Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Mohammed Said Issa

Sex

Male

Party

ACT

Constituent

Konde

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. MOHAMED SAID ISSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Naanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa kibali cha kuweza kusimama katika Bunge lako hili Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kwa kupeleka salamu za shukurani kutoka kwa wananchi wa Jimbo la Konde kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Katika Jimbo la Konde, vikosi vya KMKM Askari wake walipoteza silaha. Kadhia iliyowakuta wananchi wa Jimbo la Konde ni kukamatwa, kupigwa na kuzuiwa kufanya shughuli zao za kijamii ikiwemo kuvua na kulima. Namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais, Mheshimiwa Hemed Abdalla Suleiman na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa jinsi walivyolishughulikia suala hili likaweza kutulia kwa vile suala hili la kupotea silaha siyo suala ambalo lilikwenda kwa wananchi. Nawashukuru sana na salamu ziwafikie Mheshimiwa Waziri Mkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza kuchangia, kwanza ni kuhusu upatikanaji wa fedha za kigeni. Fedha za kigeni imekuwa ni suala gumu sana katika nchi hii kupatikana. Kwa kweli suala hili napenda linapokuja kuhitimishwa hapa tupate maelezo ya kina kwamba fedha za kigeni zinapatikana vipi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda benki unataka dola 1,000 hakuna, ukitaka dola 500 hakuna. Tunajiuliza, biashara zinafanyika lakini benki hakuna. Hii inaonesha kwamba kuna udalali wa fedha za kigeni. Kwa hiyo, hapa tunataka kujua kwamba je, ni BoT wanaofanya udalali huu au ni benki? Kwa sasabu biashara zinaendelea kama kawaida, lakini fedha za kigeni hazipatikani. Tunataka Serikali ituambie, je, fedha hizi za kigeni zinapatikana kwa njia gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, Zanzibar sasa hivi biashara imedumaa, lakini wenzetu huku Tanzania Bara makontena yanashuka kama kawaida. Hatuelewi ni lipi hapa liko nyuma ya pazia? Tunataka maelezo ya kina kuhusu upatikanaji wa fedha za kigeni. Ni nani dalali wa fedha hizi? La kwanza hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, napenda kuchangia suala la upungufu wa sukari. Upungufu wa sukari umekuwa ni jambo ambalo limetikisa nchi mpaka imeonekana Mheshimiwa Rais hafai, kumbe Mheshimiwa Rais anafanya kazi nzuri tu. Mheshimiwa Rais anafanya kazi nzuri ya kujenga nchi, kuwatumikia wananchi na kwa kweli anahitaji kupongezwa. Sasa jambo hili kwa kweli limeleta taswira mbaya katika nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaambia wahusika hawa wafanyabiashara wa sukari wame-switch tu tukifika 2025, hapo ndipo mtajua wamejipanga vipi. Nashauri sheria ya kuwapa vibali wenye viwanda ifutwe na iletwe sheria nyingine ambayo itaruhusu wafanyabiashara wote wenye uwezo waweze kuleta ama sivyo, hawa wafanyabiashara wenye viwanda wametengeneza syndicate ambapo wanaamua tu kulangua sukari. Kuna baadhi ya maeneo sukari ilifika shilingi 6,000 kwa kilo na wengine wameshindwa kupata sukari. Kwa hiyo, nashauri sheria hii haifai, irudishwe hapa Bungeni tuichakate ili mwenye uwezo yeyote aweze kuleta sukari kuondokana na tatizo hili ambalo limejitokeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni Bwawa la Mwalimu Nyerere; Bwawa la Mwalimu Nyerere limetengeneza disaster kule Rufiji. Mimi na-declare interest…