoa maji kwenye mashamba, hii yote ni miundombinu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, unajiuliza mashamba haya ambayo ni ya Serikali yanatengenezewa miundombinu hii kwa nini wananchi wasitengenezewe miundombinu kama hiyo, halafu wakachangia kidogo kidogo? Kilimo chetu kimekosa tija kwa sababu hatuna mikakati lakini hatuna nia ya dhati ya kuangalia kila shamba la mkulima kama sehemu ya uzalishaji wa nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkulima wa Kitanzania ni yatima, mkulima wa nchi hii hana msimamizi. Ndiyo maana eneo la umwagiliaji katika nchi hii ni hekta zaidi ya Milioni 29. Lakini eneo ambalo tunalitumia kwa umwagiliaji ni hekta 727,000 ambayo ni asilimia 2.5 tu ya ardhi yote ambayo inafaa kwa umwagiliaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nini ambacho nataka kuzungumza? Ni muhimu kwa Serikali yetu kuona kwamba haiwezi kufanya kila kitu yenyewe, iwezeshe sekta binafsi katika kuendeleza ardhi na maeneo mbalimbali kutengeneza mashamba ya kisasa, mifereji na mabwawa ambayo yanaweza yakavuna maji na mwananchi akapewa maeneo katika block farming akalima na akagawa sehemu ya faida yake kwa Serikali kama sehemu ya kurudisha gharama za uwekezaji.(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukifanya hili tunaenda kukitendea haki kilimo chetu na kinaweza kwenda kuajiri wananchi wetu wengi ambao Taifa hili linawahitaji.
MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa.
MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ili haya yote tufanikiwe ni vizuri sana tuka-adopt innovative economy strategy ambazo tunaenda kuangalia nchi ambazo zina-image sasa hivi katika Baltic na Former Soviet Satellite kuangalia namna gani tunaweza kubadilishana teknolojia ndogondogo ili tuweze ku-promote kilimo chetu nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha. Naomba kuunga hoja. (Makofi)